Boss la DP World
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 1,997
- 7,551
Utafiti wangu mdogo umebaini Watanzania wengi hawana urafiki na polisi, yaani ule urafiki kama wa mtu na mshkaji wake, mfano kupigiana simu kujuliana hali, kutembeleana, kubadilishana mawazo, kushirikiana katika biashara na kupeana michongo.
Mapolisi wengi wanakuwa na urafiki wao kwa wao na kwavile wengi hukutana kazini tu tena ukubwani, basi urafiki wao huwa wa juu juu tu. Vipo visa kadhaa vya askari polisi kuchukua hatua za ajabu kutokana na msongo wa mawazo.
Niliwahi kuzungumza na mkuu mmoja wa FFU katika mkoa fulani akaniambia anaongoza vijana walevi, wagomvi, wenye madeni na mzigo mkubwa wa familia, alinieleza vijana wake ni kama wanaishi kwenye dunia yao.
Nilivyo muuliza hatua gani huzichukua kuwasaidia akasema huwa anajitahidi kuwasaidia wale walio katika hali mbaya zaidi kwa kuwapangia malindo kwenye taasisi za fedha au sehemu nzuri nzuri ili wapate posho ya ziada, pia huwa anawafariji kwa neno la Mungu.
Anasema laiti raia wangekuwa na huruma na upendo kwa polisi huenda jamii ingefuta uhalifu.
Mnaonaje tukianza utaratibu wa kuwatembelea polisi kwenye kota zao, kupiga nao ma stori, kuoa watoto wao, mnadhani itapunguza hizi kelele huku mtaani?