Polisi watangaza vita Igunga: Ni baada ya kulalamikiwa kufanya kazi kwa upendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi watangaza vita Igunga: Ni baada ya kulalamikiwa kufanya kazi kwa upendeleo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 26, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  [h=3][/h]

  *Ni baada ya kulalamikiwa kufanya kazi kwa upendeleo
  *Walinzi CCM wadaiwa kumtwanga mwandishi wa habari
  *Habari zake zatajwa kumdhalilisha kigogo wa chama
  *Aliyepigwa CUF atoka hospitali, wahusika bado kunaswa


  Benjamin Masese na Peter Mwenda,Igunga

  SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi wilaya ya Igunga kulalamikiwa na vyama vya siasa vikiwemo
  Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na chama cha Wananchi (CUF) kushindwa kufanya kazi yake kama inavyostahili, sasa limejibu mapigo kwa kutangaza vita dhidi wakiukaji sheria na taratibu za uchaguzi.

  Jana jeshi hilo lilijitokeza na kueleza kuchukizwa na na vitendo vinavyojitokeza kila siku katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge, vikiwemo vya ukatili, uhalifu, mashambulio ya kudhuru, vitisho, udhalilisha na ulipizaji wa visasi.

  Pia limetoa onyo kwa vyama vya siasa, taasisi, wakazi na wananchi waliokwenda katika wilaya ya Igunga kwa shughuli mbalimbali kufanya kazi zao kufuata sheria na taratibu zilizopo, vinginevyo halitakuwa na huruma wala aibu pale watakapobainika kwenda kinyume.

  Hivi karibuni CCM na CHADEMA vilitoa malalamiko dhidi ya jeshi hilo kushindwa kuweka ulinzi katika mikutano yao ya kampeni na wakishindwa kuchukua hatua za haraka wanapopelekewa taarifa za uhalifu au uvunjaji wa sheria za uchaguzi.

  CCM ilidai kuwa polisi wamekuwa wakiacha kushughulikia taarifa wanazotoa kwao juu ya vitendo wanavyofanyiwa huku CHADEMA wakilituhumu kwa kujihusisha na masuala ya kisiasa.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) anayeshughulikia Oporesheni Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Telesphory Anacleth alisema kuwa kadri siku zinavyokaribia uchaguzi, ndivyo kunavyoibuka tabia mbaya na matukio yenye sura ya uvunjifu wa amani.

  SACP Anacleth alisema kutokana na vitendo hivyo sasa Jeshi la Polisi limesema limejipanga kuwashughulikia watu wanaokwenda kinyume na taratibu zilizowekwa pamoja kuvunja sheria na kujichukulia maamuzi ya papo kwa papo huku wakijua ni kosa kisheria.

  "Haijawahi kutokea ndani ya miaka yangu 40 kazini kupongezwa, na sitaki nipongezwe na wanasiasa, mimi nitapongezwa na bosi wangu hivyo wanaolituhumu Jeshi la Polisi Igunga kufanya upendeleo hawajui walisemalo," alisema.

  Aliongezwa kuwa kuna baadhi ya vyama vimekuwa vikitetewa katika uchaguzi, hivyo walitarajia itakuwa hivyo kila siku na kuwataka wanasiasa kufanya kampeni zao kwa kufuata sheria na sio kutegemea msaada wa kutoka polisi.

  Alisema hivi sasa Jeshi la Polisi limejiimarisha kukabiliana na matukio yanayojitokeza na kuvionya vyama vya siasa, wananchi na wakereketwa wa vyama hivyo kuishi kwa kufuata sheria za uchaguzi, vinginevyo watajikuta wakishughulikiwa na kukabiliwa na kesi.

  Bw. Anacleth alisema kuwa tangu kampeni zianze kumetokea matukio takribani sita ya kuzuru, uvunjifu wa amani, udhalilishaji, unyanyasaji, ulipizaji wa kisasi na mengineyo kama utumiaji wa risasi ambapo majalada ya matukio hayo yamefunguliwa.

  Alitaja baadhi ya matukio ni la kumwagiwa tindikali, Mkuu wa Wilaya Bi. Fatuma Kimario kufanyiwa vurugu na wafuasi wa CHADEMA, kukamatwa kwa watu wakijihusisha na ununuzi wa shahada za kupigia kura na wengine wakichana bendera na mabango ya wagombea, uchomaji wa nyumba na mengineyo.

  Alisema kuwa matukio kama hayo hayaleti sura nzuri ndani ya jamii na kwamba kuanzia sasa polisi haitakubali kupewa lawama ya kushindwa kudhibiti uhalifu na kukomesha matukio hayo.

  Alisema tayari polisi wamesambazwa na kuweka kambi kila kata wakifuatilia mwenendo mzima wa kampeni hadi siku ya kupiga kura Oktoba 2, mwaka huu.

  Wakati huo huo alitoa wito kwa waandishi wa habari kushirikiana nao ili kuwasaidia kutoa taarifa za ukweli kwani asilimia kubwa hushuhudia matukio yanayofanywa na wanasiasa.

  "Polisi tunaomba waandishi kufanya kazi yetu kwa ushirikiano wa karibuni kwani lengo ni kuimarisha miundombinu ya usalama, amani na utulivu katika kipindi hiki cha mchakato wa kampeni ili wananchi wapate fursa ya kutumia demokrasia kuchagua chaguo lao kwa hiari yao bila kushurutishwa," alisema.

  Hata hivyo, alionya waandishi kutojihusisha na siasa au vitendo vitakavyohatarisha amani na badala yake waelimishe jamii kupitia taaluma hiyo ili uchaguzi usipate dosari.

  Wakati huo huo, baadhi ya askari waliokuwa katika tukio la kurindima risasi usiku wamelieleza Majira kwamba wamechukizwa na kitendo cha mbunge wa viti maalum vijana kutoka Mara Bi. Bulaya kuwatukana na kutoa kauli chafu ambazo zilikuwa zikiwadhalilisha.

  Askari hao ambao hawakutaka kutajwa majina yao walisema kitendo cha kufokewa na mbunge huyo huku akiwauliza kama wanapenda kazi zao, kiliwachukiza na kuonesha kama yeye ndiye mwajiri wao.

  Alipotafutwa Bi. Bulaya kujibu tuhuma hizo alisema "by short this is wrong information, sio kweli, sikuwatukana wala kuwafokewa bali nilikuwa nawaeleza kuwakamata wahusika walioshambulia gari na kuvunja vyoo," alisema.

  Walinzi CCM watembeza kipigo

  Watu nane wanaosadikiwa kuwa walinzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamempiga mwandishi wa habari wa gazeti la Dira Mtanzania kwa kile kinachodaiwa aliandika habari za kukiponda chama hicho na kumdhalilisha Katibu wa Fedha na Uchumi, Bw. Mwigullu Nchemba.

  Akisimulia mkasa huo mwandishi huyo, Bw. Mussa Mkama alisema tukio la kupigwa lilimpata Jumamosi saa 1 usiku akiwa na mwenzake, Bw. George Maziku baada ya kumaliza mahojiano na Mbunge wa Viti Maalum, Bi. Ester Bulaya katika hoteli ya The Peak ambako wanakaa viongozi wa CCM.

  "Baada ya kumaliza mahojiano yetu na Bulaya wakati tukitoka getini niliwaaga walinzi nikiwambia sasa nimemaliza kazi yangu naondoka, mara niliitwa na mtu mmoja aliyevalia sare za CCM na baada ya kumkaribia nilizingirwa na kupigwa mateke na ngumi hadi kudondoka, hawakuishia hapo waliendelea kunipiga," alisema Bw. Mkama.

  Alisema mwandishi wenzake aliyekuwa naye Bw. Maziku akisaidiwa na mtu mwingine walifanikiwa kuwatuliza walinzi hao ndipo alipopata nafasi ya kukimbia na kwenda Kituo cha Polisi cha Igunga kutoa taarifa.

  Bw. Mkama alisema baada ya kutoa taarifa alikwenda hospitali ili kupata matibabu kutokana na maumivu mkononi, shavuni na sehemu za mbavu ambako walimpiga mateke hata baada ya kudondoka.

  Alisema mahojiano na Bi. Bulaya yalihusu tukio la mbunge huyo kudai kutupiwa risasi na Mratibu wa Kampeni za CHADEMA, Bw. Mwita Mwikwabe kwa kile alichodai CCM kuharibu mikakati ya chama hicho ya kukusanya shahada za kupigia kura.

  "Nadhani sababu kubwa ya mimi kupigwa ni zile habari zangu katika gazeti la Dira ya Mtanzania Jumatatu iliyopita likiwa na bahari mbili kubwa, ya kwanza ni ile ya 'CCM aibu tupu Igunga' ikieleza kufumaniwa kwa Mratibu wa Kampeni za CCM, Bw. Nchemba na nyingine ikisema kuwa 'CCM yakiri Rostam Kiboko'," alisema Bw. Mussa.

  Alisema katika tukio hilo amepoteza vifaa vya kutendea kazi yake na fedha taslimu sh. 450,000 ambazo zilikuwa katika pochi yake

  Mratibu wa Kampeni Bw. Nchemba alipoulizwa kuhusu walinzi wake kumpiga mwandishi alisema hana taarifa hizo, Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Igunga, alisema hajapokea taarifa za mwandishi huyo.

  Aliyepigwa CUF atoka hospitali

  Katika tukio jingine Mwenyekiti wa Wazee wa CUF, Bw. Salum Masanja ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Wilaya ya Igunga baada ya kudaiwa kupigwa na mabaunsa wa CCM waliokuwa katika msafara wa Katibu Mkuu wa UVCCM, Bw. Martin Shegela Jumanne iliyopita.

  Msemaji wa CUF, Bw. Silas Bwire alisema kiongozi huyo wa CUF aliyepigwa wakati akipandisha bendera ya CUF katika Kijiji cha Iyogelo kesi yake itasimamiwa na chama mpaka ukweli ubainike na wahusika waliompiga wachukuliwe hatua.

  CUF ambacho kiko katika kampeni zake za chini kwa chini, nyumba kwa nyumba na mikutano ya hadhara kimewataka wananchi wakichague kwa sababu ndicho pekee chenye kuhubiri amani kwa Watanzania wote bila kujali itikadi.

  Meneja wa Kampeni wa CUF, Bw. Antony Kayange alisema vyama vinavyowapiga viongozi wa vyama vingine wanachama wao na kumwagia watu tindikali wataendeleza visasi baada ya mbunge wa chama chao kuchaguliwa.

  Mgombea Ubunge wa CUF, Bw. Leopold Mahona alisema imefika wakati CCM iache madaraka kwa upinzani ili walete maendeleo kwa wananchi wa Igunga ambao maisha yao ni duni na ya kubahatisha.

  Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Julius Mtatiro akihutubia wananchi wa Igunga katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Sokoni mjini hapa juzi alisema chama chake kitachukua jimbo la Igunga kwa sababu kina mtaji wa kura 11,321 alizopata mgombea wao mwaka 2010 na kinakubalika kwa vwananchi kwa sababu hakina vurugu wala siasa za chuki.

  Alisema katika kampeni zao katika Kata 26 za Igunga wananchi wameahidi kuwapigia kura za ndiyo kwa sababu ya kuhubiri amani na utulivu kwa Watanzania.

  Mangula: CCM imeleta maendeleo

  Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Bw. Phillip Mangula amewataka wananchi wa Igunga wakipigie kura chama hicho kwa sababu kimeleta maendeleo makubwa kutoka upatikane uhuru nchini.

  Bw. Mangula akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Mwamasunga katika kata ya Igunga alisema wakati wa uhuru hakuna Mtanzania aliyemiliki baiskeli ikilinganishwa na sasa hivi ambako kila mmoja anao uwezo wa kununua.

  Alisema wakati huo pia mkoa wa Tabora kulikuwa na shule mmoja ya Sekondari lakini sasa hivi kuna shule zaidi ya 154 katika mkoa wa Tabora.

  Hata hivyo, wananchi hao walitoa masharti kwa CCM wamelete mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga, Dkt. Dalaly Kafumu awaahidi jinsi atakavyotatua matatizo yanayowakabili ya uhaba wa maji, masoko ya mazao yao na upatikanaji wa pembejeo.

  Wananchi hao walisema hawako tayari kupewa ahadi hewa kama alizowahi kutoa mbunge aliyejiuzulu, Bw. Rostam Aziz aliyejivua gamba kutoka CCM.

  Kuhusu amani, Bw. Mangula alisema: “Puuzeni uchochezi unaofanywa na wanasiasa ili kuenzi amani na utulivu vilivyopo nchini”.
   
 2. d

  dotto JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mwongo huyu Polisi: HApo kwenye Red: Huyo bosi wake kachaguliwa na Mwanasiasa wa Chama Tawala ndo maana yuko kama Boya!
   
 3. p

  politiki JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  jeshi la polisi limejidhihirisha kuwa si lolote wala chochote mnamuogopa hata kumuhoji naibu katibu wa umoja wa vijana wa ccm bw.shigella kwa kumpiga mzee watu na mashtaka alishafungua mzee wa watu kwenu na shigela anatembea anatamba kwa hakuna atayemfanya chochote na nyie mko kimya.
   
 4. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Ze comed imeanza sasa.
   
 5. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kauli nyingine ya ajabu kabisa. so muda wote walikuwa wanacheza makidamakida sasa ndo wanaanza kazi? polisi bwana!
   
 6. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hata siku moja
  lazima waitii CCM
   
 7. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280


  Ahhh!!we kamanda ni muongo mkubwa na mnafiki,hivi tukio la kufytua risasi lililotokea hivi majuzi ni hatua gani mmeshazichukua au kuwachukulia watuhumiwa!?,Babu wa Watu alipigwa mmeshamhoji!!?,Rage kuonyesha silaha adharani mmeshamchulia hatua gani!!?Nyie mnajua kutumia nguvu tu kwa vyama vya upinzani hasa Chadema.
  Mpaka Waziri mkuu awape tamko ndio mnaamka!!?Intelijensia kwenye maandamano tu ndio mmekalia tu wanafiki wakubwa nyie(polisi)
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Huyo kamanda inawezekana ni wale walioingia polisi baada ya kufeli shule kwahiyo anafanya kazi kwa maelekezo, hajui wajibu wake.

  Angekuwa anafahamu wajibu wake asingekurupuka sasahivi kutoa kauli, wangekuwa wamechukuia hatua tangu mwanzo.

  Na hawa ndio aina ya watu wengi walioko ndani ya jeshi la polisi ambao ni kikwazo kwa ustawi wa demokrasia kwa kushindwa kutafsiri na kusimamia sheria.
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkuu! Hakika hawa mapolisi wa namna hii ni wengi sana na ndio mizigo kwa jamii kwa nyakati hii tuliopo lakini mwisho wao waja tu.
   
 10. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,576
  Likes Received: 12,860
  Trophy Points: 280
  trailer
  bado movie yenyewe 2015
   
 11. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bila kuumauma maneno polisi Igunga imeonyesha udhaifu mkubwa na upendeleo wa wazi kwa CCM
   
 12. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  wanajipanga kuzuia wananchi kulinda kura zao, wameanza vitisho, dalili zinajionyesha watamwagwa polisi wengi sana igunga siku ya uchaguzi, watawaamuru wapiga kura kutawanyika mara baada ya kupiga kura, wata-quote sheria za uongo wanakijiji watashindwa kubishana nao, wakiondoka tu wanachakachua kwa kuweka kura feki zenye uwiano ccm>cuf>cdm. hiyo ni jaribio la kuuhadaa umma wa tanzania kuwa cuf inakuja juu na kukubalika kwenye jamii kuliko cdm. aibu yao kubwa ni kumuapisha mb kutoka cdm wakati job ndugai akiwa bungeni alitamka kuwa wananchi eti hawaridhishwi na aina ya uwakilishi wa cdm bungeni, ndugai atakosa pa kuificha sura yake pale wananchi wa igunga watakapomzodoa na kumuonya asikiseme tena cdm vibaya watakapomchagua kashindye. mipasho yao wataipeleka kwenye chaguzi za ccm. cdm toeni jipangeni kiukweli kulinda kura zenu, wajuzeni kanuni za kusimamia kupiga na kuhesabu kura, wajue nani anaruhusa na nani hana ruhusa kuingia kwenye chumba cha kupigia kura wakati gani, mipaka ya msimamizi wa kituo n.k
   
 13. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  "Aliongezwa kuwa kuna baadhi ya vyama vimekuwa vikitetewa katika uchaguzi, hivyo walitarajia itakuwa hivyo kila siku na kuwataka wanasiasa kufanya kampeni zao kwa kufuata sheria na sio kutegemea msaada wa kutoka polisi."

  Kumbe anakiri kumekuwepo na uoendeleo kwa baadhi ya vyama na vinategemea msaada wa polisi Asante kamishna kwa kutiuhabarisha
   
 14. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya kukamilisha mipango michafu ya kuchakachua kura kwa kushirikiana na tume ya uchaguzi pamoja na usalama wa Taifa, ndiyo sasa wanaweka mikakati ya kulinda udhalimu huo. Chadema kuweni macho hapo Igunga hakuna kulala hadi kieleweke. Wasimamizi wa uchaguzi lazima wachunguzwe kwa inteligensia za Chadema kabla ya siku ya uchaguzi hakuna kuogopa!.
   
 15. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Aibu,ni bora kusingekuwa na Mwakilishi wa IGP kuliko yanayofanywa na polisi
   
 16. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  sasa kumbe jitu limeshakuwa polisii zaidi ya miaka 40 linangoja nini tena? si ndio akina Gaddaf wote hao? lisijisifie ujinga, kukaaa miaka 40 kazini bila tija yoyote si ujinga huo jamani? heri angesema hata miaka kumi tu, mimi hapa kazini nina miezi kadhaa tangu niukimbie ualimu na kuja hapa lakini nimeshaona matunda ya kazi yangu pamoja na kuwa na muda wa kushinda kusoma news za ukweli from JF lakini pia huwezi kulinganisha na hilo ri SACP sijui ndio nini vile, nimezalisha na inaonekana sasa jitu miaka 40 halafu linasubiri lisifiwe na bosi wake, akili matope, kumbe hafanyi kazi kutimiza wajibu wake anafanya kazi ili asifiwe kweli Mipolisi haina nanihiii, wale askari wenye akili wote wameshaacha kazi ya upolisi, na nyie msicopy ligazeti lizima jamani, just go straight to your point, haya njooni tunywe chai.
   
 17. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
   
 18. k

  kiloni JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  WanaIGUNGA msidanganyike huyu njago ni kibaraka wa magamba. Hapa ni mkakati wa kulinda magamba waibe kura bila tatizo si muda umeisha?!!
   
 19. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Waandishi wa Tz acheni ushabiki.
   
 20. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #20
  Sep 26, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  sas siku zote walikua ka mapambo anh???
   
Loading...