Rugby Union
JF-Expert Member
- Nov 21, 2012
- 402
- 249
Jamaa anakaa Kinondoni Mkwajuni, majira ya saa 5 unusu akawa kituo cha daladala cha Chama/TANESKO akingoja usafiri, ama daladala au walau bajaj ya kudandia juu kwa juu.
Difenda ya polisi ikapaki pale kituoni na kumuuliza boi anaenda wapi na anatoka wapi, walipopishana Kiswahili jamaa wakamtia ndani ya Difenda na kumpeleka kituo Kikubwa cha OysterBay.
Kufika huko jamaa akavuliwa suruali, mkanda, waleti na pesa pamoja na kupokea kichapo kikali sana... Kisha akaachwa aondoke na boxer na tisheti iliyoloa damu bila kuchukuliwa maelezo yoyote wala kurudishiwa mazaga ambayo polisi walikwala kutoka kwake.
Mwana akaja gheto asubuhi yuko chapachapa damu, hana nguo zaidi ya boxer na hiyo tisheti iliyoloa damu na kunipa mkasa kama nilivyowaletea ninyi.
Kituo cha Ostabei ndipo yalipo makao makuu ya Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, na raia wanatendwa unyama huu na jeshi linalotakiwa liwalinde tena kwenye ofisi rasmi za usalama.
Swali: Kuna mahali popote ambapo mwana anaweza kupeleka malalamiko, jamaa wakashughulikiwa na bado ikawa salama kwake?