Nilivyowahi kutapeliwa na aliyejitambulisha ni polisi nikiwa jiji la Arusha

Jun 22, 2023
25
252
Utapeli hauna mjanja, hata mawaziri, maprofesa, wafanya biashara wakubwa, wanatapeliwa. hawa watu walaaniwe!!

Nimekuwa msomaji sana wa visa na mikasa inayowatokea watu na nimeweza kupata experience, mafunzo, kujua kujitahadhari, n.k. Leo nimeoamua na mimi niweze kuwaletea mkasa uliowahi kunitokea mwaka 2014 jiji la Arusha nikiwa mwanachuo wa chuo cha uhasibu, IAA.

Likizo ilipoisha nikiwa Mbeya, nikageuza kurudi Arusha, safari ilikuwa ndefu na hatimae nikafika saa nane usiku, kipindi hicho barabara zilikuwa mbovu mkiwahi ilikuwa saa sita usiku, kawaida ilikuwa sa saba hadi saa tisa.

Basi lilikuwa ni la Sumry / Arusha Express likafikia kituo cha mwisho stendi ofisi za Dar Express, guest mbili za karibu niliyozoea kulala kwa elf 10 & 15 zimejaa, Kuna teksi ilipaki kidogo hapo stendi, kuulizia bei ya kwenda njiro ni elf 25, bei ya mwisho kakazia 20, mi niliona nachoma pesa nikomae tu hapo masaa kadhaa panakucha nipande daladala, bodaboda sikufikira nilihofia wanaweza kucheza michezo ya kunigeuka njiani (Arusha miaka hio ilikuwa yamoto)

Nikaamua nikomoae nishinde pale pale stendi ya Dar Express pamoja na walinzi, nisubiri masaa matatu ama manne, pakipambazuka nianze kwenda Njiro chuo kilipo na ninapoishi. Kiukweli usingizi ulikuwa mzito ila nilijikaza hadi alfajiri.

Kwenye saa 11 na dakika kadhaa nikaanza kushuka kwenda stendi ya Crdb lile tawi kuu karibu na maduka ya Benson, nimefika stendi nikapanda kifodi (daladala), kulikuwa na waru wanahesabika, bado konda anaendelea kutafta abiria,

Ghafla kuna mtu akaja ambae kwa haraka haraka kimavazi ni polisi yupo yupo na mwenzake ambae kavalia nguo za raia kwa unadhifu, wakaniambia nishuke pale na begi, niliwaambia kuna nini ila wao wakakaza nipo chini ya ulinzi nishuke, kiukweli niliingia na woga hasa ukizingatia ni polisi kabisa, hata dereva na konda hawakuthubutu kuzungumza chochote.

Nikashuka na begi langu, tukaelekea kwenye gari ni kama taxi hivi, nilikaa siti ya nyuma pamoja na yule polisi, alikuwa ni mbaba flani hivi mrefu kimtindo, mweupe japo kwa mbali yule mwegine ambae kavalia nguo za uraia akakaa siti ya mbele kwenye usukani.

Huko siti ya nyuma yule askari akaanza kuniambia "tumekufatilia ukiwa unavuta begi hili (lenye matairi) tumpeta intelejensia humu kuna bangi" , dah nilipaniki. tukaanza kuzozana pale mimi sijabeba kitu wakitaka wafungue begi, nikataka kufungua mlango niondoke maana huo ni uhuni, yule mwenzake akafunga mlango, nikataka nipige kelele kuomba msaada! hata sijamaliza nikapigwa kofi wakaniambia nikirudia watanimaliza, nikifikiria Arusha watu kutembea na visu kawaida nikatulia !

Gari ikaanza kutembea ila hatuendi kule kaloleni kituo cha polisi, askari wa siti ya nyuma akaanza kupiga search begi langu, hapo najua tayari hawa ni wahuni tu na si ajabu wakaniwekea bangi ya kubambikiwa, nachowaza hapo ni kwamba nipo mtu kati, wahuni wamenibananisha na nikawa nawaza mbali zaidi kama watanidhuru maana kipindi hicho matukio ya kuchomana visu kwa Arusha ilikuwa ni kawaida na navyosema visu ni hizi sime kama za wamasai zimenolewa haswa, mwaka uliopita kwa pale chuoni kunamwenzetu alivamiwa na wahuni wakamuua kwa kumpiga visu, Tulijaribu kuandamana ila Ffu wakaja kama kawaida yao kipigo kwanza maelezo baadae, binafsi nashukuru sikukamatwa wala kupigwa.

Kwenye begi kulikuwa na nguo, vyeti vya sekondari na kuzaliwa, laptop na shilingi laki 2 na nusu ipo kwenye kabahasha, yule afande alichukua hela yote, vingine aliacha. mfukoni nilikuwa na elf 6 tu na simu.

Gari ikafika kituo cha Kijenge pale uwanjani kwenye mabasi yanayoenda njiro, nikaambiwa nishuke na begi langu, wanavyoondoka tu kitu cha kwanza nilinakili plate number, nazikumbuka hadi leo T2—ACB (kwenye dash hapo sikumbuki kwa uhakika ila picha inanijia ni T212 ama T232) ila sikuweza kuhitimisha kwa uhakika kama zilikuwa ni plate number za ukweli au za kufanyia utapeli wao wasigundulike kirahisi.

Basi mimi cha muhimu nikashukuru nipo salama na wameniachia begi lenye vitu muhimu kwajili ya chuoni.

Nilienda hostel nikaweka begi langu, nikaanza safari ya kwenda Kaloleni kituo cha polisi, nilikata RB nimeibiwa na Polisi lakini hata pale counter walishangaa sana. navyoondoka hapo kituoni kuna afande alikuwa analinda nje pale, aliniomba namba ya gari nikampa, nikaondoka.

Zaidi ya hapo niliwapigia wazazi simu kuwajulisha hali iliyonipata, ila wakaniasa nisifatilie niachane nao maana wanaweza kuwa watu hatari, Nashukuru pia waliweza kunitumia kiasi cha fedha kufidia fidia kilichopotea.

Kuanzia hapo nilijifunza kufanya booking ys vhumba cha gesti mapema hata siku 2 kabla sijafika Arusha, pia nilipata namba ya dereva Taxi mwaminifu.

Funzo nililopata ni kufanya kila jitihada kudeal na mambo haya hadharani sehemu yenye watu bila aibu, hawa jamaa moja ya mbinu yao kuu ni kuhakikisha wanakupeleka mazingira ambayo yana usiri wawe peke yao na wewe.
 
Pole ila funzo lako sijalielewa,mbona sijaona ni wapi ulipokosea,hata kama ungekuwa na chumba ukaamka saa mbili asubuhi hao matapeli ungeweza kukutana nao tu.

Au tuambie ni vipi kupata chumba ungeepuka kutapeliwa?
Dah! ila kweli, hawa jamaa huwaga hawana muda maalum, huenda walipomalizana na mimi wakatapeli mwengine mchana
 
Utaku
NB: Hadi sasa sijajua kama afande yule alikuwa wa kweli ama wa kushonesha uniform (fatilia zaidi mkasa kwa maelezo zaidi)

Nimekuwa msomaji sana wa visa na mikasa inayowatokea watu na nimeweza kupata experience, mafunzo, kujua kujitahadhari, n.k. Leo nimeoamua na mimi niweze kuwaletea mkasa uliowahi kunitokea mwaka 2014 jiji la Arusha nikiwa mwanachuo wa chuo cha uhasibu, IAA.
Matapeli huwa wanaangalia muonekano wako,utakuwa umekaa kindezi
 
Inaonekana bado hujabadilika.maana kwajinsi ulivyoandika inatia shaka.angalia watakufwatilia hadi uku mtandaoni wakutapeli tena.
 
Utaku

Matapeli huwa wanaangalia muonekano wako,utakuwa umekaa kindezi
Hii tabia ya wabongo kama wewe kucheka wengine waliopatwa na majanga haya wakati hata wao yaliwahi kuwakuta ikome.

Wewe ulitapeliwa na mganga dawa za biashara kuna mtu alikukebehi ?

Niliwahi kwenda kwa mganga kuomba dawa ya biashara haikusaidia

ukaweka uzi mwengine kulalamika unapewa kipigo na mke wako

Wanaume wengi tunapigwa na wake zetu ila hatusemi

Kuchekana sio vizuri, humu tunaelimishana,
 
Watu kama hao natamani sana nikutane nao ili niapply technique za Sholinji kempo
 
Huyu jamaa hawakumuona kwenye gari kitambo tu walishaanza kumtrack!
Arusha miaka ya 2010++ ilishaanza kupoa zilikuwa ni zile nipe nikupe kabla ya hapo kulikuwa na zle vurugu za majamaa wa mererani
 
Utapeli hauna mjanja, yeyote akifikiwa lazima aliwe.

Nimekuwa msomaji sana wa visa na mikasa inayowatokea watu na nimeweza kupata experience, mafunzo, kujua kujitahadhari, n.k. Leo nimeoamua na mimi niweze kuwaletea mkasa uliowahi kunitokea mwaka 2014 jiji la Arusha nikiwa mwanachuo wa chuo cha uhasibu, IAA.

Likizo ilipoisha nikiwa Mbeya, nikageuza kurudi Arusha, safari ilikuwa ndefu na hatimae nikafika saa nane usiku, kipindi hicho barabara zilikuwa mbovu mkiwahi ilikuwa saa sita usiku, kawaida ilikuwa sa saba hadi saa tisa.

Basi lilikuwa ni la Sumry / Arusha Express likafikia kituo cha mwisho stendi ofisi za Dar Express, guest mbili za karibu niliyozoea kulala kwa elf 10 & 15 zimejaa, Kuna teksi ilipaki kidogo hapo stendi, kuulizia bei ya kwenda njiro ni elf 25, bei ya mwisho kakazia 20, mi niliona nachoma pesa nikomae tu hapo masaa kadhaa panakucha nipande daladala, bodaboda sikufikira nilihofia wanaweza kucheza michezo ya kunigeuka njiani (Arusha miaka hio ilikuwa yamoto)

Nikaamua nikomoae nishinde pale pale stendi ya Dar Express pamoja na walinzi, nisubiri masaa matatu ama manne, pakipambazuka nianze kwenda Njiro chuo kilipo na ninapoishi. Kiukweli usingizi ulikuwa mzito ila nilijikaza hadi alfajiri.

Kwenye saa 11 na dakika kadhaa nikaanza kushuka kwenda stendi ya Crdb lile tawi kuu karibu na maduka ya Benson, nimefika stendi nikapanda kifodi (daladala), kulikuwa na waru wanahesabika, bado konda anaendelea kutafta abiria,

Ghafla kuna mtu akaja ambae kwa haraka haraka kimavazi ni polisi yupo yupo na mwenzake ambae kavalia nguo za raia kwa unadhifu, wakaniambia nishuke pale na begi, niliwaambia kuna nini ila wao wakakaza nipo chini ya ulinzi nishuke, kiukweli niliingia na woga hasa ukizingatia ni polisi kabisa, hata dereva na konda hawakuthubutu kuzungumza chochote.

Nikashuka na begi langu, tukaelekea kwenye gari ni kama taxi hivi, nilikaa siti ya nyuma pamoja na yule polisi, alikuwa ni mbaba flani hivi mrefu kimtindo, mweupe japo kwa mbali yule mwegine ambae kavalia nguo za uraia akakaa siti ya mbele kwenye usukani.

Huko siti ya nyuma yule askari akaanza kuniambia "tumekufatilia ukiwa unavuta begi hili (lenye matairi) tumpeta intelejensia humu kuna bangi" , dah nilipaniki. tukaanza kuzozana pale mimi sijabeba kitu wakitaka wafungue begi, nikataka kufungua mlango niondoke maana huo ni uhuni, yule mwenzake akafunga mlango, nikataka nipige kelele kuomba msaada! hata sijamaliza nikapigwa kofi wakaniambia nikirudia watanimaliza, nikifikiria Arusha watu kutembea na visu kawaida nikatulia !

Gari ikaanza kutembea ila hatuendi kule kaloleni kituo cha polisi, askari wa siti ya nyuma akaanza kupiga search begi langu, hapo najua tayari hawa ni wahuni tu na si ajabu wakaniwekea bangi ya kubambikiwa, nachowaza hapo ni kwamba nipo mtu kati, wahuni wamenibananisha na nikawa nawaza mbali zaidi kama watanidhuru maana kipindi hicho matukio ya kuchomana visu kwa Arusha ilikuwa ni kawaida na navyosema visu ni hizi sime kama za wamasai zimenolewa haswa, mwaka uliopita kwa pale chuoni kunamwenzetu alivamiwa na wahuni wakamuua kwa kumpiga visu, Tulijaribu kuandamana ila Ffu wakaja kama kawaida yao kipigo kwanza maelezo baadae, binafsi nashukuru sikukamatwa wala kupigwa.

Kwenye begi kulikuwa na nguo, vyeti vya sekondari na kuzaliwa, laptop na shilingi laki 2 na nusu ipo kwenye kabahasha, yule afande alichukua hela yote, vingine aliacha. mfukoni nilikuwa na elf 6 tu na simu.

Gari ikafika kituo cha Kijenge pale uwanjani kwenye mabasi yanayoenda njiro, nikaambiwa nishuke na begi langu, wanavyoondoka tu kitu cha kwanza nilinakili plate number, nazikumbuka hadi leo T2—ACB (kwenye dash hapo sikumbuki kwa uhakika ila picha inanijia ni T212 ama T232) ila sikuweza kuhitimisha kwa uhakika kama zilikuwa ni plate number za ukweli au za kufanyia utapeli wao wasigundulike kirahisi.

Basi mimi cha muhimu nikashukuru nipo salama na wameniachia begi lenye vitu muhimu kwajili ya chuoni.

Nilienda hostel nikaweka begi langu, nikaanza safari ya kwenda Kaloleni kituo cha polisi, nilikata RB nimeibiwa na Polisi lakini hata pale counter walishangaa sana. navyoondoka hapo kituoni kuna afande alikuwa analinda nje pale, aliniomba namba ya gari nikampa, nikaondoka.

Zaidi ya hapo niliwapigia wazazi simu kuwajulisha hali iliyonipata, ila wakaniasa nisifatilie niachane nao maana wanaweza kuwa watu hatari, Nashukuru pia waliweza kunitumia kiasi cha fedha kufidia fidia kilichopotea.

Kuanzia hapo nilijifunza kufanya booking ys vhumba cha gesti mapema hata siku 2 kabla sijafika Arusha, pia nilipata namba ya dereva Taxi mwaminifu.

Funzo nililopata ni kufanya kila jitihada kudeal na mambo haya hadharani sehemu yenye watu bila aibu, hawa jamaa moja ya mbinu yao kuu ni kuhakikisha wanakupeleka mazingira ambayo yana usiri wawe peke yao na wewe.
Polisi wawe wa uongo au wa kweli, hakikisha wakikuzunguruka unapiga kelele ili watoe maelezo yao mbele ya halaiki, wengine wachukue video, sura, namba za gari zionekane na zisambazwe mtandaoni.
Bahati mbaya taasisi zetu zote Tz haziaminiki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom