Jeshi la polisi limebariki huu wizi Kariakoo?

Mazima1

Member
Dec 31, 2020
20
47
Habari wana JF,

Kuna huu wizi sijui niite utapeli ambao binafsi nimeanza kuushuhudia tangu mwaka 2022 kwa maeneo ya Kariakoo na kila mara nikipita eneo hilo nakuta huo wizi unaendelea utapeli wenyewe unafanywa na jamaa wauza juice ya miwa mitaa ya karume mbele ya TBL (Tanzania Breweries Limited)

Wizi unafanyika kama ifuatavyo:
Muuza juice atakuita na kujifanya amekufananisha kisha atakuuliza ''Vipi mzee daah kitambo sana mwanangu, vipi siku hizi wapi?''

Wewe utajibu labda nipo Magomeni siku hizi.

Muuza juice: Anhaa ndiyo maana kule kitaa sikuoni siku hizi.

Wewe: Wapi? Kule kitunda au?

Basi hapo ndo utakuwa umeyavagaa jamaa atajifanya kukujua sana atakuuliza kuhusu story za vipi wale jamaa wanaopiga matizi uwanjani pale bado wapo?

Actually hakuna sehemu ambayo haina uwanja wa mpira so yote kwa yote jamaa atakuwa amekuteka akili kwa kujifanya anakujua sema ni vile tu umemsahau

Kinachofuatia jamaa atakumiminia juice " karibu juice kaka".

Ukimaliza kunywa tu hiyo juice jamaa anakubadilikia na kuanza kukudai hela ya Juice.

ukishindwa kulipa atakukaba, atakupiga hata kukuumiza.

Wahanga wakubwa wa haya matukio ni wale wa kuja lakini hata kama born town unaweza kujikuta umeingia mkenge vile vile

Kinachonifikirisha ni kuwa Kituo cha polisi Gerezani hakipo mbali na hapo Karume na pia maeneo ya China Plaza, hawa jamaa hawajanusa taarifa za huu ushenzi kweli? Au kuna mgawo, maana hawa jamaa wanafanya hii michezo kuanzia asubuhi hadi jioni tangu 2022 nimewaona hadi leo 2024 wapo.

Picha mojawapo ya mhuhusika wa hiyo michezo ni hiyo hapo huyo muuza juice na hapo alikuwa anamuingiza mkenge jamaa.

IMG_20240305_143617[1].jpg
IMG_20240305_143613[1].jpg
 
We mwenyewe ni tapeli umejifanya na wewe unamjua ili unywe juice yake bure Acha akutie vitasa.

Alafu mwanaume unakaaje kizembe hadi unapigwa na mtu mmoja? Pigana nae utoe hata droo yani unataka polisi waingilie hadi huo ujinga?
 
We mwenyewe ni tapeli umejifanya na wewe unamjua ili unywe juice yake bure Acha akutie vitasa.

Alafu mwanaume unakaaje kizembe hadi unapigwa na mtu mmoja? Komaa nae utoe hata droo achana na habari za polisi
 
Habari wana JF, kuna huu wizi sijui niite utapeli ambao binafsi nimeanza kuushuhudia tangu mwaka 2022 kwa maeneo ya Kariakoo na kila mara nikipita eneo...
Unasimamishwaje na mtu usiyemjua, usiyejua nia yake na kuongea naye kwa muda wote huo?

Kibaya zaidi, unakunywa vipi juisi yake kirahisi hivyo? Akikuwekea dawa za kukulevya na kukufanya kitu kibaya je?
 
Dar hii huna mamlaka yoyote, unapewa kitu cha bure na mtu usiemjua na unakubali kindezi tu.

Kila mtu hula kwa urefu wa kamba yake, kama wewe ni mtu wa tra vinywaji vya bure utajua pa kuvipata, kama wewe ni mgambo wa jiji vya bure vipo na unajua unavipata wapi nk.

Huna ishu yoyote ya kimamlaka town afu unapewa juice kindezi unagwia tu.
 
Unasimamishwaje na mtu usiyemjua, usiyejua nia yake na kuongea naye kwa muda wote huo?

Kibaya zaidi, unakunywa vipi juisi yake kirahisi hivyo? Akikuwekea dawa za kukulevya na kukufanya kitu kibaya je?
Mzee watu hawana ishu za kufanya, muda wanao mwingi sana.

Hizo dakika 2 anazonisimamisha ziwe na manufaa sio kufananishana kindezi.
Zaidi zaidi unachukua namba yake unamwambia kuna ishu unawahi utamcheki, ndo ntolee hiyo.
 
Back
Top Bottom