Nadhani ni simu zote ila hapo imesisitizwa Android kutokana na jamii pana ya Tanzania inatumia simu zenye mfumo huo na hawa wamekariri kwamba simu yenye Android system ikipotea/ibiwa hakuna mfumo wa kuifanya ijulikane ilipo wanachojua wao iPhones ndo zina mfumo huo tu wakisahahu technology imesogea sana that's why mkwapuaji akiiba mfano Samsung akaiingiza sokoni dk tu itanunuliwa ila yenye mfumo wa ios wanaigwaya wanaziogopa.Ko ni simu za andoid tuu..? Windows, BlackBerry na Ios tununue?
Siyo watanzania wote! Ni baadhi ya watanzania.Mtanzania ni mtu wa kuchukulia serious mambo ya kipuuzi na kupuuza mambo serious.
Polisi hawa hawa ni bora uiache .watakupa kesi ,mpaka kwisha usumbufu hata hela utapigwa.uwezo wa upelelezi mdogo rahisi kwao ni kukuhusishaPia unapoona SAMSUNG GALAXY 6 EDGE njiani iokote na ipeleke polisi. Kukaa na simu ya mtu ni hatari inawezekana mwenyewe aliuwawa.
Juzi tu nimetoka kukamata mwizi wangu wa simu. Hakuamini nilivyoweza kufika mpaka mlangoni kwake._*KUTOKA JESHI LA POLICE:*_
_*USALAMA WA MAISHA YAKO*_
☆ _*Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua*. Hiyo ni hatari kwani hujui huyo jamaa kaitoa wapi, mwisho wa siku unapewa kesi ya wizi au mauaji._ _Inawezekana simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa._
☆ _*Usimpe mtu usiyemjua* simu yako apige sehemu yoyote._
_*Unapoiona line njiani ipo chini*, usitake kuiokota na kuiweka simuni mwako ujue ina shilingi ngapi ili uchukue salio._
☆ _*Simu inapoibiwa* au_
_mwenye simu kuuawa, line hutupwa, unapoiweka simuni mwako,simuyako inahusishwa na tukio hilo_
☆ _*Unapoweka salio,* hakikisha karatasi ya vocha unaichana. Unapoitupa, watu wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe kuhusishwa._
☆ _*Usikubali kumsajilia mtu line* yake kwa jina lako, hata kama baba yako, usikubali._
☆ _*Kumbuka namba yako umesajiliwa*, moja ya matukio hayo yakitokea na namba yako kuonekana, moja kwa moja unakuwa mtuhu-miwa namba moja._
☆ _*Wengi wamepewa kesi za mauaji*, wizi bila kujua. Polisi wapo kazini, wanapoona vidhibiti wanakuchukua kwani hawatojua kama umehusika au la. Kuweni makini ili usije kuingia matatizoni, simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi kama uzembe, utaishia pabaya._
Kutoka Cyber Crimes
_*SIMU YAKO JEMBE LAKO*_
_*SHARE UJUMBE HUU UMPE ONYO NA MWENZAKO.*_
Juzi tu nimetoka kukamata mwizi wangu wa simu. Hakuamini nilivyoweza kufika mpaka mlangoni kwake.
[/QUOTE
Duh! Ulifanyaje mkuu?
...mkamalizanaje, mkuu?Juzi tu nimetoka kukamata mwizi wangu wa simu. Hakuamini nilivyoweza kufika mpaka mlangoni kwake.
Polisi wapo kazini, wanapoona vidhibiti wanakuchukua kwani hawatojua kama umehusika au la. Kuweni makini ili usije kuingia matatizoni, simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi kama uzembe, utaishia pabaya._
Kutoka Cyber Crimes
_*SIMU YAKO JEMBE LAKO*_
_*SHARE UJUMBE HUU UMPE ONYO NA MWENZAKO.*_