Polisi: Usinunue simu kwa mtu usiyemjua

Polisi: Usinunue simu kwa mtu usiyemjua

Mbona mnatuzungusha sana tunapofuatilia simu zetu zilizoibiwa, mnatutaka rushwa mara njoo kesho kesho kesho inakuwa wiki mwezi mwaka miaka, sijui kama hicho kitengo kinauwezo wa kufanya kazi kama wenzetu nchi zingine au hapa kwetu ni kitengo cha polisi kupatia kipato cha ziada tu.
Lakini vipi kuhusu ushauri wao unaukubali au hauna maana kwako.
 
Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua. Hiyo ni hatari kwani hujui huyo jamaa kaitoa wapi, mwisho wa siku unapewa kesi ya wizi au mauaji. Inawezekana simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa.

Usimpe mtu usiyemjua simu yako apige sehemu yoyote.

Unapoiona line njiani ipo chini, usitake kuiokota na kuiweka simuni mwako ujue ina shilingi ngapi ili uchukue salio.

Simu inapoibiwa au mwenye simu kuuawa, line hutupwa, unapoiweka simuni mwako,simuyako inahusishwa na tukio hilo

Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha unaichana. Unapoitupa, watu wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe kuhusishwa.

Usikubali kumsajilia mtu line yake kwa jina lako, hata kama baba yako, usikubali.
Kumbuka namba yako umesajiliwa, moja ya matukio hayo yakitokea na namba yako kuonekana, moja kwa moja unakuwa mtuhu-miwa namba moja.

Wengi wamepewa kesi za mauaji, wizi bila kujua. Polisi wapo kazini, wanapoona vidhibiti wanakuchukua kwani hawatojua kama umehusika au la. Kuweni makini ili usije kuingia matatizoni, simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi kama uzembe, utaishia pabaya.

Kutoka kitengo cha Cyber Crimes

SIMU YAKO JEMBE LAKO. . . .USICHUKULIE POA!!!!!
 
Hii elimu iwe endelevu kwa kutolewa redioni, kwenye tv, magazetini na hata ujumbe kwenye simu.. kama ilivyokuwa kampeni ya mifuko ya plastiki..
 
Hii elimu iwe endelevu kwa kutolewa redioni, kwenye tv, magazetini na hata ujumbe kwenye simu.. kama ilivyokuwa kampeni ya mifuko ya plastiki..
Kweli kabisa, haifai kuishia kwenye mitandao ya kijamii tu. Ni vema jeshi la Polisi likatafuta namna ya kuwafikishia huu ujumbe wananchi kama ulivosema
 
Hivi vocha bado zipo?
Sikumbuki mara ya mwisho nilinunua lini credo!.
Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha unaichana. Unapoitupa, watu wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe kuhusishwa.
 
I aappreciate, lkn tuambiwe matapeli wengi sasahv wanaotumia line kibao, na wamefikia kias kwamba wametengeneza ofisi zao kama Huduma kwa wateja, na mitandao ya namba hzo inafahamika,
Je, hizo lines nani anatumia?
Je, mnashirikianaje na TCRA kuwadhibiti matapeli hawa?
Je, matapeli hawa ni vishoka wa mitandao husika?
Je, Kama ni vishoka wanagawana na nani mafungu haya ya kitapeli wanayopata?

Maana imekuwa kawaida tu kwa Tanzania, kutapeli watu usiku na mchana......hii pia ni kusema Tanzania ni Salama? Ni pamoja na haya. Inakera sana hii.
Nawasilisha.
 
KUTOKA JESHI LA POLICE: USALAMA WA MAISHA YAKO.

* Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua. Hiyo ni hatari kwani hujui huyo jamaa kaitoa wapi, mwisho wa siku unapewa kesi ya wizi au mauaji. Inawezekana simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa.

* Usimpe mtu usiyemjua simu yako apige sehemu yoyote.

* Unapoiona line njiani ipo chini, usitake kuiokota na kuiweka simuni mwako ujue ina sh ngapi ili uchukue salio. Simu inapoibiwa au mwenye simu kuuawa, line hutupwa, unapoiweka simuni mwako, simu yako inahusishwa na tukio hilo.

* Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha unaichana. Unapoitupa, watu wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe kuhusishwa.

* Usikubali kumsajilia mtu line yake kwa jina lako, hata kama baba yako, usikubali. Kumbuka namba yako umesajiliwa, moja ya matukio hayo yakitokea na namba yako kuonekana, moja kwa moja unakuwa mtuhumiwa namba moja.

Wengi wamepewa kesi za mauaji, wizi bila kujua. Polisi wapo kazini, wanapoona vidhibiti wanakuchukua kwani hawatojua kama umehusika au la. Kuweni makini ili usije kuingia matatizoni, simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi kama uzembe, utaishia pabaya.

MPE ONYO NA MWENZAKO.
Nikweli kabisa,kuna jamaa yangu alisota mwezi mzima osterbay kisa kuna mtu alikuwa naye Mwendokasi akampa demu Simu yake awasiliane na mtu,yule mtu kumbe alikuwa lodge anamsubilia akampa madawa na kumwibia kila kitu,last call ikawa ya mshikaji wakamnasa
 
KUTOKA JESHI LA POLICE: USALAMA WA MAISHA YAKO.

* Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua. Hiyo ni hatari kwani hujui huyo jamaa kaitoa wapi, mwisho wa siku unapewa kesi ya wizi au mauaji. Inawezekana simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa.

* Usimpe mtu usiyemjua simu yako apige sehemu yoyote.

* Unapoiona line njiani ipo chini, usitake kuiokota na kuiweka simuni mwako ujue ina sh ngapi ili uchukue salio. Simu inapoibiwa au mwenye simu kuuawa, line hutupwa, unapoiweka simuni mwako, simu yako inahusishwa na tukio hilo.

* Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha unaichana. Unapoitupa, watu wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe kuhusishwa.

* Usikubali kumsajilia mtu line yake kwa jina lako, hata kama baba yako, usikubali. Kumbuka namba yako umesajiliwa, moja ya matukio hayo yakitokea na namba yako kuonekana, moja kwa moja unakuwa mtuhumiwa namba moja. Wengi wamepewa kesi za mauaji, wizi bila kujua.

Polisi wapo kazini, wanapoona vidhibiti wanakuchukua kwani hawatojua kama umehusika au la. Kuweni makini ili usije kuingia matatizoni, simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi kama uzembe, utaishia pabaya.
Kwanini iwe kwa simu za Android tu? Ujambazi au jinai haiwezi kufanywa kwa simu zingine?
 
Back
Top Bottom