Mlalamikaji daily
JF-Expert Member
- May 19, 2014
- 1,018
- 2,366
dah hii ya kuchana vocha imenigusa sana.
Deejaywillzz hakika wewe ni mmoja wapo wa wanajamvi ninao waheshimu sana! ila kwa kweli hiyo heading imekaa vibaya sana maana hapa wengi wetu tulidhani ni suali la bei tu lakini dhahiri hapa unazungumzia simu za wizi ambazo aghalab huuzwa kwaa bei ya chini.
mkosoaji hakuwa na nia mbaya na wala hakukuwa na haja ya sacarsm kwenye comment yako dhidi ya Shiy c.
Sio kwamba hawato mkamata muhusika bali wakati wa kutafuta ukweli wewe lazima uwe primary suspect...na hili kuondoa usumbufu na matatizo utakayo yapata ni vyema kujiepusha na yanayo semwa hapo juu!Mh,kazi sana.Hivi mtu anaokota vocha katika katika tukio la kihalifu hakuna forensic investigation inayoweza kufanyika na kugundua ukweli.Kutonunua simu kwa mtu au kutomuazimisha simu mtu kufanya mawasiliano sidhani kama inaleta tija sana kama kuna weledi mzuri wa kiuchunguzi.Inakuwaje kama uliyemuazima mtu simu ni ndugu yako then ndo mhalifu mkubwa na hujui kuhusu ayafanyayo.Naona bado kuna mapungufu makubwa katika hayo.
Hoja kubwa hapo ni kusajili sim card ya mtu mwingine kwa jina lako,japo napo ikitokea uhalifu uchunguzi waweza fanyika na kukutoa katika matatizo.
Tatizo ni kutokujua. Kikubwa ni kupeana elimu kama hivi itasaidia kupunguza tatizoKUTOKA JESHI LA POLICE:
USALAMA WAKO
View attachment 335060
* Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua. Hiyo ni hatari kwani hujui huyo jamaa kaitoa wapi, mwisho wa siku unapewa kesi ya wizi au mauaji. Inawezekana simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa.
* Usimpe mtu usiyemjua simu yako apige sehemu yoyote.
* Unapoiona line njiani ipo chini, usitake kuiokota na kuiweka simuni mwako ujue ina shilingi ngapi ili uchukue salio. Simu inapoibiwa au
mwenye simu kuuawa, line hutupwa, unapoiweka simuni mwako, simu yako
inahusishwa na tukio hilo.
* Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha unaichana. Unapoitupa, watu wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe kuhusishwa.
* Usikubali kumsajilia mtu line yake kwa jina lako, hata kama baba yako, usikubali.
Kumbuka namba yako umesajiliwa, moja ya matukio hayo yakitokea na namba yako kuonekana, moja kwa moja unakuwa mtuhu-miwa namba moja. Wengi wamepewa kesi za mauaji, wizi bila kujua. Polisi
wapo kazini, wanapoona vidhibiti wanakuchukua kwani hawatojua kama umehusika au la. Kuweni makini ili usije kuingia matatizoni, simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi kama uzembe, utaishia pabaya.
SIMU YAKO JEMBE LAKO
SHARE UJUMBE HUU UMPE TAHADHARI NA MWENZAKO.