Polisi: Usinunue simu kwa mtu usiyemjua

Polisi: Usinunue simu kwa mtu usiyemjua

Tunashukuru mkuu kwa kutukumbusha wenye akili tumekuelewa vizuri
 
KUTOKA JESHI LA POLICE:

USALAMA WAKO

View attachment 335060

* Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua. Hiyo ni hatari kwani hujui huyo jamaa kaitoa wapi, mwisho wa siku unapewa kesi ya wizi au mauaji. Inawezekana simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa.

* Usimpe mtu usiyemjua simu yako apige sehemu yoyote.

* Unapoiona line njiani ipo chini, usitake kuiokota na kuiweka simuni mwako ujue ina shilingi ngapi ili uchukue salio. Simu inapoibiwa au
mwenye simu kuuawa, line hutupwa, unapoiweka simuni mwako, simu yako
inahusishwa na tukio hilo.

* Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha unaichana. Unapoitupa, watu wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe kuhusishwa.

* Usikubali kumsajilia mtu line yake kwa jina lako, hata kama baba yako, usikubali.

Kumbuka namba yako umesajiliwa, moja ya matukio hayo yakitokea na namba yako kuonekana, moja kwa moja unakuwa mtuhu-miwa namba moja. Wengi wamepewa kesi za mauaji, wizi bila kujua. Polisi

wapo kazini, wanapoona vidhibiti wanakuchukua kwani hawatojua kama umehusika au la. Kuweni makini ili usije kuingia matatizoni, simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi kama uzembe, utaishia pabaya.

SIMU YAKO JEMBE LAKO

SHARE UJUMBE HUU UMPE TAHADHARI NA MWENZAKO.


Lakini Polisi nao wanazifanya kesi za hizi simu mtaji kwao, ukipeleka taarifa ya kuibiwa simu wanakuzungusha kama vile umeenda kuomba ajira, ati mara tupatie laki moja ili tuitafute, je kama kiongozi wa serikali akiibiwa simu na kutoa taarifa polisi naye hutakiwa kutoa laki moja kama gharama ya kutafutia hiyo simu?
 
Again hili jambo lishazungumzwa sana,inasikitisha mno kuwa mpaka karne hii jeshi letu la polisi haliendani na mabadiliko ya kiteklonojia,mimi ninaamini jeshi letu la polisi halina FORESINC INVESTIGATORS,hawa ni wataalamu muhimu mno katika kupeleleza na kukusanya ushahidi,ndio maana tunatumia nguvu mno kuliko utaalamu katika kuendesha kesi,nikitumia vocha nikaitupa na mhalifu akaitumia katika uhalifu wake,ni kazi ya kitengo hiki kutambua hilo,na wanauwezo huo bila ya usumbufu hadi watakapo kuwa wamelink crime scene na suspect,hivi ndani ya nchi yetu tuna finger prints system?,maana bila ya kuwa na hii system utambuaji wa suspects ni mgumu mno,tuache kufanya kazi kwa mazoea ni lazima jeshi letu liendane na dunia ya sasa.
 
Ni dhahiri kuwa, mawasiliano kwa njia ya simu yamerahisisha ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi. Katika hatua hii, yapo mambo yanayotumika kinyume na lengo lililokusudiwa ambapo wapo baadhi ya watu wenye kutumia mawasiliano kwa njia za kiuhalifu na kupeana mbinu hasi zenye kujenga chuki, umasikini, hofu na visasi.

Kwa sasa hapa nchini wapo baadhi ya watu wenye kutumia mawasiliano ya simu kutapeli na kuwahadaa watu kwa lengo la kufanya uhalifu ama kutekeleza dhamira ovu, jambo ambalo linapaswa kukemewa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Simu za mkononi zimekuwa zikitumika sana sio tu kwa ajili ya mawasiliano (kupiga, kupokea ama kutuma ujumbe mfupi wa maneno), bali pia zimekuwa zikitumika kama nyenzo ya kufanyia miamala mbalimbali ya kifedha, mitandao ya kijamii kama whatsApp, Instagram, facebook na mambo mengi mengineyo.

Kutokana na kuimarika kwa matumizi ya simu kwenye miamala ya kifedha, wahalifu nao wamekuwa wakiitumia fursa hiyo katika kufanikisha malengo yao ya kuwaibia watu fedha zao.

Wahalifu hao wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali katika kuwaibia watu ikiwamo kuwapigia simu na kujifanya watu fulani ambao wanataka kufanya biashara na wewe hivyo muwasiliane kwa ajili ya kufanya miamala ya kifedha.

Na kwamba ili kukamilisha biashara hiyo, unahitajika kutuma kiasi fulani cha fedha na ukituma fedha hiyo inakuwa tayari umeshaibiwa.

Mbali na mbinu hiyo, wapo pia wanaoiba simu za watu na kuzitumia simu hizo kuwaibia hela ndugu na jamaa wa mwenye simu kwa kuwatumia ujumbe mfupi wa maneno kuwa mwenye simu ana shida ya kiasi fulani cha fedha na alipo hawezi kupokea ama kupiga simu hivyo umjibu kwa meseji.

Watu wengi wameshakutana na wizi wa mitandao aidha wao wenyewe ama jamaa zao na wengi wamekuwa wakiishia kulalamika bila kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika.

Pengine ni kutokana na kutofahamu nini cha kufanya au wengine kwa kufahamu ila hawaoni umuhimu wa kuchukua hatua za kisheria kwa kuripoti matukio hayo katika vituo vya Polisi.

Jeshi la Polisi lina kitengo kinachoshughulikia masuala ya uhalifu wa mitandao (Cyber Crime). Kitengo hiki kinao utaratibu wa kufanya doria za mitandao ikiwa ni pamoja na kupambana na wahalifu wanaowabaini kujihusisha na uhalifu kwa njia ya mitandao.

Kupitia kitengo hiki cha Cybercrime, Jeshi la Polisi limekuwa likiwashughulikia wahalifu wanaojihusisha na uhalifu wa aina hii kwa kuwafikisha mahakamani.

Takwimu za Jeshi la Polisi Tanzania zinaonyesha kuwa kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2017, matukio ya makosa yatokanayo na miamala ya simu yaliyoripotiwa yalikuwa 1,149.

Msaidizi wa Mkuu wa Kitengo cha Cybercrime Makao Makuu ya Polisi, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Joshua Mwangasa, amesema kuwa tatizo la wizi wa kutumia simu limekuwa ni kubwa nchini kutokana na kukua kwa teknolojia.

“Kwa sasa matumizi ya simu yamekuwa makubwa sana kwani zaidi ya mawasiliano, sasa hivi simu zimekuwa zikitumika kama benki ambapo watu wanazitumia kwa kufanya miamala ya kifedha” alisema ASP Mwangasa.

Mbali na kuwashughulikia wahalifu, Jeshi la Polisi pia limekuwa likitoa tahadhari kwa wananchi kuhusiana na uhalifu wa mitandao hususani simu.

Miongoni mwa tahadhari hizo ni pamoja na kuwataka wananchi kuwa makini na matumizi yao ya simu za mkononi kwa kuepuka kutoa namba zao za siri za miamala ya fedha.

Pia wananchi wanaaswa kuwa makini na mtu/watu wanaowatumia ujumbe mfupi wa maandishi (sms) unaowataka kuwatumia fedha au kutaka taarifa zao za siri za miamala kutoka kwa jamaa zao ama wanaojifanya kuwa ni watoa huduma za simu.

Endapo utatumiwa ujumbe wa maandishi utakaokutaka kumtumia mtu fedha, hakikisha unampigia mhusika na uongee nae na kumuuliza maswali yatakayokusaidia kujihakikishia kuwa kweli ni yeye unayemfahamu. Usifanye muamala wowote kwa mtu usiyekuwa na uhakika naye.

Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua kwani huwezi jua huyo mtu ameitoa wapi, inawezekana imetumika kufanyia matukio ya kihalifu na hivyo kujikuta ukiingia matatani na polisi baada ya upepelezi kufanyika na wewe kukutwa ukiitumia simu hiyo.

Usimpe mtu usiyemjua kutumia simu yako kumpigia mtu yoyote na usiokote laini ya simu iliyotupwa na kuitumia au hata kuuliza salio lake ili ujihamishie halafu uitupe kwani ni hatari, huwezi kujua nani aliyeitupa na kwanini.

Usikubali kutumia kitambulisho chako kumsajilia mtu laini yake hata kama ni ndugu yako kwa kuwa mtu huyo akiitumia simu yake kufanyia uhalifu, wewe ndiwe utakayekamatwa kwa kuwa jina litakaloonekana kuwa mmiliki wa simu hiyo ni la kwako wewe uliyeisajili.

Ikiwa imetokea umeibiwa kwa njia ya mtandao, nenda kituo cha Polisi kilicho karibu nawe, katoe taarifa kuhusiana na tukio zima bila kuficha taarifa zozote muhimu kwani taarifa sahihi ndizo zitasaidia kufanikisha kukamatwa kwa mhalifu. Usione aibu kuripoti tukio la kuibiwa kwa njia ya mtandaoni wala usijione mshamba kwani uhalifu hauna mshamba wala mjanja.

Tushirikiane na Jeshi la Polisi kwa kuwafichua wahalifu wa aina zote hata kama ni ndugu, jamaa au rafiki zetu. Mhalifu ni mhalifu tu, ukimficha leo kesho atakurudi wewe mwenyewe.

Imetolewa na;
Kitengo cha habari, Elimu na mawasiliano,
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
S.L.P 9141
Dar es Salaam
 
Unaongea na vodacom hapa makao makuu,fuata maelekezo yafuatayo ili tuweze kukuingizia bonus yako
 
".....Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua kwani huwezi jua huyo mtu ameitoa wapi"

basi nitanunua za ios au windows
 
Mtanisamehe mimi mvivu wa kuandika nimei-post kama nilivyoichukua hakuna popote nilipo-edit muhimu ujumbe utufikie.

KUTOKA JESHI LA POLICE: USALAMA WA MAISHA YAKO

Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua. Hiyo ni hatari kwani hujui huyo jamaa kaitoa wapi, mwisho wa siku unapewa kesi ya wizi au mauaji. Inawezekana simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa.

Usimpe mtu usiyemjua simu yako apige sehemu yoyote.

Unapoiona line njiani ipo chini, usitake kuiokota na kuiweka simuni mwako ujue ina shilingi ngapi ili uchukue salio.

Simu inapoibiwa au mwenye simu kuuawa, line hutupwa, unapoiweka simuni mwako, simu yako inahusishwa na tukio hilo

Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha unaichana. Unapoitupa, watu wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe kuhusishwa.

Usikubali kumsajilia mtu line yake kwa jina lako, hata kama baba yako, usikubali.

Kumbuka namba yako umesajiliwa, moja ya matukio hayo yakitokea na namba yako kuonekana, moja kwa moja unakuwa mtuhumiwa namba moja.

Wengi wamepewa kesi za mauaji, wizi bila kujua. Polisi wapo kazini, wanapoona vidhibiti wanakuchukua kwani hawatojua kama umehusika au la.

Kuweni makini ili usije kuingia matatizoni, simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi kama uzembe, utaishia pabaya.

Kutoka Cyber Crimes
SIMU YAKO JEMBE LAKO. SHARE UJUMBE HUU UMPE ONYO NA MWENZAKO

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
1d59fcbb513c2184e84cfccd512e4e45.jpg
 
Back
Top Bottom