Polisi na ukatili wa kutisha Igunga na Dar

Kwa kwel ht mi2 nmeona ITV,CHANNEL 10,MLIMANI TV
Daah!Huyo mama walivyomrusha km mzigo hyo siyo fail km kunam2 aliona ataniunga mkono
Haya BAKWATA kaz kwenu coz mlikuwa wa kwanza kula2mika
Wanaharakat kaz kwenu
Ha2taki uonevu wa design hii!
Ope mmeisoma
CHADEMA HONGERA KWA USHINDI BESIDE OV OL ZE BOUNDARY
 
Ni kweli polisi wetu wengi hawana reasoning capacity,hii pengine inachangiwa na upeo finyu ama mapokeo ya kazi zao.Njia ya haraka waliyojifunza ni ambush zaidi ya mbinu nyingine ya kumkamata mtuhumiwa pasipo kumzuru.Hii dhana ya ''kutii sheria pasipo shuruti'' inapaswa ifafanuliwe vizuri na wahusika wa pande zote yaani polisi na raia waitekeleze.

Hili la Mzee/wazee wastaafu EAC halikutisha sana kwani nimeona Mzee alivyokuwa shapu kwa kuchenga na kumyumbisha askari hatimae kutoweka.Issue ya mama aliyegongwa ngongwa na jinsi walivyomshika makalio na kumrusha ndani hapa ndipo pa kujiuliza.Hivi hakuna mbinu nyingine ya kudeal na hawa mnaosema wanasababisha uvunjifu wa amani hasa akina mama.

Ushauri; Pamoja na madhaifu ya polisi,tukiwa raia tunapaswa kujiepusha nao hawa wapiganaji.Tutii sheria na kuepuka ubishi usio na maana hasa unapotiwa nguvuni vinginevyo watatuua hawa maake kwao sifa ni jinsi gani wamemdhibiti wanae muita ''muarifu''.

Hii slogan ya polisi ya kutii sheria bila shuruti inanichefua sana. Polisi ndio wanavunja sheria kuliko raia wa kawaida na hawachukuliwi hatua lakini hao hao ndio wanahubiri utii wa sheria bila shuruti.

Narudia tena kusema tatizo kubwa la polisi wetu hasa wa vyeo vya chini ni upeo mdogo wa kielimu na uelewa finyu wa masuala ya sheria za nchi.
 
Kwani huyo mama ni wa CCM-A (Magamba) mpaka CCM-C (bakwata) walalamike?

Na pia hata kama ni wa CCM-C hawawezi kulalamika maana waliolifanya hilo ni CCM-D (Polisi) na sio CHADEMA

Nimeipenda ila umesahau CCM E(Usalama wa Taifa)!
 
Wana jf nimeangalia taarifa ya habari ITV kuna mwanamke amebebwa kwa nguvu na kutupwa kama mzigo kwenye gari la police.
Najiuliza BAKWATA wako wapi? mbona hawatoi tamko au kwa sababu si mkuu wa wilaya?au police wanayo hiyo haki?January makamba yuko wapi mbona alalamiki kwa watetezi wa haki za binadamu? au wametoa? natafuta picha ni upload muone .

Kwani huyo mama ni wa CCM?kama sio wa CCM Bakwata hawajamuona maana bakwata wako kwa ajiri ya CCM tu na si wengine,kwanza saa hizi wanakula pilau kwa KAFYUMU hivyo wako buzy.
 
Wakuu kama hujaliona lile tukio ni heri ubakie hivyo hivyo unaweza usiamini. Binafsi kama waliofanya vile wangekuwa wanawake walau ingepunguza hamaki, ila tobaaaaaaaa, ni polisi wanaume tena walimkamata sehemu ya kiuno na makalio then wakamrusha mithili ya gunia linavyopakiwa ndani ya gari. Acha tu, hata jamaa wa channel ten on monday ameliongelea hilo ingawa kwa kifupi sana sababu ya muda
 
ukweli ni kwamba DCalidhalilishwa kwani ana hadhi mama wa kawaida hadhi ataipata wapi? Usishangae akigeuziwa yeye kibao. Jana nilimsikia Manumba akisikitika kuhusu FC kudhalilishwa natamani angulizwa leo je, kile walichofanya vijana wake ni nini? TUTASHINDA DAIMA!!
 
Mwenye video clip aweke ili ambao hakutazama tv waone. Kwa kweli polisi wale wamemfanyia mama wa watu udhalilishaji wa hali ya juu na lazima atakuwa kaumia maana alirushiwa ndani ya gari kama mzigo! Mlaaniwe polisi wa Tanzania!
 
Utii wa sheria bila kushurutishwa,huyo punguani wenu angekuwa nyumbani kwake nani angemfuata?
 
HIli swala linabidi lijadiliwe kwa mapana DC kushikwa mkono bakwata walikuja juu kama moto wa kifuu,sasa kwa hili wako wapi??? inasikitisha yule mama kapigwa virungu akatupwa kama gunia kwenye gari daa alikuwa ajavaa kilemba alishika chupa ya maji safi ya kilimanjaro ile kubwa kabisa 1.5ltr
 
Wale vijana wa polisi ni wadogo sana kwa umri kumshika yule mama na kumpiga virugu kweli yule mama alikuwa wa kupigwa virungu akiwa hana lolote ? Wameondoka kwa kasi ya ajabu utadhani wana jambazi mh .Tanzania hii kweli hakuna haki .
 
Wana jf nimeangalia taarifa ya habari ITV kuna mwanamke amebebwa kwa nguvu na kutupwa kama mzigo kwenye gari la police.
Najiuliza BAKWATA wako wapi? mbona hawatoi tamko au kwa sababu si mkuu wa wilaya?au police wanayo hiyo haki?January makamba yuko wapi mbona alalamiki kwa watetezi wa haki za binadamu? au wametoa? natafuta picha ni upload muone .

Kwani kavuliwa hijab huyo hata Bakwata walalamike au kavuliwa nguo? katupwa kama mzigo kwa ujuvi wake, yeye anaambiwa panda juu ya gari anajidai kutoa mdomo, watu wako kazini anawapotezea muda, wamfanye nini? Hakudhalilishwa kajidhalilisha kujidai kujiingiza kwenye fujo.
 
nililona lile tukio, nikajiuliza ndiyo askari polisi wamemua kudhihirisha ukatili wao mbele ya kamera ya vyombo vya habari?

halafu wanalalamika hotuba ya waziri kivuli mambo ya ndani mhe. Lema ilikuwa na maneno makali
 
Kwani kavliwa hijab huyo hata Bakwata walalamike au kavuliwa nguo? katupwa kama mzigo kwa ujuvi wake, yeye anaambiwa panda juu ya gari anajidai kutoa mdomo, watu wako kazini anawapotezea muda, wamfanye nini? Hakudhalilishwa kajidhalilisha kujidai kujiingiza kwenye fujo.

Hivi kwanini hawa wanaolipwa buku 2 na nape akili zao wote ni za aina moja yani kama za Tambwe Hizza(wa CCM),FF sio kila kitu ni cha kubisha kuna vingine support nape hawezi kukutosa buku 2 yako
 
Hili jeshi linahitaji kulekebishwa mfumo wake b'se kila kukicha hawaishi kulalamikiwa juu ya uvunjivu wa haki za binadamu, Cha ajabu watawala wamewafumbia macho huku raia wakisulubika!

Na wewe unatakiwa kurekebishwa kiswahili chako.
 
inackitisha kwa kweli...hata km n huo uhalf lkn kwa style ile...hapana!!
 
Back
Top Bottom