figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,895
Kumbe sio kila Polisi ana roho mbaya wala katili. Wapo Polisi baadhi wema.
Yupo Rasha mmoja kwa Polisi 1,000. Sema watu kama hawa wanakomolewa kwa kupelekwa Vijiji vya ndani ili wasionekane kitaifa.
Rasha alitakiwa ahudumie japo Wilaya nzima sio kata tu.
Wanaotenda mema bila kujali mapito yao, tuwatie moyo
Nilimshuhudia akivusha wanafunzi kwenye mto uliofulika wengine akiwabeba Mgongoni.
Mungu amlipe nini?
Polisi Kata wa Kata ya Usangule Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Michael Rasha akiongea na kumfariji mtoto Erick Hongera (6 ) ambaye amekuwa akikaa kwa upweke katika maeneo ya Shule.
Mtoto Erick amekuwa na mazoea ya kwenda shule ya Msingi Manda Juu na kukaa nje ya jengo la shule hiyo kwa upweke na mfadhaiko kutokana na wazazi wake kutokumpeleka shule.
Mkaguzi Rasha ameongea nae na kumfariji ili kuona ni jinsi gani anaweza kumsaidia aweze kujiunga na watoto wenzake ili kupata haki yake ya msingi ya kusoma.
Katika harakati za kumsaidia mtoto huyo, Mkaguzi Rasha amechukua hatua ya kwenda kuongea na wazazi wake ili kujua changamoto na kuitafutia ufumbuzi ili mtoto huyo aweze kwenda shule kama wanafunzi wenzake.
Credit: Picha na caption nimeitoa Channel ten