Polisi Mbeya wamkamata Msabila Raulent Leonsia akituhumiwa kutengeneza silaha (gobore) kienyeji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na maafisa maliasili – TAWA Pori la Akiba Rungwa, linamshikilia Msabila Raulent Leonsia [48] Mkazi wa Kambi Katoto Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya kwa tuhuma ya kupatikana na silaha – gobore mbili ambazo zimetengenezwa kienyeji.

Mtuhumiwa alikamatwa Aprili 15, 2023 katika misako iliyofanyika huko kambi katoto na baada ya kupekuliwa ndipo alikutwa na silaha hizo mbili pamoja na vifaa mbalimbali vya kutengenezea silaha aina ya gobore ambavyo ni:-
  • Baruti.
  • Misumeno midogo
  • Goroli ambazo hutumika kama risasi
  • Nyundo
  • Vyuma vidogo vidogo
Aidha, ufuatiliaji ulifanyika na kubaini kuwa mtuhumiwa licha ya kutengeneza silaha pia anajihusisha na ulimaji wa zao haramu la bhangi ambapo katika kambi yake iliyopo ndani ya hifadhi Rungwa alikutwa amepanda miche 60 ya bhangi. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

NOTI BANDIA
Wakati huohuo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamini Kuzaga amesema wanamshikilia Paul Ezron [33] Mkazi wa Mwenge Jijini Mbeya kwa tuhuma ya kupatikana na vifaa mbalimbali vya kutengenezea noti bandia.

Mtuhumiwa alikamatwa Aprili 17, 2023 katika misako iliyofanyika maeneo ya Mwanjelwa Jijini Mbeya na katika upekuzi uliofanyika katika chumba alichopanga alikutwa na vifaa vya kutengenezea noti bandia:-
  • Pasi ya umeme moja,
  • Gundi aina ya Solo,
  • Tape 02,
  • Gundi moja ya maji,
  • Vipande vya karatasi mfano wa fedha rangi nyeusi bunda 02,
  • Vimiminika ambavyo ni madawa na kemikali chupa 04.
Pia katika upekuzi amekutwa na vifaa vya Hospitalini ambavyo ni sindano za binadamu na groves. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani.

DEREVA ATELEKEZA GARI NA KUKIMBIA
Aidha katika misako dhidi ya wahalifu wa bidhaa za magendo, uliofanyika Aprili 15, 2023 huko Uzuo, Kata ya Iyunga mapinduzi, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kukamata gari yenye namba za usajili T.956 AWA aina ya Toyota Mark II iliyokuwa ikitokea Tunduma kuelekea Mbeya Mjini.

Dereva wa gari hilo baada ya kusimamishwa na askari alitelekeza gari hilo na baada ya kupekua ndani ya gari zilikutwa mali mbalimbali za magendo ambazo ni:-
  • Vitenge ambavyo havijalipiwa ushuru
  • Nyavu za kuvulia Samaki dazani 40 zikiwa ndani ya mifuko ya salfeti,
  • Mifuko ya Nylon iliyopigwa marufuku nchini vifungashio dazani 10
Jeshi la Polisi linaendelea na msako ili kubaini dereva wa gari hilo na mmiliki halali wa gari hilo.

Aidha, Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata mali za wizi Pikipiki mbili zenye namba za usajili MC.435 DJA aina ya Sanlg na MC.798 BNW aina ya Sanlg ambapo madereva wa Pikipiki hizo mara baada ya kuwaona askari walitelekeza Pikipiki hizo na kukimbia.

Tunaendelea kufuatilia kwa kushirikiana na TRA ili kubaini wamiliki wa Pikipiki hizo. Pia tunaendelea kutoa wito kwa wananchi kwa yeyote aliyeibiwa Pikipiki kufika kituo cha Polisi Rujewa Wilaya ya Mbarali kwa ajili ya utambuzi wa Pikipiki hizo.
 
Hiyi nch viongoz wetu wangekuwa seriou sizani kama vijana wangetegemea ajira coz kuna watu wana vipawa ila shida hawana paku endelezwa ama kwel ngoz nyeus ina laaana ya asili fvack all leader of african
 
Back
Top Bottom