Polisi jamii wanalipwa na nani?

Polisi jamii wanalipwa na nani?

Polisi jamii is not the same as sungu-sungu, but they are a like.
Tofauti yao ni kuwa Police Jamii ni mfumo uliobuniwa na Police na kutambulishwa kwa raia wakati sungusungu ni mfumo ulionzishwa na raia, wakajijengea taratibu za namna ya kuundesha.
Kwa upande wa malipo sidhani kama kuna utaratibu wowote wa maana unaotumika, labda kama watendaji wa kata wanahusishwa katika sualla hilo la malipo yao ndiyo litawezekana.
 
Kila mtu anajua kuwa mishahara ni midogo mno
kwa polisi wa Tanzania hadi wengine kudai rushwa
na hata kushiriki uhalifu ili wapate kipato

Sasa ghafla bin vuuu kuna wimbi la watu ambao wanaitwa
'polisi jamii' wanavaa uniform na wamesambaa jiji zima
kwa Daresalaam....
nasikia kwamba hawa watu hawalipwi ni wanajitolea

haingii akilini mtu kujitolea siku nzima au wiki nzima
kufanya kazi ya kujitolea bila malipo
je hawa watu wanalipwa?
na kama hawalipwi wanaishije?
na hatari za kuwa na hili jeshi lisilo rasmi ni zipi?

sasa naona wameanza kukamata magari barabarani pia
what next huko mbeleni?

Niliwahi kuwaona kariakoo..afu wana confidence ya ajabu kuliko hata polisi wenyewe

Wamevaa na flana zao zimeandikwa polisi jamii....kunasiku utakuja kusikia wememilikishwa silaha...haitakuwa ajabu kwa Tanzania.
 
Sungusungu wako juu zaid ya Polisi jamii,kwani apo polisi jamii mijambazi kibao imejificha humo.hamnaga kazi ya kujitolea siku hiz.
 
Wanajilipa wenyewe,green guard watarajiwa
 
malipo yao huwa ni hivi,hususani hawa wanaowasaidia trafic polisi,unapopaki,simamisha gari sehemu ovyo na kusababisha foleni hususani kwa daladala,wanakukamata/kuandika namba ya gari na kumpelekea trafik,trafiki atakapo kukamata ukimpa ki2 kidogo naye ndio mgao wake humo humo,au ukiona kwa trafiki itakuwa hela nyingi una mtafuta yeye una mpa buku 2,maisha yanaendelea!na mtaji wao mkubwa ni daladala,wanazipata japo nao kwa kiasi fulani wanasaidia kwenye foleni.Hawa wengine wa mtaani wa kulinda ucku kwa kule uswahilini kila nyumba inachangia pesa kwa mwezi.
 
Sungusungu hadi leo wanatumika katika baadhi ya mikoa, na ni kweli wanafanya kazi vizuri kwenye maeneo husika, ingawa kuna hoja ya mchangiaji mmoja kuwa sungusungu huwa hawana mafunzo ni kweli kabisa hivyo mara nyingine hutumia nguvu kubwa kwa washukiwa hata huleta vifo au ulemavu.

Kuhusu polisi jamii na weza kusema wazo la kuanzisha kunauwezekano lilikuwa zuri, ila na fikiri mpangilio wake haupo vizuri, kwa kuwa haupo kisheria, pia hata hawa wahusika pia hawana mafunzo.

Jambo ambalo linanisikitisha ni kwamba kama hawa polisi jamii hawalipwi basi hapa ndio tunatengeneza njia nyingine ya uhalifu wa kula rushwa kwa kuwa haiwezekani kabisa mtu mwenye familia yake afanye kazi ya kujitolea kwa muda wote wa maisha yake ya kila siku.

Lakini na kwenda mbali na kujiuliza hata kama watakuwa wanalipwa then, malipo yao yanatoka kwenye bajeti gani? na kama hizi halmashauri zinauwezo wa kuwalipa then sioni kwanini washindwe kutumia watu waliopitia mafunzo kama mgambo au vijana wetu wa JKT kufanya kazi hii kwa kipindi ambacho wanangoja kuchanguliwa kwenda kwenye sehemu zao za ajira.

Nilisema mwanzo kuwa mara nyingi sisi watanzania tunapenda kurupuka kwenye mambo yetu na mwisho wa siku mambo hutushinda na huleta madhara kwa taifa, je unakumbuka wakati fulani kulikuwa na wale jamaa wanakamata magari yanayo vunja sheria, ilikwenda vizuri lakini mwisho wa siku wakawa ndio wala rushwa wakubwa na kibaya zaidi walianza kutekwa na kupigwa na watu wa daladala.

Sasa na uhakika kwenye jambo hili kama kuna malipo kweli ni bora kuchukua vijana wetu wa mgambo au JKT kuweza kufanya hili jambo na si kwa watu wa mtaani, kwani kwa wingi wa hawa polisi jamii naona anguko la kushindwa kuwalipa na kwa malalamiko ya wanajamvi kuwa haya jamaa wengine ni wahalifu sioni kama watatusaidia ila ni bomu jingine tunatengeneza na wakati litakapo kuja lipuka...............

So serekali inapaswa kuhakikisha hawa polisi wanaolipwa pesa za walipa kodi wanafanya kazi yao vizuri na si kutumika kwenye mambo yenu ya kisiasa tuu wawajibike kulinda wananchi na mali zao wanalipwa kwa jambo hilo, si kungoja wakati wa uchaguzi kwenda kuiba kura na kula rushwa hovyo kiasi wahalifu wawe wengi mpaka tupate msaada kwa wananchi wa kujitolea.

So nitaleta hoja binafsi kupiga kura ya kutokuwa na imani na uwezo wa POLISI TANZANIA hivyo wote wajiuzuru tuajiri hao vijana wa polisi jamii inaonyesha wanamoyo wa kulinda nchi yao zaidi ya hawa policcm
 
[h=2] community policing[/h] POLISI JAMII/ULINZI SHIRIKISHI:
Polisi Jamii au Ulinzi Shirikishi(community policing) ni mkakati wa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi. Lengo kuu la mkakati huo ni kuweka mazingira ya ushirikiano wa dhati baina ya wananchi na Polisi. Kwa misingi hiyo mpango wa Polisi Jamii ni utaratibu mpya wa utendaji kazi wa polisi. Ni mpango kamambe ambao unalenga kuleta mabadiliko ya namna Idara ya Polisi inavyohusiana na jamii, falsafa mpya inayopanua malengo ya Polisi kutoka kwenye mtizamo wa kadri (limited) unaolega kwenye tukio moja au pengine aina moja tu ya uhalifu kwenda kwenye mtizamo mpana unaohamasisha Jeshi la Polisi kulenga kwenye ufumbuzi wa matatizo ya jamii kwa ujumla wake: ikiwemo uhalifu wenyewe, woga wa kudhurika na uhalifu (fear of victimization), vurugu na hali ya wasi wasi ndani ya jamii na kuzorota au kutojali kwa jamii.


CHIMBUKO LA DHANA NA IMANI (FALSAFA) YA POLISI JAMII:
Mpango wa polisi jamii ni mtizamo madhubuti wa jinsi ya kupanga mikakati ya utendaji ya polisi; msingi wake mkuu ukiwa ni imani kuwa askari Polisi wakifanya kazi pamoja na wananchi – raia wa kawaida, wanaweza kusaidiana kutatua matatizo yanayokabili jamii yanayohusu uhalifu, woga kuhusu uhalifu (fear of victimization), vurugu ndani ya jamii, pamoja na jamii kuzorota (social decay) kutokana na kutojali. Chini ya mpango huu polisi wanatakiwa kuweka misingi ya ushirikiano wa karibu kabisa baina yao na raia wema katika jamii. Ushirikiano wa aina hiyo utawawezesha raia wema kuwa na kauli kubwa zaidi katika uwekaji wa mipango na malengo ya polisi na kwa njia hiyo kuwahusisha kikamilifu katika jitihada za kuboresha hali na thamani ya maisha (quality of life) katika sehemu wanazoishi.
Majeshi ya Polisi mengi duniani yameanza kutizama upya sera zake za kiutendaji kwa lengo la kuweka taratibu madhubuti zenye kuzingatia misingi ya Polisi Jamii. Wimbi la mabadiliko haya linatokana na kutambua uzito wa tatizo la uhalifu katika karne hii ya 21. Uhalifu na wahalifu katika ulimwengu wa sasa vimejitokeza kuwa ni changamoto la aina yake. Uhalifu unafanyika kwa njia za kitaalam zaidi (sophisticated) na hasa kwa kutumia mitandao ya kisasa inayotokana na maendeleo katika nyanja mbali mbali za sayansi na teknolojia. Njia za jadi za kukabiliana na uhalifu huu zinaonekana kutokuwa jibu la kutosha.
Mathalan, doria ya polisi mitaani ni moja ya njia za jadi za kukabiliana na uhalifu. Lengo lake ni kuzuia uhalifu; kuwahi kwenye matukio ya uhalifu ili kuwahoji mashahidi, kukamata watuhumiwa, kupeleleza na kukusanya ushahidi. Uchambuzi hata hivyo umeonyesha kuwa ingawaje hatua zote hizo ni muhimu haziwezi kwa peke yake kuwa ni ufumbuzi wa tatizo la uhalifu.
MISINGI YA POLISI JAMII/ULINZI SHIRIKISHI:
Msingi mkuu wa mpango wa Polisi Jamii ni imani (falsafa) kuwa uboreshaji wa maisha ya jamii kwa kuiondolea jamii kero ya uhalifu; unaweza kupatikana kutokana na jamii kufanya kazi pamoja na Jeshi la Polisi. Polisi wanakuwa ni washauri, wawezeshaji, wasimamizi na waimarishaji wa jitihada za jamii za kuondokana na kero za uhalifu.


KWA NINI MPANGO WA POLISI JAMII NI MUHIMU?
Uanzishaji wa Polisi Jamii ni changamoto lisiloepukika kwa sasa. Mpango huu umejitokeza kuwa na umuhimu wa aina yake kwa sababu katika mazingira ya nyakati zetu hizi; ya maendeleo ya sayansi na teknologia wahalifu hutumia mbinu za kisasa kama vile teknologia ya mawasiliano, usafiri n.k. kufanikisha malengo yao maovu. Aidha wahalifu nao ni watu wenye akili. Huunda asasi za aina mbalimbali zilizo rasmi na zisizo rasmi, pamoja na mitandao kemkem ya kufanikisha malengo yao ya kiuhalifu. Haya yametokea kwa sababu kuu tatu tutakazochambua hivi punde.
Kwanza wahalifu hutumia sheria kufanikisha maelengo yao na kwa hiyo sheria peke yake haiwezi kuleta ufumbuzi wa matatizo ya uhalifu. Kutokana na mapato ya vitendo vyao viovu wahalifu huweza kuwakodi washauri wa kisheria waliobobea ambao huwatumia kufanikisha malengo yao. Mathalan, si aghalabu wezi wa magari kuhalalisha miliki au uuzaji wa magari waliyoiba kwa kutumia wanasheria. Vile vile wahalifu wanaelewa sheria za ushahidi hususan; wajibu wa mshtaki kuthibitisha shtaka bila kuacha mwanya wo wote wa mashaka (burden of proof). Pamoja hayo wahalifu huunda asasi zilizo halali kisheria kama vile makampuni, shughuli za biashara (business enterprises) n.k kwa ajili ya kufanikisha malengo yao ya kiuhalifu; mfano mzuri ni usafishaji wa fedha haramu kwa kuziingiza katika shughuli halali za kibiashara (money laundering).
Pili wahalifu wanafahamu taratibu za kiserikali. Wanafahamu sheria zinavyotungwa na jinsi zinavyopaswa kutekelezwa. Wanafahamu mbinu za kuhamasisha maoni na mawazo yanayowaunga mkono. Wahalifu waliobobea huweza hata kupanga taratibu za kuwahamasisha wapiga kura ndani ya jamii na kwa hivyo kufanikisha malengo yao.
Sababu ya tatu ni kuwa uhalifu hutoa ajira kwa wale walioukumbatia. Hali hii hujenga mtandao wa utegemezi juu ya mapato yanayotokana na uhalifu. Kwa njia hiyo wahalifu huweka mazingira ambapo kuna kundi fulani miongoni mwa jamii litakalowaunga mkono.
Pengine mambo hayo matatu miongoni mwa mengine hufanya changamoto la kuanzisha mpango wa polisi jamii lisiweze kuepukika. Kama wahalifu wanafahamu sheria na taratibu za serikali na huzitumia kwa manufaa yao, polisi wakitegemea sheria peke yake mafanikio yao ya kupata ufumbuzi wa matatizo ya uhalifu yatakuwa ni ya kadri kwa vile wanatumia chombo hicho hicho wanachotumia wahalifu.


FAIDA ZA MFUMO WA POLISI JAMII
Mfumo wa polisi jamii una faida kuu zifuatazo ambazo haziwezi kupatikana kikamilifu chini ya mfumo uliozoeleka wa utendaji wa kazi za polisi. Faida hizi ni: polisi kufanya kazi na wananchi kwa pamoja, kujenga mazingira ya kuaminiana, kuweka mazingira ya ubia (partnership) baina ya polisi na jamii, kuhamasisha ubunifu na kupata ufumbuzi stahimilivu (sustainable) wa kero za wananchi. Tutachambua kwa ufupi faida hizi.


UBIA (PARTNERSHIP) BAINA YA POLISI NA JAMII
Tofauti moja kubwa iliyiopo kati ya utaratibu uliozoeleka na mfumo wa polisi jamii inahusu mipango ya utendaji ya polisi. Wakati mipango ya polisi kwa utaratibu uliozoeleka huzingatia malengo na matakwa ya Idara ya Polisi peke yake, chini ya mfumo wa polisi jamii mipango ya utendaji hutia maanani matakwa ya jamii kwa vile huandaliwa na wananchi wa sehemu hiyo wakishirikiana na Askari Polisi Kata. Mantiki ya utaratibu huu inaweza kutoeleweka vizuri katika utaratibu uliozoeleka (traditional policing). Inaweza ikatokea hisia kuwa jamii inaweza kukwamisha malengo na mipango ya polisi. Hii si kweli kamwe. Kinachotokea, kinadharia ni kuwa askari polisi kata huwaelewesha wananchi katika sehemu au mtaa wake kuwa iwapo mtatoa ushirikiano na taarifa; matokeo yake mtakuwa na nafasi ya kushiriki kikamilifu katika kupanga malengo ya polisi katika mtaa wenu. Askari Polisi Kata mzuri hufahamu na kukiri kuwa wananchi si kikwazo kwa malengo ya polisi. Badala yake ni hazina muhimu ambayo inaweza kuchotwa kwa njia ya jamii kushiriki kikamilifu katika mipango ya polisi kwa lengo ka kufanya jamii hiyo iishi katika mazingira ya utulivu. Mazingira ambapo uhalifu umedhibitiwa kikamilifu.
Utaratibu na dhana nzima ya wananchi kushiriki katika kuandaa mipango inatakiwa ifikishwe kwa wananchi ili waweze kutambua kuwa mchango wao unathaminiwa. Changamoto kubwa iliyopo kwa askari kata ni pamoja na kushirikisha wananchi moja kwa moja katika ufumbuzi wa matatizo yanayokabili mtaa wao au sehemu yao wanayoishi. Mpango wa polisi jamii siyo tu huwafanya wananchi kuwa ni macho na masikio ya polisi kwa saa 24 kila siku bali pia huhamasihsa wananchi kushiriki katika ufumbuzi wa matatizo yanayojitokeza ndani ya jamii yao. Pale ambapo mfumo wa polisi jamii umepokelewa kwa mafanikio na wananchi; baadhi yao wanaweza kujitolea katika mambo mbalimbali yaliyoko ndani ya mpango wao kama vile wazazi kusimamia mipango ya kuendesha michezo ya vijana wa mtaa huo; wafanya biashara kujitolea vifaa vya michezo n.k. lengo likiwa ni kuwashughulisha vijana waondokane na kukaa bure na hivyo kujiingiza katika matendo yasiyofaa kama vile: kuvuta bangi, unywaji pombe n.k., mambo ambayo baadye huweza kuzaa uhalifu.

Neno ‘community policing’ limekuwa na tafsiri ya ‘Polisi Jamii’ kwa muda. Kwa sasa kuna mwelekeo wa tafsiri mpya ambayo ni ‘Ulinzi Shirikishi’. Pengine tafsiri hii mpya ni nzuri zaidi. Maana haiathiriki kwa tafsiri zote mbili.
 
Kila mtu anajua kuwa mishahara ni midogo mno
kwa polisi wa Tanzania hadi wengine kudai rushwa
na hata kushiriki uhalifu ili wapate kipato

Sasa ghafla bin vuuu kuna wimbi la watu ambao wanaitwa
'polisi jamii' wanavaa uniform na wamesambaa jiji zima
kwa Daresalaam....
nasikia kwamba hawa watu hawalipwi ni wanajitolea

haingii akilini mtu kujitolea siku nzima au wiki nzima
kufanya kazi ya kujitolea bila malipo
je hawa watu wanalipwa?
na kama hawalipwi wanaishije?
na hatari za kuwa na hili jeshi lisilo rasmi ni zipi?

sasa naona wameanza kukamata magari barabarani pia
what next huko mbeleni?
Wanasema ukiwa umeajiri kondakta na dereva halafu huwalipi vizuri na hawalalamiki,basi watakuwa wanajilipa wenyewe. Mwisho utalikuta gari /basi lako juu ya mawe kama sio gereji likiwa taabani.

Mkuu hili swala la polisi jamii halikufanyiwa upembuzi yakinifu kabla ya utekelezaji. Soon madhara yake yatajulikana kwani kuna baadhi ya maeneo raia washaanza onjo joto ya jiwe. Serikali inayokwepa majukumu yake siku zote huja na mipango mibovu kama hii.
MUNGU IBARIKI TZ.
 
Kila mtu anajua kuwa mishahara ni midogo mno
kwa polisi wa Tanzania hadi wengine kudai rushwa
na hata kushiriki uhalifu ili wapate kipato

Sasa ghafla bin vuuu kuna wimbi la watu ambao wanaitwa
'polisi jamii' wanavaa uniform na wamesambaa jiji zima
kwa Daresalaam....
nasikia kwamba hawa watu hawalipwi ni wanajitolea

haingii akilini mtu kujitolea siku nzima au wiki nzima
kufanya kazi ya kujitolea bila malipo
je hawa watu wanalipwa?
na kama hawalipwi wanaishije?
na hatari za kuwa na hili jeshi lisilo rasmi ni zipi?

sasa naona wameanza kukamata magari barabarani pia
what next huko mbeleni?

Niisivyo mimi, hawa watu hawana maslahi yoyote ya maana ila kunakupoozwa kidogo, kuna chochote kitu kutokana na kodi za wananchi. Hawa watu wanachukuliwa kulinda sehemu husika na kupewa kitu kidogo ingawa si ajira as we can col it.
Hawa watu hawajajitolea, wengi wao hawana hata ivo vibarua, so huponea hapo kwa kupata chochote kitu. Dunia ya sasa ni ngumu mtu kujitolea muda wake wote for others bro.
Hatari ya kuwa na hawa watu, kwanza wengi wao wanachukuliwa na kufanya polisi jamii huku wakiwa hawana dhamira ya kuwa polisi jamii. Wengi wanawaza pesa na mambo mengi maovu. Mtu wa aina iyo, atapata nafasi nzuri ya kufanya uovu wake kwa urahisi huku wengine wakidhani ni polisi jamii mfano kuiba, kudhulumu nk.
Kitakachoendelea huko mbeleni, hawa vijana wataongezeka na kusababisha ongezeko la vijana wababe kwenye jamii za watu. Wataweza kufanya maovu mengi huku wakijifunika kwenye shuka la polisi jamii.
Hivo ndivyo nionavyo mie.
 
Niisivyo mimi, hawa watu hawana maslahi yoyote ya maana ila kunakupoozwa kidogo, kuna mchango watu wanatozwa na wajumbe wao kwenye maeneo yao ya kuishi na hawa watu wanachukuliwa kulinda sehemu husika na kupewa kitu kidogo ingawa si ajira as we can col it.
Hawa watu hawajajitolea, wengi wao hawana hata ivo vibarua, so huponea hapo kwa kupata chochote kitu. Dunia ya sasa ni ngumu mtu kujitolea muda wake wote for others bro.
Hatari ya kuwa na hawa watu, kwanza wengi wao wanachukuliwa na kufanya polisi jamii huku wakiwa hawana dhamira ya kuwa polisi jamii. Wengi wanawaza pesa na mambo mengi maovu. Mtu wa aina iyo, atapata nafasi nzuri ya kufanya uovu wake kwa urahisi huku wengine wakidhani ni polisi jamii mfano kuiba, kudhulumu nk.
Kitakachoendelea huko mbeleni, hawa vijana wataongezeka na kusababisha ongezeko la vijana wababe kwenye jamii za watu. Wataweza kufanya maovu mengi huku wakijifunika kwenye shuka la polisi jamii.
Hivo ndivyo nionavyo mie.

Wale tunatozwa wa sungu sungu
 
Polisi jamii ndio wezi wenyewe usiombe ukutane nao usiku watakuchukulia hadi magwede aka masimbi aka jiti,fisi na karume
 
Pale mtaani kwetu kuna hiyo makitu inaitwa polisi jamii,
na kwambia ni majanga
kwa kuwa kila mwezi mjumbe anapita kila nyumba akikusanya hela
sh elfu kumi kumi kwa ajili ya hiyo polisi jamii.

Inatia hasira sana,
nyumba zipo zaidi ya hamsini, sijaweza kufanya utafiti kama ni kila mtu
analipa hiyo hela au wanatukomalia sie watoka usiku na kurudi usiku as
huwa hatujui hata story za mtaani.

Nasikia kiongozi wao ni polisi mmoja ambaye ni mhasibu,
jamaa keshajilimbikizia mali kibao amejenga hadi maghorofa
pale mtaani eti zinaitwa ni hostel, as pana chuo cha st joseph jirani.

Mwezi majuzi kuna watu kama kumi walikuwa wameweka ngumu kutoa
hiyo hela ikabidi wasombwe wakatiwa kituo cha polisi.
 
Haijitoshelezi
maswali yangu hayajibiwi humo

Mkuu wale ndo wala rushwa wakubwa na vibaraka wa trafiki... wananikera wakiwa na trafiki wanajifanya vimbelembele kuchomoa funguo kwenye gari.. kuna mmoja nilitaka kumpasua kichwa pale chama buguruni.. Wale ni WALA RUSHA tu. Period..
 
-wana maconfo ya ajabu!
-jeuri kwisha kazi
-wanamaamini kila kitu kipo chini yao hata pochi yako ya mkononi
-wanaweza kukatisha ruti ya daladala liende mahali fulani na kweli haliendi,mbezi mwisho wanaisoma hii
-wanaamini foleni ni miongoni mwa majukumu yao ya kikazi,uliza wanaopita njia ya kigogo wanamjua yule dogo pale round about!
-kale kakoti kapo ka kijani ni leseni yao ya kufanya uhalifu mwingi tu
-zaidi ya kuwa hawajui haki na sheria hawataki kuamini kuwa raia wanajua haki zao,hapo msambwe wake mpk lije greda!
yani mradi kero tupu!
 
Back
Top Bottom