Basi hawa nadhani watakuwa ni vibarua kutokana na kodi za wananchi.
Polisi jamii wa kwa Mtogole ni zaidi ya wahalifu
Hawa wanakula faini ya papo kwa papo mfano anakufuma unakunya kichochoroni faini Tsh.50,000/= anakula yeye
Pale mtaani kwetu kuna hiyo makitu inaitwa polisi jamii,
na kwambia ni majanga
kwa kuwa kila mwezi mjumbe anapita kila nyumba akikusanya hela
sh elfu kumi kumi kwa ajili ya hiyo polisi jamii.
Inatia hasira sana,
nyumba zipo zaidi ya hamsini, sijaweza kufanya utafiti kama ni kila mtu
analipa hiyo hela au wanatukomalia sie watoka usiku na kurudi usiku as
huwa hatujui hata story za mtaani.
Nasikia kiongozi wao ni polisi mmoja ambaye ni mhasibu,
jamaa keshajilimbikizia mali kibao amejenga hadi maghorofa
pale mtaani eti zinaitwa ni hostel, as pana chuo cha st joseph jirani.
Mwezi majuzi kuna watu kama kumi walikuwa wameweka ngumu kutoa
hiyo hela ikabidi wasombwe wakatiwa kituo cha polisi.
we Mamndenyi weweeee?
elfu kumi?
mnalipa???
khaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!
aisee mi wangeisikia kwenye bomba, la wanipe sheria inayoruhusu kukusanya mapato ya namna hiyo kwa wananchi
then najizatiti kiulinzi maana ndo vibaka wenyewe, huku nikimpiga biti mwenyekiti ole wako niibiwe hata kijiko...
Katika mikoa mikubwa kma dsm kamati za ulinzi na usalama mkoa huwa wanaomba misaada kwa makampuni na wafanyabiashara wakubwa kila mwezi kuchangia mfuko wa pj
Niisivyo mimi, hawa watu hawana maslahi yoyote ya maana ila kunakupoozwa kidogo, kuna chochote kitu kutokana na kodi za wananchi. Hawa watu wanachukuliwa kulinda sehemu husika na kupewa kitu kidogo ingawa si ajira as we can col it.
Hawa watu hawajajitolea, wengi wao hawana hata ivo vibarua, so huponea hapo kwa kupata chochote kitu. Dunia ya sasa ni ngumu mtu kujitolea muda wake wote for others bro.
Hatari ya kuwa na hawa watu, kwanza wengi wao wanachukuliwa na kufanya polisi jamii huku wakiwa hawana dhamira ya kuwa polisi jamii. Wengi wanawaza pesa na mambo mengi maovu. Mtu wa aina iyo, atapata nafasi nzuri ya kufanya uovu wake kwa urahisi huku wengine wakidhani ni polisi jamii mfano kuiba, kudhulumu nk.
Kitakachoendelea huko mbeleni, hawa vijana wataongezeka na kusababisha ongezeko la vijana wababe kwenye jamii za watu. Wataweza kufanya maovu mengi huku wakijifunika kwenye shuka la polisi jamii.
Hivo ndivyo nionavyo mie.
we Mamndenyi weweeee?
elfu kumi?
mnalipa???
khaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!
aisee mi wangeisikia kwenye bomba, la wanipe sheria inayoruhusu kukusanya mapato ya namna hiyo kwa wananchi
then najizatiti kiulinzi maana ndo vibaka wenyewe, huku nikimpiga biti mwenyekiti ole wako niibiwe hata kijiko...
-wana maconfo ya ajabu!
-jeuri kwisha kazi
-wanamaamini kila kitu kipo chini yao hata pochi yako ya mkononi
-wanaweza kukatisha ruti ya daladala liende mahali fulani na kweli haliendi,mbezi mwisho wanaisoma hii
-wanaamini foleni ni miongoni mwa majukumu yao ya kikazi,uliza wanaopita njia ya kigogo wanamjua yule dogo pale round about!
-kale kakoti kapo ka kijani ni leseni yao ya kufanya uhalifu mwingi tu
-zaidi ya kuwa hawajui haki na sheria hawataki kuamini kuwa raia wanajua haki zao,hapo msambwe wake mpk lije greda!
yani mradi kero tupu!