Polisi dar waua tena

ABEDNEGO

Senior Member
Aug 20, 2009
109
30
SNC00153.jpg Ilikuwa majira ya saa nne na nusu usiku wa jana,Polisi wa kituo cha Oysterbay walipotumia risasi za moto kuumua kijana Octavian fundi magari eneo la Victoria karibu na nyumba za viongozi.Polisi aliyehusika na tukio hilo anajulikana kwa jina moja la Constable Crycipin.Ambaye alitumia bastola yake kumpiga na kumuua kwa mabishano yasiyomhusu kijana huyo.Mashuhuda waliokuwa katika eneo la tukio wanadai kuwa polisi hao waliletwa kwenye gari mbili aina ya RAV 4 na cresta(Namba zimehifadhiwa) na wasichana wawili (Changudoa) waliokuwa wakimsaka mtoto wao waliyedai alichukuliwa na babake bila ya ridhaa yao.Ndipo katika majibishano ya mdomo askari huyo alichomoa bastola na kumuua fundi magari huyo ambaye alikuwa hahusiki na ugomvi huo.Cha kushangaza na kukatisha tamaa ni jinsi polisi walivyolichukulia kwa urahisi jambo hilo kiasi ya kwamba Muuaaji hakufanyiwa gwaride la utambulisho wala kutoa maelezo kituoni.
Askari Muuaji Constable Cricipin huyu hapa (Angalia attachment):mad2:
 
Mmh jamahi hawa police mauwaji ya wasio na hatia hadi lini!!!!

Pole kwa wafiwa kwa kuondokewa na mpendwa wenu!

lakini ilikuwaje huyo kijana auwawe kwani yeye alikuwa anawaamulia hao walio kuwa wanagombana ama ilikuwakuwaje? ama yeye ndio baba wa huyo mtoto aliekuwa anagombaniwa na mtoto mwenyewe ni wa umri gani?
Huyo askari aliefanya hayo mauwani ni mmoja wa mabwana wa hao machangu au??? kwanini atumie silaha yake ndivyo sivyo??

IGP Mwema tunaomba majibu ama tusubiri tume ya uchunguzi iundwe majibu mtayapata mwakani uchaguzi ukipita!
nia aibu kwa jeshi la police tuna maaskari wasio jua wajibu wao naomba washughulikiwe ipasavyo kwa muujibu wa sheria za nchi yetu
 
Jamani hii hoja ya mwanajamii mbona mmeichunia? Ni issue sensitive sana, hebu ikodoleeni
 
Naomba muache kukimbilia kuwalaumu polisi. Kwenye hii issue, huyu mtu aliyeuwawa alikuwa na genge la watekaji nyara. Walikuwa wamemteka baba wa mtoto. Kwa hiyo Polisi walikwenda pale kuokoa mtu ambaye ametekwa na hili genge. Huyu muhuni akaanza kupelekeshana na polisi mwenye silaha. Nia yake ilikuwa nini kama si kumnyang'anya ili afanye uhalifu zaidi ? Ukitilia maanani kwamba tayari alikuwa ameshafanya kosa jingine la jinai la kumteka mtu.

Kwa hiyo, pamoja na kuwa hatujui kama ni polisi huyu aliyemuua huyu mtekaji nyara, Nadhani polisi wetu wapewe benefit of the doubt kwanza. Walifuatwa kituoni ikiwa imeripotiwa kwamba kuna tukio la utekaji. Wamewakuta watekaji, watekaji wanataka kupokonya silaha!!!! Ulitaka waachwe waendelee kuteka na kuua wengine????? Give me break
 
dah
fanyia editing hiyo picha ifit ktk size tuweze kumkagua huyu krispin.

Ila mtoa hoja ametoa hoja yake kama anakimbia vile. je kuna nini kimemsukuma na maelezo ya hii picha ameyapata wapi na ameipataje picha? nadhani pia ana uhakika na anachokisema? kuna mashahidi walikuwepo pale, gari zilikuwepo na kamera ya cctv ilirekodi kila hatua.

tunataka maelezo ya kina ili tusije tukaanza kujadili hewani hewani
 
View attachment 10310Ilikuwa majira ya saa nne na nusu usiku wa jana,Polisi wa kituo cha Oysterbay walipotumia risasi za moto kuumua kijana Octavian fundi magari eneo la Victoria karibu na nyumba za viongozi.Polisi aliyehusika na tukio hilo anajulikana kwa jina moja la Constable Crycipin.Ambaye alitumia bastola yake kumpiga na kumuua kwa mabishano yasiyomhusu kijana huyo.Mashuhuda waliokuwa katika eneo la tukio wanadai kuwa polisi hao waliletwa kwenye gari mbili aina ya RAV 4 na cresta(Namba zimehifadhiwa) na wasichana wawili (Changudoa) waliokuwa wakimsaka mtoto wao waliyedai alichukuliwa na babake bila ya ridhaa yao.Ndipo katika majibishano ya mdomo askari huyo alichomoa bastola na kumuua fundi magari huyo ambaye alikuwa hahusiki na ugomvi huo.Cha kushangaza na kukatisha tamaa ni jinsi polisi walivyolichukulia kwa urahisi jambo hilo kiasi ya kwamba Muuaaji hakufanyiwa gwaride la utambulisho wala kutoa maelezo kituoni.
Askari Muuaji Constable Cricipin huyu hapa (Angalia attachment):mad2:

mkuu una uhakika na maelezo yako au umesoma sehemu?, maana ni hatari sana kuweka picha ya huyo askari kwenye public na hasa ikizingatiwa kuwa hiyo issue inahusiana na mambo ya utekeji na vitu kama hiyo, please hebu fatilia kwa kina na lete habari ambayo haiko biased kwa kiasi hicho, maana kuna watu ambao umewaita Machangudoa sasa sijuhi una uhakioka au ni basi tu,
tuwe makini jamani
 
Hii ni ishu sensitive inahitaji umakini kwenye kuijadili, kesi ya kuua si mzaha mzaha inabidi zipatikane data safi zisizo na chembe ya kuhisi.Nashauri mjadala wa hii ishu uahirishwe mpaka uchunguzi wa kina utakapofanyika na kupata real source ya mauaji haya, bado sakata hili ni hear say hakuna uhakika wa jambo hili.
 
duh nimeogopa nilivyoiona hio picha nikajua ndiye yeye aliyeuwawa.....
 
mmmh .....hapa mara tuambiwe wamemuuwa mtu asiye na hatia mara wamemuuwa mtekaji! jamani tunaomba maelezo ya kueleweka kabla hatujatakiwa kutoa hukumu kwa kesi ambayo iko mahakamani ( i suppose)
 
Mtoa mada hajaibalance taarifa yake na hata kama anachoeleza ni kweli kilitokea hivyo bado maelezo zaidi yanahitajika maana kwa ulivyoelezea ni kama vile una chuki au maslahi katika upande mmoja.
 
police gani anayefyatua risasi hovyo kwa mtu asiye na silaha??? shida ya police wetu hawana mazoezi, hawana nguvu; wengi ni walevi - kama ni defence si angetumia mbinu nyingine??? Kumwaga damu ya mtu ni kitu kibaya sana - amemhukumu mtu kifo - kabla hajahukumiwa kisheria - kama alikuwa mhalifu au la?

Issue ni kwamba "UKIMWAGA DAMU YA MTU INABIDI YA KWAKO IMWAGWE PIA - la sio maisha yako yatakuwa ya KUWEWESEKA - its so disgusting!!!!!
 
Ni jambo la kushangaza sana kwamba habari za matukio ya aina hii zimekuwa kama wimbo mwororo katika masikio ya wananchi wa Tanzania, hadi lini tutaendelea kusikia visa hivi vya kusikitisha vinavyofanywa na watu tuliowapa dhamana ya kuhakikisha usalama wetu, huku tukiwalipa kwa kodi zetu, ni lini mwisho wa kusikia hizi cold blood killings.,viongozi wa jeshi la polisi hajagundua tu kuwa ongezeko la matukio haya ni ishara kuwa kuna tatizo kubwa sana ndani ya jeshi hilo?.,yawezekana kwamba si polisi wote lakini miongoni mwao wapo ambao hawakustahili kuwa polisi.,hebu kina Said Mwema wafunguke macho jamani, kulea uovu ndani ya chombo nyeti kama hicho kuna siku yatatokea makubwa zaidi, ni bora kuziba ufa ili baadae usijejikuta unajenga ukuta mzima.
 
Raia wengi wamekwishauliwa na Polisi katika mazingira yasiyoelezeka,Ambapo ni polisi wachache sana waliwahi kuhukumia kwa mauaji ya raia kiholela.Ni wakati muafaka sasa vyombo vya ulinzi na usalama kujua kuwa dhamira ya serikali siyo wawauwe wananchi ,Kwani hata mhalifu ana haki ya kuishi.
 
Mimi napata kigugumizi cha kuchangia maana hoja yenyewe imejichanganya...habari tunazopata ni mkanganyiko..ila kama ni kweliaskari atakuwa ameuwa kimakosa then tunakoenda si kuzuri!
 
hehehe
tunahitaji chama mbadala kitakachosimamia uadilifu wa utendaji wa dola nzima.
Kama kiongozi wa juu ana maamuzi ya hovyo usitarajie kwa mtendaji wa chini kutenda kwa busara.
Matokeo ndo hayo na hakuna hatua intakayochukuliwa gadem
 
Back
Top Bottom