Polisi Dar wamvamia Mbowe usiku wa manane

Polisi Dar wamvamia Mbowe usiku wa manane

Uvamizi mi neno linalotumiwa vibaya na baadhi y wanasiasa uchwarakwa malengo ya FITINA. uvamizi ni lugha inayotumika kuelezea hujuma inafanywa na Jambazi au kikundi chenye lengo la kupora mali ya mtu/Watu. Polisi ni chombo kilicho anzishwa kwa misingi ya kisheria na kina mamlaka ya kukamata, kuhoji, kukagua mtu yeyote anayetiliwa shaka kwa uharifu.

Kuita utekelezaji wa Kazi za kipolisi ni uvamizi huo ni upotoshaji wenye lengo la Kufitini ili kuonewa huruma. inasikitisha chombo cha habari makini kama Mwananchi kinapokubali kupotoshwa na kuripoti habarikwa kutumia Lugha za wanasiasa.

.....Basi tuite 'ambush in the night'......ingawa hii hata Bob Marley aliilalamikia !
 
Vamia ni kitendo cha kuingia sehemu bila taarifa au bila kuomba na kukubaliwa ombilako
 
Unyanyasaji huu utafika kikomo tu na haki itapatikana


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Huyu kinyago aliyetoa maelekezo kuwa polisi wafanye watakavyo anailetea nch matatizo.akili yake mbaya kama sura yake
 
Uvamizi mi neno linalotumiwa vibaya na baadhi y wanasiasa uchwarakwa malengo ya FITINA. uvamizi ni lugha inayotumika kuelezea hujuma inafanywa na Jambazi au kikundi chenye lengo la kupora mali ya mtu/Watu. Polisi ni chombo kilicho anzishwa kwa misingi ya kisheria na kina mamlaka ya kukamata, kuhoji, kukagua mtu yeyote anayetiliwa shaka kwa uharifu.

Kuita utekelezaji wa Kazi za kipolisi ni uvamizi huo ni upotoshaji wenye lengo la Kufitini ili kuonewa huruma. inasikitisha chombo cha habari makini kama Mwananchi kinapokubali kupotoshwa na kuripoti habarikwa kutumia Lugha za wanasiasa.

Kiongozi!

Kama wakuu (OCD/RPC) wao wamekana kujua/kutuma askari wao kwenda kumkamata Mh. Mbowe nyumbani kwake usiku wa manane, huo tuuite nini kama sio UVAMIZI?
 
Ata sielewi wapi watanzania tunaelekea chombo kama hiki kila kukicha kinapata tuhuma je sisi walalahoi tunaoishi chini ya dola moja kwa siku nani atatutetea kama wanasiasa wenye majina wanatafutwa usiku na mchana, Ee mungu tuepushe na aya mambo awa wa roho wamadalaka watatuua
 
KUNDI la polisi wenye silaha za moto jana usiku walivamia nyumbani kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, kwa nia ya kumkamata.

Askari hao wanaokisiwa kufikia saba, wakiwa na silaha nzito katika gari la wazi waliwasili nyumbani kwa Mbowe majira ya saa saba na nusu usiku na kuwaamuru askari wanaolinda nyumbani kwake kumtoa Mbowe nje ili waonane naye.

Walinzi wa Mbowe walihoji uhalali wa ukamataji huo na kuwataka polisi wawaoneshe hati ya kumkamata, lakini hawakuweza kuionesha, hali iliyozusha wasiwasi kwa walinzi wa kiongozi huyo.

Hata hivyo walinzi hao waliwaambia polisi hao kuwa Mbowe ambaye pia ni kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni alikuwa safarini, jibu ambalo lilipokewa kwa shingo upande na askari hao.

Polisi hao baada ya kuona wameshindwa kukamilisha kazi hiyo, waliwaachia walinzi hao namba ya simu 0754-085600 ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Ernest Kimola, wakiwaagiza kuhakikisha wanamwambia Mbowe awasiliane na kamanda huyo.

RCO amsukumia RPC, akana
Hata hivyo, alipohojiwa na Tanzania Daima Jumapili kwa njia ya simu, Mkuu wa Upelelezi Kimola aligoma kuzunguzia suala hilo na kumtaka mwandishi kuwasiliana na mkuu wake wa kazi, ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamilius Wambura, akidai ndiye mwenye haki ya kutoa ufafanuzi wa jambo hilo.

“Unajua mimi si msemaji wa polisi, wasiliana na kamanda wa mkoa, maana ndiye mwenye uwezo wa kutoa maelezo,” alisema Kimola na kukata simu. Lakini alipopigiwa simu Kamanda Wambura aliruka kimanga, kwa mshangao, akidai kutojua lolote kuhusiana na polisi kuvamia nyumbani kwa Mbowe.
“Kwa kweli ndiyo napata taarifa hizo kutoka kwako, kuwa kiongozi huyo alifuatwa na polisi, maana silijui suala hilo hata kidogo,” alisema Wambura, naye kama alivyofanya Kimola akakata simu.

Kauli ya CHADEMA
Lakini wakati Kimola akikataa kusema chochote, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema kuwa alizungumza kwa njia ya simu na Kimola kuhusiana na kitendo cha polisi kuvamia nyumbani kwa kiongozi huyo wa juu wa kisiasa, na kudai kupewa majibu ya kushangaza.

Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika Manzese, Wilaya ya Kinondoni, Dk. Slaa alisema Kimola alijitetea akidai kwanza kukana kufika nyumbani kwa Mbowe usiku wa manane. Pili, alisema kuwa hawakwenda kumkamata Mbowe, isipokuwa kufanya naye mazungumzo na kisha wangemwacha.

Slaa alisema kitendo hicho kimewashitua na ni cha kinyama na kilichokiuka sheria za nchi na haki za binadamu. Aliongeza kwamba, daima wamekuwa wakilishutumu Jeshi la Polisi kwa kutumika vibaya kukandamiza wapinzani, lakini mara zote CHADEMA kimepuuzwa na sasa jeshi hilo limeamua kuvamia makazi ya viongozi wa kisiasa kwa madhumuni yasiyoeleweka.

Alisema haijulikani nini kingetokea ikiwa Mbowe angekuwa ndani, ikiwa walinzi wangeamua kugoma kumwachia kiongozi wao. “Tuna hofu kubwa na usalama wetu, maana pale wangeweza kufanya lolote, hata kumuua na kisha kutoa matamshi kuwa walikuwa wanajibishana kwa risasi, kama ambavyo imekuwa jadi ya askari polisi kutoa taarifa za uongo na upotoshaji wanapoua watu,” alisema Slaa.

Alisema ikiwa polisi walikuwa na shida ya kweli, wangemwita kwa njia sahihi na si kumvamia na kuingilia uhuru wake na wa familia yake kama wanakamata gaidi ama jambazi hatari.

Dk. Slaa alisema Mbowe anayo ofisi inayojulikana, na kama kweli hakukuwa na jambo baya lililopangwa na polisi hao wasingeweza kufanya uhuni kama walioufanya.

“Kama wanaweza kuvamia nyumbani kwa kiongozi mkubwa kama Mbowe wakiwa na silaha nzito, itakuwaje kwa viongozi wa kawaida na raia?” alihoji Slaa.

Kutokana na tukio hilo la kuogofya, CHADEMA imemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwaeleza Watanzania maana ya matukio haya ambayo yamedhamiria kuleta vurugu kubwa nchini. Kadhalika, wamemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, kuueleza umma kile kilichokusudiwa na askari wake kuvamia nyumbani kwa Mbowe mithiri ya jambazi.

Itakumbukwa pia kuwa hivi karibuni askari polisi wa Mkoa wa Arusha walivamia nyumbani kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakiwa na silaha nzito na mbwa, na kumkamata, kisha kumtupa rumande kwa siku nzima.

===================================
My Take
Polisi , Hata kama Mmekubali kutumika Kuidhhofisha CHADEMA, basi jaribuni hata Kutumia Njia za Kisasa Jaman
===================================

chagonja hata zero draft hajatoa anaweweseka na ushahidi dvr
 
Huu ukarumekenge wa Said Mwema kuwatumia polisi kulinda himaya yake ya Kifisadi na akina Ridhiwani kwa gharama yoyote italiingiza taifa katika machafuko makubwa. Polisi kwa sasa hawaheshimiki kabisa kwa kuwa wanatuniwa kama condom kwa maslahi binafsi na ya kusiasa.

Shime vijana wa kitanzania, unyanyasaji huu uwe ni HAMASA kwetu kujiunga na Red Brigade maana hawa tuliowapa kazi ya kutulinda wanalinda maslahi ya mafisadi wachache kwa gharama ya damu ya watanzania
 
Ngoja nikanunue AR zangu mbili na magazine 20 siku nikirudi Bongo wimbo wowote wa polisi na mimi naimba

Hahahaha huko zinapatikana kirahisi eh. Sijui nikutumie some dollars unifanyie mpango na mimi maana tunapoelekea kila mtu atatakiwa ajilinde mwenyew
 
Wanasiasa kwa media coverage si haba. Ili mradi wawe na kitu cha kurubuni wafuasi wao, mbona ashakamatwa mara nyingi tu na mtu wenyewe mwepesi. Ila shongondo nyingi tu

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Kabla hatujaenda mbali inabidi utuambie shongondo ni kitu gani na ni lugha gani hiyo. Sio mnajifanya kunena kwa lugha zenu huku mkitukana watu.

Cc Moderator: - Kwa taarifa.
 
Last edited by a moderator:
Tunapungukiwa strategies za kiintelijensia kama nchi, na yaonyesha vyombo vya dola haviwasiliani ipasavyo kitu ambacho ni hatari sana.

Ni vema pia ingebainika the root cause ya kuhitaji kumkamata Mbowe akiwa ni raia mwema wa nchi hii.

nimejiuliza maswali mengi nimekosa majibu.wameacha namba za simu getini.....yaani wana sachi waranti na wameishia getini hawajaingia ndani?kwa nini waache namba za simu badala hata ya kuingia ndani na kuacha ujumbe kuwa mh akirudi mjulisheni kuwa anahitajika kituo cha polisi kwa mahojiano....polisi wa kutengeneza?wako anprofesheno kabisa!!!!
 
Tanzania siyo kama tuijuavyo.

Polisi wanaenda kumkamata mtuhumiwa, wanafika getini, wanakuta walinzi, walinzi wanawaambia Mh. Mbowe hayupo. Wanaamini maneno ya walinzi na kuacha namba ya simu ili akirudi awapigie simu. Just like that?.

Maswali la msingi:
Kama walifahamu mawasiliano ya simu ni njia mbadala ya kumpata Mh. Mbowe, kwa nini hawakumpigia simu kabla ya kwenda nyumbani kwake?.

Kama walikuwa na nia ya kumkamata, kwa nini waliishia getini badala ya kuingia ndani kama wafanyavyo na ikichukuliwa kuwa walikuwa wamejiandaa na siraha kama ilivyofanyika kwa polisi Arusha wakati wanamtafuta Mh. Lema?.

Kama walikuwa ni polisi, ni kwa nini viongozi wa polisi wanakanusha na kusema hivi,

Ina maana kuna vikundi/kikundi kinajifanya ni polisi kwa ajiri ya kufanya uhalifu kwa manufaa ya kisiasa?.

Kikubwa zaidi, matatizo haya yanatokea kwa sababu Tanzania kuna OMBWE la vyombo vya kuangalia usalama wa raia. Kunafikia hatua ambapo kwa sasa inakuwa ni vigumu kutofautisha kazi ya polisi na kazi ya watu wabaya wanaojifanya polisi.

Matukio kama haya yataendelea kutokea na yataongezeka zaidi kadri tunavyoelekea kwenye uchaguzi mkuu kama hakutafanyika UAMUZI mapema wa kuvisuka upya vyombo vya ulinzi nchini.

Is this happening because of Arusha local election?. Jibu wanalifahamu wale "polisi" walioenda "kumkamata" Mh. Mbowe.

Wanaoyafanya hayo ni polisi kweli na wanatumwa hasa na hao hao wanaokanusha,hawawez kukubali wakati wana malengo mabaya,kwan kwa Ulimboka na Kibanda ilikuaje?
 
Kabla hatujaenda mbali inabidi utuambie shongondo ni kitu gani na ni lugha gani hiyo. Sio mnajifanya kunena kwa lugha zenu huku mkitukana watu.

Cc Moderator: - Kwa taarifa.
Sasa shongondo ndo nin?kama huna la kuandika tuliza ujinga sio unaleta lugha za huko kwenu sitimbi
 
Last edited by a moderator:
Uvamizi mi neno linalotumiwa vibaya na baadhi y wanasiasa uchwarakwa malengo ya FITINA. uvamizi ni lugha inayotumika kuelezea hujuma inafanywa na Jambazi au kikundi chenye lengo la kupora mali ya mtu/Watu. Polisi ni chombo kilicho anzishwa kwa misingi ya kisheria na kina mamlaka ya kukamata, kuhoji, kukagua mtu yeyote anayetiliwa shaka kwa uharifu.

Kuita utekelezaji wa Kazi za kipolisi ni uvamizi huo ni upotoshaji wenye lengo la Kufitini ili kuonewa huruma. inasikitisha chombo cha habari makini kama Mwananchi kinapokubali kupotoshwa na kuripoti habarikwa kutumia Lugha za wanasiasa.

We anaandika vitu gani? Huyo aliyekuwa anaenda kukamatwa ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani,achilia mbali ya kuwa Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani. Huwezi kwenda kumkamata kibwegebwege kama unaenda kushika mwizi wa kuku.
 
Watakuwa walitaka kumn'goa meno na kucha
 
Mie nasema kweli hapa, watu hao walishakuja kumsachi Bosi wetu ila SIO Usiku ilikuwa mchana. Wana Silaha Na pick up, wakasema Kwa walinzi kwamba tumekuja kumsach Mtu huyu sisi ni polisi Na vitambulisho wakatoa. Kisha wakaingia Ndani wakasach pote Na Watoto walikuwepo. Walinzi wakachukua namba Za gari, kisha wakaitisha cm zote "za gharama" wakasema wanazipeleka kituoni Na laptop mbili.

Walipoondoka bosi wetu kumbe alikuwa nje akawaona Na kunote namba Za gari. Cha kushangaza wakamwachia mlinzi namba ya cm awapigie Bosi akija. Wakaondoka. Nilipopigiwa cm nilitua hapo faster, tukaenda kituo Cha polisi Cha karibu wakasema namba hizo hawazitambui Wala watu hao, tukatumia njia zetu kupata call history ya namba hiyo Na tukafanikiwa, Cha kushangaza inaonekana ni ya Mtu iliyosajiliwa Dodoma, Na Mara nyingi imempigia IGP Mwema. Tukaenda hadi oysterbay Kwa kamanda Kanyela that time akiwa RPC wa Kinondoni, tukakaa nae ofisini Na kumpa vielekezo vyote Kwa Muda sana. Akasema atalishughulikia. Kama kawaida Nchi HII kukosa uwajibikaji kukawa kimya.

Baadae tukasikia walimvamia Mtu mwingine maarufu hotelini ili wamkamate, walinzi wa hoteli wakamficha Na kusema katoka kisha wakawaachia walinzi namba hiyo hiyo. Ukiipiga inaita sana Na kukatika yenyewe.

Kwa upande wetu tuna Hoja 3

1:- AMA mabosi wakubwa Wa Polisi wameunda within respond unit kikosi kingine Cha siri Cha kufanya Kazi zao!! Lakini hoja HII hatuikubali sana Kwa Sababu wasingekuwa wajinga kuacha namba ya cm ambayo mkuu Wa polisi inamwonyesha kwamba naye ni mpiga au mpigiwa.

2:- Ni kikosi Cha ex-polisi wanaofanya uhalifu au ni majambazi yanayojifanya polisi. Hoja hii inaweza kuwa Na nguvu lakini Bado maswali yapo mengi. Ni kweli wanaonyesha vitambulisho vya polisi but hiyo siyo hoja sana siku hizi Mtu anajitengenezea Chochote. Kama ni wahalifu kwanini waache namba Za Cm!?, Na Kama ni majambazi, mzigo wote wa Silaha Na gari Na usumbufu wote ni kwa ajili ya kupora cm Na laptop?!????? Haingii akilini. Na kwanini wafuate watu maarufu wasio Na fedha wakiwaacha matajiri ambao huko wangetoka Na vitita vya fedha. Ni watu wengi maarufu wanetendewa mcheZo huu but Kwa kuwa hawakumdhuru Mtu wala kuiba kitu Chenye samani kubwa wanaamua kuripoti polisi Na kuwa kimya kutoyakuza mambo.

3:- HII ya tatu yaweza kuwa Na nguvu zaidi, yawezekana ndani ya polisi hiyo hiyo wameshaanza kupakana matope au kumpaka matope Mkubwa wao. Inawezekana hao jamaa ni polisi kweli tena Wa quick respond unit (TiGO) , Kama watano hivi but kiongozi wao ndio anaujua mcheZo wengine ni wa kuambiwa tu twende hapa wanaenda. Naamini hivi Kwa Sababu wakifika sehemu wanapack kabisa Na hukaa zaidi ya nusu saa Na hawakurupuki Wala kuonyesha kwamba wana haraka. Wangekuwa Wezi mambo Yao ni faster faster. Wana uhakika Hata mkiita polisi watawakuta wenzao Na watajua wako kazini. Hiyo namba ya cm wanayoacha ndio hasa lengo Lao, wanajua mtaenda polisi Na kuchukua kibali Cha kupatiwa call history Na kugundua he mbona Mzee naye yumo Kwenye list. I think ndio lengo Lao, Na wala SIO namba ya cm ya yeyote within that group.

That's why wameemvamia Chair wa CDM, wakijua jamaa atatambaa na hiyo namba sana Na kuamsha ugomvi Na Mzee Mwema.

Mimi nadhani tabia HII ya polisi kuacha uwajibikaji itagharimu sana ustaarabu Na Amani yetu. Kama tokea that time tumeripoti tukio hili oysterbay wangemtaarifu Mwema hopely hawa watu wangesakwa Na kupatikana. Au Na polisi wanataka tuamini Mwema naye ni miongoni mwa wanaotafuta watu Na kuwaibia cm au laptop?,!?.

Tanzania Ina kiongozi mmoja tu -------- anayetengeneza dili Za kigaidi Kwa kutuma facilitations kwa M-PESA via simu yake halali, sidhani Kama kuna rekodi ya upumbavu mwingine kiasi hiki Tanzania. So hao respond unit AMA ya kweli au kichina wasirichoree Picha Lao la kichina kutuingiza mkenge tusearch users wa hiyo namba. Sijui Kwa Nini polisi Nchi HII imegoma Kufanya Kazi, ukiwaambia fanyeni Kazi wanakusaka wewe uliyewakumbusha wajibu wao, Na kuishia kukamata chokoraa, watu wasio Na Kazi Na kusubiria asubuhi ndugu Na jamaa waje kituoni kuwatoa jamaa zao Kwa kulipia 50,000 hadi laki. Nchi HII ..!?
 
Mbowe ni mharifu lazima awajibike kwa uharifu wake asifikiri kila kitu ni kirahisi tu anatoa matamko ya hovyo bila hata ya kujua madhara yake.

Bei ya Pedi nasikia imepanda.
Vp ;Buku Saba inakutosha kweli...
 
Back
Top Bottom