Polisi Dar wamvamia Mbowe usiku wa manane

Polisi Dar wamvamia Mbowe usiku wa manane

Bramo

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2009
Posts
13,242
Reaction score
10,227
KUNDI la polisi wenye silaha za moto jana usiku walivamia nyumbani kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, kwa nia ya kumkamata.

Askari hao wanaokisiwa kufikia saba, wakiwa na silaha nzito katika gari la wazi waliwasili nyumbani kwa Mbowe majira ya saa saba na nusu usiku na kuwaamuru askari wanaolinda nyumbani kwake kumtoa Mbowe nje ili waonane naye.

Walinzi wa Mbowe walihoji uhalali wa ukamataji huo na kuwataka polisi wawaoneshe hati ya kumkamata, lakini hawakuweza kuionesha, hali iliyozusha wasiwasi kwa walinzi wa kiongozi huyo.

Hata hivyo walinzi hao waliwaambia polisi hao kuwa Mbowe ambaye pia ni kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni alikuwa safarini, jibu ambalo lilipokewa kwa shingo upande na askari hao.

Polisi hao baada ya kuona wameshindwa kukamilisha kazi hiyo, waliwaachia walinzi hao namba ya simu 0754-085600 ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Ernest Kimola, wakiwaagiza kuhakikisha wanamwambia Mbowe awasiliane na kamanda huyo.

RCO amsukumia RPC, akana
Hata hivyo, alipohojiwa na Tanzania Daima Jumapili kwa njia ya simu, Mkuu wa Upelelezi Kimola aligoma kuzunguzia suala hilo na kumtaka mwandishi kuwasiliana na mkuu wake wa kazi, ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamilius Wambura, akidai ndiye mwenye haki ya kutoa ufafanuzi wa jambo hilo.

"Unajua mimi si msemaji wa polisi, wasiliana na kamanda wa mkoa, maana ndiye mwenye uwezo wa kutoa maelezo," alisema Kimola na kukata simu. Lakini alipopigiwa simu Kamanda Wambura aliruka kimanga, kwa mshangao, akidai kutojua lolote kuhusiana na polisi kuvamia nyumbani kwa Mbowe.
"Kwa kweli ndiyo napata taarifa hizo kutoka kwako, kuwa kiongozi huyo alifuatwa na polisi, maana silijui suala hilo hata kidogo," alisema Wambura, naye kama alivyofanya Kimola akakata simu.

Kauli ya CHADEMA
Lakini wakati Kimola akikataa kusema chochote, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema kuwa alizungumza kwa njia ya simu na Kimola kuhusiana na kitendo cha polisi kuvamia nyumbani kwa kiongozi huyo wa juu wa kisiasa, na kudai kupewa majibu ya kushangaza.

Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika Manzese, Wilaya ya Kinondoni, Dk. Slaa alisema Kimola alijitetea akidai kwanza kukana kufika nyumbani kwa Mbowe usiku wa manane. Pili, alisema kuwa hawakwenda kumkamata Mbowe, isipokuwa kufanya naye mazungumzo na kisha wangemwacha.

Slaa alisema kitendo hicho kimewashitua na ni cha kinyama na kilichokiuka sheria za nchi na haki za binadamu. Aliongeza kwamba, daima wamekuwa wakilishutumu Jeshi la Polisi kwa kutumika vibaya kukandamiza wapinzani, lakini mara zote CHADEMA kimepuuzwa na sasa jeshi hilo limeamua kuvamia makazi ya viongozi wa kisiasa kwa madhumuni yasiyoeleweka.

Alisema haijulikani nini kingetokea ikiwa Mbowe angekuwa ndani, ikiwa walinzi wangeamua kugoma kumwachia kiongozi wao. "Tuna hofu kubwa na usalama wetu, maana pale wangeweza kufanya lolote, hata kumuua na kisha kutoa matamshi kuwa walikuwa wanajibishana kwa risasi, kama ambavyo imekuwa jadi ya askari polisi kutoa taarifa za uongo na upotoshaji wanapoua watu," alisema Slaa.

Alisema ikiwa polisi walikuwa na shida ya kweli, wangemwita kwa njia sahihi na si kumvamia na kuingilia uhuru wake na wa familia yake kama wanakamata gaidi ama jambazi hatari.

Dk. Slaa alisema Mbowe anayo ofisi inayojulikana, na kama kweli hakukuwa na jambo baya lililopangwa na polisi hao wasingeweza kufanya uhuni kama walioufanya.

"Kama wanaweza kuvamia nyumbani kwa kiongozi mkubwa kama Mbowe wakiwa na silaha nzito, itakuwaje kwa viongozi wa kawaida na raia?" alihoji Slaa.

Kutokana na tukio hilo la kuogofya, CHADEMA imemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwaeleza Watanzania maana ya matukio haya ambayo yamedhamiria kuleta vurugu kubwa nchini. Kadhalika, wamemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, kuueleza umma kile kilichokusudiwa na askari wake kuvamia nyumbani kwa Mbowe mithiri ya jambazi.

Itakumbukwa pia kuwa hivi karibuni askari polisi wa Mkoa wa Arusha walivamia nyumbani kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakiwa na silaha nzito na mbwa, na kumkamata, kisha kumtupa rumande kwa siku nzima.

===================================
My Take
Polisi , Hata kama Mmekubali kutumika Kuidhhofisha CHADEMA, basi jaribuni hata Kutumia Njia za Kisasa Jaman
===================================
 
Polisi ndio wanaiharibu hii nchi.
Bila juhudi za makusudi Polisi wanafanya siasa za hatari za kuvuruga nchi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwakweli matendo ya aina hii hayafai, yatasababisha uvunjifu wa amani. Mi naamini kama Mbowe anatakiwa, aitwe kwa taratibu zilizowekwa!

Yeye si gaidi wala jambazi. Anastahili heshima yake. Lakini pia matendo kama haya yakiendelea, tunu ya amani yetu itapotea.

Kwa sasa TZ inao maadui wengi, naomba tuwe makini na matendo ya kutugawa, tusimpe adui fursa ya kupenyeza mamluki kirahisi!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Polisi wana haki ya kumkamata mtu muda wowote wanaopenda.

Ni kweli, lakini kuna sheria wanazopaswa kuzifuata. wanaruhusiwa kumkamata muarifu wakati wowote! Lakini mbona RCO na RPC wanazunguka? Huoni kuna mchezo mchafu hapo?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Tanzania Daima ni gazeti la propaganda na kumsifia Mbowe na CHADEMA
 
Unaeleza mazoea siyo haki.

Pia polisi hawamkamati mtu kwa kupenda wao kama polisi bali kwa kufuata sheria za nchi.
Tumezoezwa kukamatwa na kuwekwa ndano hovyohovyo mpaka tunadhani ukiukwaji huo wa sheria ni utendaji kazi wa kisheria wa polisi.

Matongotongo ya kulala kwa miaka 50 yatatutoka lini?????!!!
Polisi wana haki ya kumkamata mtu muda wowote wanaopenda.
 
Mkuu Polisi wanatumika tu kutekeleza matukio ya wakubwa zao, pamoja na hayo wao pia wanastahili lawama. Haya yote yanayoendelea DHAIFU atakuwa anayafahamu hivyo yeye ndio anastahili lawama nyingi zaidi. Nchi iko katika njia panda bila hekima na busara za hali ya juu inaweza kutumbukia kwenye machafuko ya kutisha.

Polisi ndio wanaiharibu hii nchi.
Bila juhudi za makusudi Polisi wanafanya siasa za hatari za kuvuruga nchi.
 
Polisi wana haki ya kumkamata mtu muda wowote wanaopenda.

we 'mshindo' mbona hawajamkamata wala kuzuia madawa ya kulevya yanayopita uwanja wa ndege kila kukcha hebu utueleze maana ya kuweka ile VIP mlilenga nini na kama si kupitisha madawa ya kulevya kwa urahisi?
 
Radhia...nenda kasome kitabu cha civics form two...ukimaliza am sure utakuja kufuta ur comment...
 
Ee! Hii ni hatari. Labda walitaka uchaguzi AR usitishwe kwa kuwa CDM wangefanya fujo bila shaka. Mambo ya namna hii yanafanya majeshi yetu kuchukiwa na wananchi.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Acha polisi wafanye kazi,kwani yeye ni nani asikamatwe na polisi.
 
Mbowe ni muhalifu ndiyo
Mhalifu amefanya nini? Hizi siasa za kufuata mkumboa zitawacost siku moja...Ujue janga lolote likitokea litakukumba na wewe. Tumia akili na maarifa kuliko kutumia hisia.
 
Back
Top Bottom