Tanzania siyo kama tuijuavyo.
Polisi wanaenda kumkamata mtuhumiwa, wanafika getini, wanakuta walinzi, walinzi wanawaambia Mh. Mbowe hayupo. Wanaamini maneno ya walinzi na kuacha namba ya simu ili akirudi awapigie simu. Just like that?.
Maswali la msingi:
Kama walifahamu mawasiliano ya simu ni njia mbadala ya kumpata Mh. Mbowe, kwa nini hawakumpigia simu kabla ya kwenda nyumbani kwake?.
Kama walikuwa na nia ya kumkamata, kwa nini waliishia getini badala ya kuingia ndani kama wafanyavyo na ikichukuliwa kuwa walikuwa wamejiandaa na siraha kama ilivyofanyika kwa polisi Arusha wakati wanamtafuta Mh. Lema?.
Kama walikuwa ni polisi, ni kwa nini viongozi wa polisi wanakanusha na kusema hivi,
Ina maana kuna vikundi/kikundi kinajifanya ni polisi kwa ajiri ya kufanya uhalifu kwa manufaa ya kisiasa?.
Kikubwa zaidi, matatizo haya yanatokea kwa sababu Tanzania kuna OMBWE la vyombo vya kuangalia usalama wa raia. Kunafikia hatua ambapo kwa sasa inakuwa ni vigumu kutofautisha kazi ya polisi na kazi ya watu wabaya wanaojifanya polisi.
Matukio kama haya yataendelea kutokea na yataongezeka zaidi kadri tunavyoelekea kwenye uchaguzi mkuu kama hakutafanyika UAMUZI mapema wa kuvisuka upya vyombo vya ulinzi nchini.
Is this happening because of Arusha local election?. Jibu wanalifahamu wale "polisi" walioenda "kumkamata" Mh. Mbowe.