Mwanamasumbwi kutoka America Joe Louis Barrow aliwahi kusema "Everybody wants to go to heaven but no one wants to die", hata hivyo mwanalege kutoka nchini Jamaica Peter Tosh alisema 'everyone speaks of peace, no one speaks of rights". Kwenye kila Jema unalopambana kubali maumivu, kuvuliwa uanachama ni bora zaidi kuliko kuwa mtumwa wa kisiasa kuwapigia magoti watawala. Mimi binafsi hata ukiweka bunduki kifuani siwezi badili msimamo wangu mpaka haki kwa kila raia itakapopatina ikiwemo uhuru wa maoni na kuruhusu mitazamo tofauti na ya watawala.