Polepole usingekubali kuachia ubunge, Rais hana mamlaka ya kukung'oa

Polepole usingekubali kuachia ubunge, Rais hana mamlaka ya kukung'oa

pole pole alikua mbunge wa kuteuliwa, aliyemteau amemtumbua, simple mathematics kabisa.
 
Asingekubali ili awe adui wa mfumo uliopo madarakani aishi kwa mashaka ili wewe umuite shujaa mwenye msimamo huku JF.
Huwa nikiona mtu ana underestimate mamlaka ya raisi wa Jamhuri namuona kama mtu asiyeijua hii nchi. Raisi kama hakutaki mfumo utatafuta namna ya kukulazimisha utoke na utatoka hata uwe na mizizi migumu kama spika, cag n.k
 
Maana yake umeshaambiea huna lako hapo,unatakiwa utoke,huyo polepole hawezi kushindana na Rais,ni nyenyere tu,pia ametegwa hapo,malawi wanakuja kuomba vibarua huku,akatae akae nje.
 
Asingekubali ili awe adui wa mfumo uliopo madarakani aishi kwa mashaka ili wewe umuite shujaa mwenye msimamo huku JF.
Huwa nikiona mtu ana underestimate mamlaka ya raisi wa Jamhuri namuona kama mtu asiyeijua hii nchi. Raisi kama hakutaki mfumo utatafuta namna ya kukulazimisha utoke na utatoka hata uwe na mizizi migumu kama spika, cag n.k
..Kifupi usijaribu kudhalilisha mamlaka na madaraka ya RAIS hata siku moja
 
Kwanza nikurekebishe kuwa Vuai Nahodha hajateuliwa kuziba nafasi ya Polepole kwakuwa mpaka sasa wabunge wa kuteuliwa wapo Tisa tu ikiwemo huyu Vuai, hvyo bado kuna nafasi moja kukamilisha idadi ya nafasi KUMI

Pili,
licha ya kwamba Rais hana mamlaka ya kutengua uteuzi wa mbunge yoyote au mteule yoyote aliye ktk muhimili mwngne kama Jaji nk lakn Rais kwa nguvu na mamlaka makubwa aliyonayo basi Polepole angekutana na force plus pressure kubwa sana kuanzia ndani ya bunge, chamani mpaka mtaani ambapo ingemlazimu tu ajiuuzulu ubunge wake kwasbb kitendo cha kukataa uteuzi wa Rais kisa eti ung'ang'anie ubunge ingekuwa umeifedhehesha mamlaka ya Rais

Rais hana mamlaka ya kumtengua Spika wa bunge, ila ile kauli ya Rais dhidi ya Ndugai ilipelekea bwana huyu kukutana na presha kubwa kutoka kwa wabunge mbalimbali na wanachama wa CCM mpaka akaamua kung'atuka kwa hiari yake mwenyewe

Nampongeza tu Mh Polepole kwa kutumia hekma na busara ktk kutafakari mambo vngnevyo angejitia kichwa ngumu basi moto ambao angekumbana nao angehama hii nchi

Nguvu na Mamlaka aliyonayo Rais ktk nchi zetu hizi za Kiafrika ni kubwa sana
Bobi wine mwenyekiti wa Chama cha National Unity Platform aliwahi kusema "if you are right better stand alone", hata ukitengwa na jamii nzima mpaka ulimwengu ni hafadhari zaidi kuliko kupata tabasamu mbele ya waovu. Naomba ikumbukwe kuwa kijana mkosoaji mkubwa nchini Liberia [emoji1148] Ton Tobias mwenye umri wa miaka 17 aliwahi kupata teuzi na Charles Taylor lakini akasema ni bora kuwa masikini sehemu salama kuliko Tajiri sehemu hatari. Kitendo cha polepole kukubali kuwa balozi na kukosa malupulupu ya ubunge ni kukosa akili

Naomba ujue kuwa uongozi sio Ajira ni huduma, Sasa ngozi nyeusi ikipata uongozi inaona ni sehemu ya kutengeneza pesa, na hapa ndipo tunapojikwaa.
 
Rais hana mamlaka ya kumvua mwanaccm uanachama, wenye mamlaka ni halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi Taifa

Bosi wa hiyo halmashauri kuu ya taifa ni nani?

Mwenyekiti wa ccm ana nguvu kubwa sana katika katiba ya ccm. Nenda kaisome
 
Ila watanzania sijui lini akili zitawakaa vizuri ili wawe na uwezo wa kutofautisha hulka za wanasiasa wenye misimamo ya kweli na wale wenye misimamo ya uwongo uwongo. Hivi kweli kuna mtu na akili zake kabisa alikuwa anakaa anaamini kuwa Pole Pole ana msimamo? Yaani kule kubwabwaja sijui shule ya uongozi, sijui tusichanje, sijui tuendelee kujifukiza, sijui COVI 19 haipo na kuita wenzake wahuni basi eti mtu ana msimamo. Na wengine wakaja hapa kwa mbwembwe eti hatakubali kuapishwa. Siku zote nasema usiwaamini wanasiasa kwani wengi wao wanchozungumza mara zote sicho wanachomaanisha. N mara nyingine hata wanachotuhubiria majukwaani hata wao wenyewe hawakiamini na hawakikubali.

Huyo jamaa juzi tu hapa hata miaka mingi haijapita yeye na Kabudi walikuwa na msimamo juu ya katiba ya Warioba lakini baada ya yeye tu kuteuliwa na hayati Magufuli na kupewa ukuu wa wilaya na baadaye katibu uenezi wa chama tawala basi misimamo yake juu ya katiba ya Warioba ikawa kwishney. Tokea hapo wenye akili walishajua hamna mwanasiasa mwenye msimamo hapo bali mchumia tumbo tu kama wengine.

Kwa vyovyote iwavyo Pole Pole alikuwa na machaguo mawili tu ama achague kukubali uteuzi wa ubalozi na kwenda Malawi au aachane na siasa kabisa arudi kwenye NGO yake. isingewezekana kabisa eti akatae ubalozi halafu ang'angánie ubunge wakati juzi tu spika Ndugai katemeshwa uspika wake. Na hapa Pole Pole alikuwa kwenye mtego mkubwa kwani ni lazima watu walisha mfanyia "homework" na kujua madahaifu yake na atanasa vipi. Na kweli jamaa kashanasa basi aende zake Malawi na zile kelele zake sijui shule ya uongozi kwisha habari yake kama yule mwenzake wa Kawe aliyekuwa na kelele za tunachanja au hatuchanji.
 
Binafsi nimekuja kujua ndani ya nchi yetu wenye misimamo isiyoteteleka hakuna labda wamejificha. Kitendo cha aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa mh. Polepole kukubali kuwa balozi na kuacha nafasi yenye malupulupu ya kutosha ni kuendekeza uoga na kutawaza matako ya watawala.

Binafsi mheshimiwa Polepole hakutakiwa kukubali kuachia ngazi na asingetolewa ubunge kwa kuwa ukomo wa ubunge upo kikatiba hakuna mwenye mamlaka ya kumtoa unless akose sifa na vipengele vyote vya ukomo wa ubunge vimeorodheshwa kikatiba.

Cha ajabu nilichokuja kushangaa Rais kumteua Vuai Nahodha kuwa mbunge kabla ya Polepole kutoa taarifa either kakubali ubalozi au laa, je Polepole angekataa ubalozi Vuai Nahodha angekuwa Nani?.

Usishangae mlima Kilimanjaro kuhamia Dar es Salaam ila nitashangaa sana siku nikisikia CCM wamebalika kifikra.

Kuna wakati unadhani unaelewa kumbe huelewi. Kama kweli huyo Polepole ana nia ya kulifanyia kazi Taifa, hawezi kwa kukaa nje. Akiwa ndani na akafanya kazi yake kwa uadilifu hata kama atasulibishwa, atakuwa ametimiza wajibu Wake. Usitake polepole awe wewe.
 
Binafsi nimekuja kujua ndani ya nchi yetu wenye misimamo isiyoteteleka hakuna labda wamejificha. Kitendo cha aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa mh. Polepole kukubali kuwa balozi na kuacha nafasi yenye malupulupu ya kutosha ni kuendekeza uoga na kutawaza matako ya watawala.

Binafsi mheshimiwa Polepole hakutakiwa kukubali kuachia ngazi na asingetolewa ubunge kwa kuwa ukomo wa ubunge upo kikatiba hakuna mwenye mamlaka ya kumtoa unless akose sifa na vipengele vyote vya ukomo wa ubunge vimeorodheshwa kikatiba.

Cha ajabu nilichokuja kushangaa Rais kumteua Vuai Nahodha kuwa mbunge kabla ya Polepole kutoa taarifa either kakubali ubalozi au laa, je Polepole angekataa ubalozi Vuai Nahodha angekuwa Nani?.

Usishangae mlima Kilimanjaro kuhamia Dar es Salaam ila nitashangaa sana siku nikisikia CCM wamebalika kifikra.

Alikua mbunge wa Jimbo gani? We hujapiga hesabu ila mwenzako kapiga hesabu hauziki tena na hakutakua na uchaguzi kama ule wa kupeleka majina

Hivyo kanusuru tumbo lake kuendelea kula kidogo kidogo,kule alipo yeye hakuna competition ni kuomba Mungu tu asahaulike ili aendelee kula

Wewe umewaza masilahi mafupi ila mwenzako kawaza masilahi marefu,Ajira ngumu [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] shaur yako!!!!

Usione watu wanavaa suti tu wana yao moyoni
 
Sio kweli, kwani wamalawi wote kweli wamechanjwa? Wamalawi wote million 35???. Wote wamechanjwa kweli. Kama sio wote basi polepole anaweza asichanjwe pia.
Ubishi wa kijinga sana huo,kuna vitu ni ngumu kiongozi kuvikuepa,
 
Back
Top Bottom