Polepole: Muda wowote kuanzia sasa naenda kuyataja magazeti makubwa Mawili ya ‘hovyo hovyo‘ nchini Tanzania

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,925
Akizungumza mubashara kabisa leo asubuhi ndani ya kituo cha redio cha Magic FM ambacho pia kinamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM Ndugu Humphrey Polepole amesema kwamba kuanzia sasa muda wowote ataenda kuyataja magazeti mawili makubwa aliyoyaita mwenyewe kuwa ni ya ‘hovyo hovyo‘ nchini Tanzania.

Sababu kuu ya yeye kuja na hili ‘tamko‘ ni kitendo cha magazeti hayo mawili makubwa nchini Tanzania kuacha ‘kuripoti‘ vizuri na kwa haki juu ya kuhama kwa aliyekuwa Meya wa CCM Arusha Lazaro kuja CCM.

Labda niwaambieni tu kama kuna mtu ambaye ndani ya CHADEMA alikuwa na umuhimu mkubwa, amekisaidia hicho Chama, amefanya makubwa na hata Uwezo wake wa Kiutendaji hadi Kiupeo ni mkubwa kuliko wengi walioko huko ni huyu Lazaro. Binafsi nilishtushwa sana kumuona amehamia kwetu na baadae nilianza kufurahi kwani nilijua kuwa kumpata Mtu kama Lazaro basi CCM tumepiga bao la kisigino. Lakini angalia namna haya magazeti mawili ambavyo yaliripoti juu ya ujio wake huyu aliyekuwa Meya wa Arusha akiwa CHADEMA. Hawajamtendea haki na wamemripoti kama tu ni mtu mwepesi mwepesi wakati anaweza akawa ana uwezo kuliko huyo anayewadanganya au hao wachache wanaowadanganya ndani ya hicho Chama

Je, wewe unayahisi haya magazeti ni gani?

Namalizia kwa kutuma salamu zangu nyingi na za dhati kabisa kwa wakazi wapendwa wa Tabata Relini na Sinza Kijiweni.
 
😂😂😂😂😂😂🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

CCM bana...... Sasa alitaka waseme Trump ahamia CCM.....???????????

Huyo kwanza si alitoka TLP akaja CDM...... Hana uspesho wowote hata umeya Ni Lema alipiga cross Hadi akaupata.

Sisi watu weusi bado Sana.. BTW Sudan pamoja na kwamba Bashir katoka juzi wamerusha Sattelaite kwenda anga za mbali......... Nyie endeleeni kununua akina Kalist...
 
Jamaa anaharibu biashara za watu hayo magazeti hayalipi kodi au? Ndiyo maana kila raia wa nje ukimpelekea business plan aje awekeze Tanzania anakuambia hana interest na Tanzania ni kutokana na upuuzi kama huu
 
Chakubanga bwana, wao si walisema CDM haina viongozi makini? Leo huyo kahamia kwao kuunga mkono juhudi tayari amekuwa kiongozi mzuri, makini, mwenye maono na anatakiwa apewe nafasi kubwa kwenye magazeti yakielezea umahiri wake!!! Kweli siasa bila unafiki labda haiwezekani.
 
Acha hizo revelations, mada IPI uliyoitoa ya maana, eti fikra yakinifu.. Dialectic materialism ambazo zimefail Russia.... Nitawapiga hata shangazi ndiyo akili yakinifu? We nshomile vipi
Mods mnaruhusu vitu vya hovyo na kufuta mada na hoja zenye fikra yakinifu...zenye kuhitaji akili ,busara na elimu kujadiri.
Vitu vya hovyo kwenye jamii ni chachu ya kufanya jamii kua ya hovyo
 
Mods mnaruhusu vitu vya hovyo na kufuta mada na hoja zenye fikra yakinifu...zenye kuhitaji akili ,busara na elimu kujadiri.
Vitu vya hovyo kwenye jamii ni chachu ya kufanya jamii kua ya hovyo

Tengua Kauli yako haraka sana Mkuu kabla hujaiamsha ' Mizimu ' yangu na ukajuta Kunifahamu. Nimelileta hili hapa ili kuliletea Mjadala wake hasa ule wa Kifikra kwani huenda Polepole akawa ana Hoja au akawa hana vile vile juu ya hili Tamko lake. Huo ubaya wa huu Uzi uliouona Wewe hapa umetoka wapi? Je, una uhakika kwamba katika Mada za ' hovyo hovyo ' na hii yangu utaiweka? Unadhani Mimi ni Mpumbavu / Popoma kama Wewe hadi nikaiweka hapa? Kuna Vitu Moderators wanaweza wakavielewa na kuvifanyia Kazi ila kamwe siyo huu ' Upuuzi ' wako.

Halafu katika Lugha adhimu ya Kiswahili huwa hatuna neno la ' kujadiri ' kama uliloliandika hapo juu bali tuna neno sahihi la ' Kujadili ' sawa? Sasa kama Kuandika tu Kiswahili Fasaha hujui na kinakupa Shida utaweza kweli Kupambana Kihoja na Kimantiki na Mimi GENTAMYCINE? Nilikuwa sitaki Kukudharau ila kwa huu ' Ujuha ' wako uliouleta hapa sasa natangaza rasmi Kukudharau.
 
Mnyarwandwa

Back
Top Bottom