GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,853
- 109,547
Akizungumza mubashara kabisa leo asubuhi ndani ya kituo cha redio cha Magic FM ambacho pia kinamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM Ndugu Humphrey Polepole amesema kwamba kuanzia sasa muda wowote ataenda kuyataja magazeti mawili makubwa aliyoyaita mwenyewe kuwa ni ya ‘hovyo hovyo‘ nchini Tanzania.
Sababu kuu ya yeye kuja na hili ‘tamko‘ ni kitendo cha magazeti hayo mawili makubwa nchini Tanzania kuacha ‘kuripoti‘ vizuri na kwa haki juu ya kuhama kwa aliyekuwa Meya wa CCM Arusha Lazaro kuja CCM.
“ Labda niwaambieni tu kama kuna mtu ambaye ndani ya CHADEMA alikuwa na umuhimu mkubwa, amekisaidia hicho Chama, amefanya makubwa na hata Uwezo wake wa Kiutendaji hadi Kiupeo ni mkubwa kuliko wengi walioko huko ni huyu Lazaro. Binafsi nilishtushwa sana kumuona amehamia kwetu na baadae nilianza kufurahi kwani nilijua kuwa kumpata Mtu kama Lazaro basi CCM tumepiga bao la kisigino. Lakini angalia namna haya magazeti mawili ambavyo yaliripoti juu ya ujio wake huyu aliyekuwa Meya wa Arusha akiwa CHADEMA. Hawajamtendea haki na wamemripoti kama tu ni mtu mwepesi mwepesi wakati anaweza akawa ana uwezo kuliko huyo anayewadanganya au hao wachache wanaowadanganya ndani ya hicho Chama “
Je, wewe unayahisi haya magazeti ni gani?
Namalizia kwa kutuma salamu zangu nyingi na za dhati kabisa kwa wakazi wapendwa wa Tabata Relini na Sinza Kijiweni.