Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 877
- 4,106
Pole pole anapiga kazi , ana uwezo wa kujenga hoja na anayo maono makubwa kuhusu kesho ya Tanzania.
Kwa akili alizonazo hawezi kukubalika ndani ya CCM kirahisi na mwisho wa siku watampiga Majungu hata nafasi yake ya Ubalozi apokonywe. Waliona akiwa Malawi anafaidi wakampeleka Cuba . Amefika Cuba ametulia na kufanya mazungumzo na mamlaka husika na zimemwelewa, amepata fursa ya kuleta dawa tiba kwa watanzania.
Kuonyesha wana CCM walivyo na wivu na chuki, imemlazimu yeye binafsi afanye mazungumzo na hospitali ya Kairuki na kuwaomba wenye hospital nyingine wamtumie majina ya wagonjwa. Wizara ya Afya hakuna Sehemu kwenye website wala mitandao ilipoonyesha kumuunga mkono. Maana yake wapo watu wanajadili namna yakumkwamisha kwa kisingizio cha taratibu za kuingiza dawa nchini.
Watafanya hivyo kumkwamisha kwa sababu wao siyo wahanga wa magonjwa haya manne anayowaza kutusaidia mdogo wetu Polepole. Wapo watu wizara ya Afya watataka waende Cuba kujiridhisha na dawa hizi kwa gharama za serikali au cuba , jiulize kama hizo dawa hazipo nchini wao walizosomea wapi hadi wakazifanyie uchunguzi?
Nimeandika haya kwa sababu kwenye moja ya droup la whatsapp nimeona kiongozi mmoja Mwanza mwenye taaluma ya dawa akisema Polepole hatofanikiwa kwenye mpango wake kwa sababu hizo dawa anqzosema hazijasajiliwa na Mamlaka za Tanzania na kwamba serikali haiwezi kuziruhusu ziingie nchini. Pia ameongeza hakuna dawa zinaingizwa nchini kwa sababu tu balozi kaomba, dawa zinatakiwa zifanyiwe utafiti na wataalam wetu aidha kwa wao kwenda Cuba au sample kuletwa Tanzania. Haya mawazo ndiyo mtizamo wa wasomi wengi wa Afya, ndio mtizamo wa washauri wa serikali kwamba wao dawa hawana lakini wanataka wapewe wazichunguz3....Pole pole usikate tamaa tunahitaji msaada huu wa tiba kwa ajili ya ndugu zetu. Ila fanyia utafiti vikwazo vinavyotarajiwa kuwekwa na wanasiasa wenzako kukuzina mdomo na kukufanya uonekane umewalaghai wananchi.