GE2025 Polepole kachemka, bora angemtafuta msemaji mwingine kusema maneno yale

GE2025 Polepole kachemka, bora angemtafuta msemaji mwingine kusema maneno yale

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Inahitaji akili ya juu unapopanga jambo kama hilo. Kama Polepole angerudisha band nyuma kidogo (2020-Uchaguzi wa wabunge), na kumuona Polepole wa wakati ule akajilinganisha na Polepole wa 2025, kweli asingesema maneno hayo.

Kitu sahihi cha kufanya katika hali hiyo ni kuingiza maneno hayo katika kinywa cha mtu mwingine, vinginevyo ataonekana yeye mwenyewe kuwa ni MUHUNI NAMBA 1.

Sasa kalishalikorogo, hana cha kufanya ispokuwa kuogelea bahari asiyeimudu akiwa PANGONI. Kwa sasa ana mambo matatu tu ya kufanya.
  • Kuomba ukimbizi ughaibuni
  • Kuomba msamaha katika Press ile ile aliyejitokeza
  • Kutokomea kusikojulikana.
Kama kachemka bona kila kukicha mnasogeza mbele tarehe za Mkutano Mkuu? Mnafikiri mkipeleka mbele tarehe hiyo haitafika?
 
Kama.kachemka bora kila kukicha mnasogeza mbele tarehe za Mkutano Mkuu? Mnafikiri hata mkipeleka mbele haitafika?
Tutafika tu, ila Polepole asijifanye kuwa yeye ndio mtakatifu sana. Na mbaya zaidi anapenda kujifanya kuwa yeye ni mtu wa MUNGU SANA. Binafsi namuona kama mtumwa wa shetani, na sasa anataka kutuharibia nchi. Hii ndio kazi kubwa ya SHETANI, kufitinisha watu mpaka waingie katika mgogoro mkubwa.
 
Wapo watu wengi wanatamani hiyo kazi yake ya Ambassador, tumesema moyo wake haujatulia. Anatamani kuwa President kitu ambacho ni very impossible
Wewe ni nani ujue hatima ya kesho ya Polepole?
Nani miaka 10 iliyopita alijua Samia atakuwa raisi?
 
Polepole kaongea mara moja tu lakini wiki nzima hamlali usiku kucha mnatoa milio ya kila aina , hakika amekujambisheni sawa sawa.
 
Hazina mashiko yoyote. Lema kampambanua vizuri sana. Polepole ni mshtakiwa namba one. Kwa kuibaka demokrasia yetu.

Eti anasema Demokrasia, hivi POLEPOLE alikuwa mtu wa kutaja na kutetea Demokrasia kweli. Mchozi unataka kunitoka nikikumbuka enzi zake.

Kama mna kifua, Leteni video zake za wakati ule, halafu zilinganisheni na za sasa. MBAKAJI MKUBWA WA DEMOKRASIA.
mgombea batili kakataliwa, tulitegemea mtoe milio kama hii
mtu anataka awe rais mara mbili kwa dezo thubutu!
 
Hiyo sio ajenda kuu. La msingi ni kuwa vyombo vyote vilivyohitajiwa kuwepo kumpitisha mgombea wa CCM vilikuwepo pale. Na vilifanya kazi yake. Na kubwa zaidi uchaguzi ulifanyika wa wazi na huru. Dr Samia akaibuka kwa ushindi wakishindo.

Unajua ni kwanini msajili wa vyama aliwapiga ban chadema?

Ni kwa mfano wa kosa kama hilo

So kwa maana hiyo ni kwamba, kosa la sisiem sio kosa ila kosa la chadema ndio kosa au sio?

Katiba na utaratibu wenu miaka yote ukoje?
 
Kabla ya kumjadili Polepole kwanza jiulize.
Alichosema ni kweli au siyo kweli?
Kilichotokea Dodoma kumpitisha samia hapo February ni sawa?
Je wewe ulimuelewa Polepole.
Kuishi uhamishoni hata kina Oliver tambo walishaishi tu wala siyo jambo jipya labda kwako
Alichosema ni kweli au siyo kweli?
Kilichotokea Dodoma kumpitisha samia hapo February ni sawa?
Je wewe ulimuelewa Polepole
 
Kachemka alafu wiki nzima machawa wote wa ccm mmetumwa kumjibu
Mtu aliyechemka hupuuzwa
 
Inahitaji akili ya juu unapopanga jambo kama hilo. Kama Polepole angerudisha band nyuma kidogo (2020-Uchaguzi wa wabunge), na kumuona Polepole wa wakati ule akajilinganisha na Polepole wa 2025, kweli asingesema maneno hayo.

Kitu sahihi cha kufanya katika hali hiyo ni kuingiza maneno hayo katika kinywa cha mtu mwingine, vinginevyo ataonekana yeye mwenyewe kuwa ni MUHUNI NAMBA 1.

Sasa kalishalikorogo, hana cha kufanya ispokuwa kuogelea bahari asiyeimudu akiwa PANGONI. Kwa sasa ana mambo matatu tu ya kufanya.
  • Kuomba ukimbizi ughaibuni
  • Kuomba msamaha katika Press ile ile aliyejitokeza
  • Kutokomea kusikojulikana.

Polepole katumia haki yake ya kikatiba na kibinadamu kujieleza.

Mambo mengine yote ya alifanya nini lini vipi ni false dichotomy fallacy.

Polepole si mtume, si hero, si msafi sana, tunajua ana makandokando mengi.

Ila, kitu muhimu kuliko Polepole ni hoja. Usimjadili mtu, jadili hoja.

Kwa sababau kama Polepole kaongea hoja ya ukweli, hata akifa leo, hoja ya ukweli itabaki kuwa ya ukweli tu.

Mtu akikosea jana haina mana leo hana haki ya kubadilisha mawazo na kufanya tofauti.
 
Tutafika tu, ila Polepole asijifanye kuwa yeye ndio mtakatifu sana. Na mbaya zaidi anapenda kujifanya kuwa yeye ni mtu wa MUNGU SANA. Binafsi namuona kama mtumwa wa shetani, na sasa anataka kutuharibia nchi. Hii ndio kazi kubwa ya SHETANI, kufitinisha watu mpaka waingie katika mgogoro mkubwa.

Mungu na Shetani ni mambo ya hadithi za kutungwa na watu tu. Nikikubana uthibitishe wapo kweli hutaweza.

Hayo mambo ya utakatifu ni mbwembwe tu. Kwenye saikolojia kuna kitu kinaitwa "virtue signaling". That was just virtue signaling. Ma inawezekana Polepole ana unafiki mwingi au hata hila za kisiasa.

Kwenye kuongea, Watanzania kiujumla hawajui kufanya kitu kinaitwa "sticking to the message". Kuwa focused kwenye main point iliyokuleta bila kuleta stories nyiingii za ku distract watu kutoka kwenye main message. Huu mtihani Watanzania karibu wote wanafeli.

Nikianza na marais, marais karibu wote wa Tanzania wamefanya kosa hili.Kuanzia Nyerere mpaka Samia. Aliyeukwepa katika marais ni Mkapa tu, kwa sababu alikuwa muandishi wa habari na hotuba zake karibu zote alisoma.

Mtu akiwa na point moja ya muhimu kuongelea atakupa hadithi mia moja na moja. Polepole is no exception, so I am not going to judge him harshly for being verbose. That is a Tanzanian character. Ningeshangaa asingekuwa all over the place. Very few Tanzanians are capable of that discipline in unprepared speech.

Lakini mbwembwe, unafiki, hila za kisiasa na indisciplined speech hazimaanishi hana point ya msingi na ya kweli.
 
Kachemka. Kwa wenye akili akiwa yeye ni character ndio hayana thamani kabisa. Kumbuka, watu wa Hitler mpaka leo wakiwa na zaidi ya miaka 90 wakipatikana kokote walikojificha wanafunguliwa kesi na kuhukumiwa.
Sembuse Polepole aliyetuharibia uchaguzi mwaka 2020.

Hatuhitaji kusahau ujinga wake, mahali pake ni Lupango tu.
Leo ndio unakiri hayo wakati mlikuwa mnajisifia kushinda kwa kishindo? Halafu kwa huu upuuzi wenu ndio mnataka bado tuingie kwenye uchaguzi kwa sheria hizo hizo mbovu?!
 
Polepole katumia haki yake ya kikatiba na kibinadamu kujieleza
Ni kweli na Tupo pamoja kwenye hoja hii
Mambo mengine yote ya alifanya nini lini vipi ni false dichotomy fallacy.

Polepole si mtume, si hero, si msafi sana, tunajua ana makandokando mengi
Hapa tunatofautiana, tena sana. Ni upungufu kumpa mtu point kwa kuangalia aliyoyasema leo bila kuangalia jana yake. Polepole si mtume ni kweli, lakini ni lini aliomba msamaha kwa Watanzania kwa Makosa aliyofanya ili tumsafishe. Bahati mbaya mimi sijamsikia. Kama una video au maandishi alipoomba msaha, tafadhali niwekee hapa kwa faida ya wote.
Hata siku moja hajasema kuwa uchaguzi mwaka 2020 ulikuwa batili, hasa mchakato wa wabunge.
Ila, kitu muhimu kuliko Polepole ni hoja. Usimjadili mtu, jadili hoja.

Kwa sababau kama Polepole kaongea hoja ya ukweli, hata akifa leo, hoja ya ukweli itabaki kuwa ya ukweli tu
Hoja ndizo tunazozijadili. Sina haja na sura yake, shati lake, umbo lake wala mali yake. Ninachojadili hapa ni hoja, na hasa kwa Polepole ni lazima tumjadili msimamo wake akiwa sehemu ya utawala 2020. mchakato wa uchaguzi wa wabunge 2020- Msimamo wake. hIZI NDIO HOJA ZA MSINGI.
Ni dhambi kujadili hoja zake za leo bila kuangalia alifanya nini 2020.
 
Ni kweli na Tupo pamoja kwenye hoja hii

Hapa tunatofautiana, tena sana. Ni upungufu kumpa mtu point kwa kuangalia aliyoyasema leo bila kuangalia jana yake. Polepole si mtume ni kweli, lakini ni lini aliomba msamaha kwa Watanzania kwa Makosa aliyofanya ili tumsafishe. Bahati mbaya mimi sijamsikia. Kama una video au maandishi alipoomba msaha, tafadhali niwekee hapa kwa faida ya wote.
Hata siku moja hajasema kuwa uchaguzi mwaka 2020 ulikuwa batili, hasa mchakato wa wabunge.

Hoja ndizo tunazozijadili. Sina haja na sura yake, shati lake, umbo lake wala mali yake. Ninachojadili hapa ni hoja, na hasa kwa Polepole ni lazima tumjadili msimamo wake akiwa sehemu ya utawala 2020. mchakato wa uchaguzi wa wabunge 2020- Msimamo wake. hIZI NDIO HOJA ZA MSINGI.
Ni dhambi kujadili hoja zake za leo bila kuangalia alifanya nini 2020.
Unamjadili Polepole na alifanya nini huko nyuma na kafanya nini leo.

Hujadili hoja ya Polepole kwamba Tanzania kuna ombwe la uongozi na Samia kapitishwa harakaharaka bila kufuata utaratibu.

Small minds discuss people, average minds discuss events, great minds discuss ideas.

Nishakwambia Polepole ni inconsistent, si mtume, si hero, ana makandokando mengi. Hilo tunajua.

Hakuna kiongozi asiye na makandokando. So Polepole is not unique in that.

Ila, mbona unaacha kujadili hoja za msingi alizotoa Polepole unaishia kwenye ad hominem logical fallacy kwa kumu attack Polepole kwa character yake binafsi?

Unaelewa ad hominem fallacy ni nini?
 
Mungu na Shetani ni mambo ya hadithi za kutungwa na watu tu. Nikikubana uthibitishe wapo kweli hutaweza.

Hayo mambo ya utakatifu ni mbwembwe tu. Kwenye saikolojia kuna kitu kinaitwa "virtue signaling". That was just virtue signaling. Ma inawezekana Polepole ana unafiki mwingi au hata hila za kisiasa.

Kwenye kuongea, Watanzania kiujumla hawajui kufanya kitu kinaitwa "sticking to the message". Kuwa focused kwenye main point iliyokuleta bila kuleta stories nyiingii za ku distract watu kutoka kwenye main message. Huu mtihani Watanzania karibu wote wanafeli.

Nikianza na marais, marais karibu wote wa Tanzania wamefanya kosa hili.Kuanzia Nyerere mpaka Samia. Aliyeukwepa katika marais ni Mkapa tu, kwa sababu alikuwa muandishi wa habari na hotuba zake karibu zote alisoma.

Mtu akiwa na point moja ya muhimu kuongelea atakupa hadithi mia moja na moja. Polepole is no exception, so I am not going to judge him harshly for being verbose. That is a Tanzanian character. Ningeshangaa asingekuwa all over the place. Very few Tanzanians are capable of that discipline in unprepared speech.

Lakini mbwembwe, unafiki, hila za kisiasa na indisciplined speech hazimaanishi hana point ya msingi na ya kweli.
... point ya msingi huwa inasindikizwa na ka'defence mechanism', hasahasa point hiyo ikiwa dhaifu! ... hapa Polepole, pole zake, anajaribu kuwavuta waumini wa kweli wamuone nayeye ni mwenzao anayetaka MBINGU TUUU!
 
Sisi ambao hatuamini Mungu wala mbingu tunaona hizi ghasia tu.

Kwenye siasa, keep it secular please.

Kama unataka kuhubiri Mungu anzisha kanisa, msikiti au taasisi ya kidini.
 
Kabla ya kusema kama amechemka au kupoa labda kwanza tungejiuliza au ungetwambia Motive yake ilikuwa ni nini ?

Kama tukiamini kwamba Motive yake ilikuwa ni kusema kilicho rohoni mwake basi kulikuwa hakuna jinsi ya kufanya (tumeona kina Mpina hata wakipigania wenye nchi kwa kuwaeleza ukweli kuhusu sakata la Sukari wanaishia kupigwa pini na kuitwa watovu wa nidhani kwenye Kamati ya Bunge)

Nadhani sometimes njia pekee ya kudeal na wahuni ni kihuni...
 
Lakini mbwembwe, unafiki, hila za kisiasa na indisciplined speech hazimaanishi hana point ya msingi na ya kweli
Hapa ndio tunaweka kituo- Unafiki, hila za kisiasa na indiscipline speech... Kwa neno moja hawa ndio wanaitwa WAHUNI. Polepole naye yumo humo. Ni unafiki mkubwa eti uwe madarakani hukufanya hata moja kati ya haya unayoyalalamikia, aliingiwa na nini? Kilichomuingia tafuta jina lolote utalolipenda lakini maana ni moja tu.
 
Back
Top Bottom