denoo49
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 6,113
- 6,953
Kwa kauli za kila mwanachi abebe msalaba wake, ndi recognition yenyewe?Nimemuelewa pole pole hapo, ana maana kwamba, ccm kiwe ni chama cha maskini na wanyonge, wapaze sauti zao zisikike ili waweze kujikwamua na umaskini.
kwa upande mwingine bashe yupo sahihi kwamba umaskini sio sifa, na wala haiwezi kuwa sifa ya uadilifu. lakin anashindwa ku recognise idea ya pole pole kwamba ukitaka kuwainua maskini ni lazima uwape nafasi ya kuwasikiliza na kuwarecognise ili nao waweze kuinuka.
Ni vizuri kuuchukia umaskini, lakin usiwachukie maskini, kaa nao, kula nao, waheshimu na wape nafasi ya kujikwamua na umaskini. naona bashe anauchukia umaskini pamoja na maskini wenyewe.
Na yote kwa yote, bashe ni hazina kubwa ya ccm, wakimtumia vizuri anaweza kusaidia kujenga chama na taifa kwa ujumla.
Hivi Kuna mtu anajua kesho kuna janga gani la taifa linakuja?
Sasa leo masikini kaongezewa umaskini na janga la taifa, bado unakuja na kauli kama hizo ndio kumsikiliza kwenyewe unakomaanisha.
Hivi majuzi nilikuwa kagera, mfuko wa cement za msaada ni 15 elfu, hizi za kawaida ni 20 elfu.
Na kama tunavyojua UJENZI wa nyumba sio wa siku moja au wiki moja, na mbaya zaidi Unaweza kukuta baadhi ya raia aliyevunjikiwa nyumba, kwa siku au wiki hata hiyo 15 or 20 elfu ya mfuko wa saruji haipati, je tuendelee kuwafariji kwa kauli hizo na kuzidi kuwaacha kwenye maturubali wazidi kumenyeka?