Alloyce PR
JF-Expert Member
- Nov 15, 2020
- 798
- 865
66 UMASKINI WA KUJITAKIA NA KITENDAWILI CHA MCHANGO,
UCHAGUZI NGUVU YETU
Hebu tushirikiane kutafuta jibu la hili fumbo: Chama cha siasa Afrika kinaingia mtaani na kuwapa wananchi somo la ulaghai kwamba serikali imewafanya maskini. Wananchi wanaitikia kwa huzuni, 'Kweli kabisa!'
CHAMA KINAWEZA
Lakini cha ajabu, hapo hapo hicho chama kinaanza kuwakusanya hao hao maskini waliochoka kisha kuwaomba PESA ili waweze kujaza mafuta kwenye magari yao. Sasa hapa, nani ana uhitaji zaidi kati ya chama na yule mwananchi anayetafuta hela ya kula kwa kusuasua? Hapo ni kama kumnyang'anya mgonjwa dawa ili ukarabati hospitali!
Aombaye hupewa na Mungu huibariki mkono unaotoa.
Na tukienda madhabahuni, hali ni hiyohiyo. Mchungaji anasimama kwa bashasha na kuwaaminisha waumini wake kwamba 'aombaye hupewa na Mungu huibariki mkono unaotoa.' Lakini siku mchungaji huyo huyo akiamua kubadili gari la mwaka jana kwa sababu limechoka, ghafla anageuka kuwa mhasibu na kuanza kukusanya michango ya waumini ili 'mkono ule uweze kununua mashine mpya ya kutembelea.'
MICHANGO YA WAAMINI
JENGO
MASHINE
GARI MPYA
SAFARI ZA KIKAZI
+
Mbona kama huku ndiko kule 'ujinga' uleule ambao waasisi wetu wa Ukombozi wa Afrika walipigana nao kwa jasho na damu? Inaonekana tumekuwa wataalamu wa kucheza dansi ya umaskini; viongozi kwenye vyama vya siasa wanatunga muziki, wananchi wanacheza kwa bidii, na mwisho wa siku, wote wanabaki kutazama mfuko mtupu!
Na: Alloyce, P.R.