Polepole: CCM kitakuwa chama cha maskini na wanyonge - Bashe: Umaskini sio sifa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
FB_IMG_1483425612379.jpg
Ndo tujue Umaskini unasababishwa na CCM ili watawale wataka
 
Ndo tujue Umaskini unasababishwa na CCM ili watawale watakavyo
Kina Lowasa walijiunga wakiwa hawana chochote na utajiri wameupatia CCM, sasa CCM wanafanyaje wawe masikini.. Jaribu kumuelewa Polepole... Tunajua siku zote masikini hana sauti, ni mnyonge sasa CCM inataka awo watu wakimbilie CCM, ili kupaza sauti
 
Kina Lowasa walijiunga wakiwa hawana chochote na utajiri wameupatia CCM, sasa CCM wanafanyaje wawe masikini.. Jaribu kumuelewa Polepole... Tunajua siku zote masikini hana sauti, ni mnyonge sasa CCM inataka awo watu wakimbilie CCM, ili kupaza sauti
tangu lini ccm ikasaidia wanyonge

ccm imekuwa ni chaka la wezi na wapiga dili na kamwe haisaidii wanyonge inanyonga wanyonge si ni juzi hapa raisi kasema wapiga dili walikuwa washafanya yao kwa dangote ,,, pale miajira kibao ya watanznia ingepotea


by the way walichukuliwa hatua gani hawa wapiga dili au ilikuwa funika kombe mwanaharamu apite maana sijasikia tena walipelekwa wapi
 
Nimemuelewa pole pole hapo, ana maana kwamba, ccm kiwe ni chama cha maskini na wanyonge, wapaze sauti zao zisikike ili waweze kujikwamua na umaskini.

kwa upande mwingine bashe yupo sahihi kwamba umaskini sio sifa, na wala haiwezi kuwa sifa ya uadilifu. lakin anashindwa ku recognise idea ya pole pole kwamba ukitaka kuwainua maskini ni lazima uwape nafasi ya kuwasikiliza na kuwarecognise ili nao waweze kuinuka.

Ni vizuri kuuchukia umaskini, lakin usiwachukie maskini, kaa nao, kula nao, waheshimu na wape nafasi ya kujikwamua na umaskini. naona bashe anauchukia umaskini pamoja na maskini wenyewe.

Na yote kwa yote, bashe ni hazina kubwa ya ccm, wakimtumia vizuri anaweza kusaidia kujenga chama na taifa kwa ujumla.
 
Bashe anajielewa sio wanafiki hawa ? Chadema aaaaaaah nimekosea sio chadema
 
Tunajua toka zamani CCM imekuwa ikiogopa kuongoza matajiri. Nakumbuka miaka ya 70. Waharabu, wahindi na wazungu ndyo walikuwa wakichukua mikopo mikubwa ya biashara bank. Ila watz walikuwa wanabaniwa ili wasije kuwa matajiri. Ndyo maana wahindi na waharabu wengi tz ni matajiri kuliko watanganyika
 
Bashe ni luba wa lowassa chochote kitakachoongelewa kutamkwa au kufanywa hadharani chenye mrengo wa kumgusa lowassa kwa namna moja ama nyingine lazima atapinga
Futa kauli yako hyo haraka bashe ni level zingne kabisa ni msema ukwel
 
Polepole anasema hivyo kufurahisha baraza. Anafahamu fika kuwa CCM ndiyo imelifikisha taifa hapa ilipo hivyo bbasi wakati akihangaika kutafuta ungwaji mkono lazima aeneze propaganda kama hizi.

Bashe kwa upande wake anazungumza ukweli halisi ambao wengi ndani ya CCM hawataki kuusikia. Bahati nzuri mambo kama hata yanatokea wakati wananchi hawadanganyiki tena.

Ni ukweli usiyopingika kuwa historia ikizingatiwa ndiyo pumzi za mwisho mwisho kwa CCM.

Viwanda vimekufa mikononi mwao na madhambi mengi kama vile Deep green, Meremeta, Richmond, Lugumi, Escrow zilikofanyika. Tusiaminishwe uongo waliohusika wote ambao ni matajiri walioisadia hiyo taasisi inayodaiwa na polepole kuwa ni ya wanyonge waadhibiwe wote kwa mujibu wa sheria. Hii itatupa imani kuwa CCM kweli ni kimbilio la wanyonge.

Vinginevyo tuendelee kuimba ngonjera isiyokuwa na ukweli na utakatifu ndani yake.
 
View attachment 453635 Ndo tujue Umaskini unasababishwa na CCM ili watawale wataka
Kimsingi CCM ijiangalie vizuri sana kiitikadi ili iweze kukidhi matakwa ya watu wote.
Umasikini sio dili, na mtu masikini siku zote atataka kuondokana na umasikini.

Sasa kama utakuwa na sera ya kuendeleza viwanda, hii ninaendana vipi na suala la ajira na kuondoa umasikini, hilo ndio swala muhimu.
Halafu watakaojenga viwanda ni nani haswa, ni serikali au wafanya biashara?
Je serikali itaweza kujenga viwanda vingi ili ku absorb vijana wengi walioko mitaani na hatimaye kuondoa umasikini na umachinga?
Je nini nafasi ya wawekezaji wa ndani/afayabiashara ambo ni dhahiri sio masikini, ni vema serikali ikatamka kuwa hawa maslahi yao ni yepi?
Au kama tumeshawabatiza jina geni la wapiga dili!!!

Haya ni masuala ya muhimu sana kuapatia majibu, kwa maana kwa lolote tutakalo amua una madhara.
Ni heri tu tukazane kelekea kwenye malego tuliyojiwekea ya kujenga viwanda vingi iwezekanavyo, ili kuondoa si tu umasikini bali kuinua uchumi.
 
Kina Lowasa walijiunga wakiwa hawana chochote na utajiri wameupatia CCM, sasa CCM wanafanyaje wawe masikini.. Jaribu kumuelewa Polepole... Tunajua siku zote masikini hana sauti, ni mnyonge sasa CCM inataka awo watu wakimbilie CCM, ili kupaza sauti
Kwa maana hiyo mtaji wa ccm ni umaskini siyo? Na haitakaa hata siku moja inahakikisha hao watu wanapata sauti yao wenyewe maana wakipata sauti chama hakitakuwepo, siyo? Kwa jinsi yoyote ile ccm inahakikisha watu wanabaki na elimu duni ili majinga yawe mengi muyaburuze mtakavyo. Na mjinga hawezi kuwa na sauti kwasababu haijui kazi ya sauti yake ni nini. Na mjinga hana maarifa ya kuyakabili mazingira na kuboresha maisha yake. Fanyeni hayo lakini mjue Mungu anawaona.
 
Back
Top Bottom