Polepole: CCM kitakuwa chama cha maskini na wanyonge - Bashe: Umaskini sio sifa

Polepole: CCM kitakuwa chama cha maskini na wanyonge - Bashe: Umaskini sio sifa

Ni wachache wanajua kuwa vyama vingi tawala Afika kusini mwa jangwa la sahala vinatumia umaskini na ufukara wa raia wao kutawala na kubaki madarakani kwa mgongo wa kwamba wao(vyama hivyo) ndio suluhisho lao pekeee lakuwaondoa kwenye
ufukara na umaskini wao huku kwa miongo kadaa umaskini na ufukara umetamalaki kusini mwa jangwa la sahara.
 
Mwambieni Bashe( moderators mngekuwa wa wazi kwa wote ningewaambia mpeni na jina langu ) utajiri halali ni jambo la heri,utajiri wa wizi na dhuluma ni jambo la shari na laana.

Kuna eneo anatuhumiwa Bashe kulinnyang'anya kwa wakulima wanyonge kando ya Ruvu na lina hati.Je kawarudishia wenye nalo? je ndiyo aina ya utajiri anaousifia na ni njia sahihi ya kuupata?

Mnaotaka ushahidi nendeni Ruvu darajani mkaulize je kuna tuhuma kama hii? ilianzaje? ulizeni ni lini imeanza? maana hatua zikichukuliwa hamchelewi kusema visasi,huyu alikuwa kundi la Fulani.

Hakuna anayependa umaskini wala kuwa na wananchi maskini ila ni wendawazimu kutegemea miujiza iondoe umaskini.
 
Ni mimi mr mkiki.

15822901_1813631085592102_8973469880834679143_n.jpg
 
Mimi huwa sihisi vitu, natumia akili yangu tu aliyonipa Mungu baba. Hivyo kwa kutumia akili yangu, ninakiri kuwa hawa wote ni vibaka wa fadhila na si watu wa kuwaamini.
 
Bashe sio wa kufaninisha na mnafiki polepole............

Bashe ukimwangalia unaona kabisa kuna kitu anakisimamia na ni mkweli.........

Polepole anaongea kitu ambacho wala hamaanishi......

Polepole huyu huyu Msaliti wa katiba ya wananchi.......
 
Bashe sio wa kufaninisha na mnafiki polepole............

Bashe ukimwangalia unaona kabisa kuna kitu anakisimamia na ni mkweli.........

Polepole anaongea kitu ambacho wala hamaanishi......

Msaliti wa katiba ya wananchi.......
nice
 
hujamuelewa bado polepole...mfuatilie polepole utamuekewa tu...
 
Nikimkumbuka H.POLEPOLE wa katiba mpya na nikimlinganisha na H.BASHE nadiriki kusema kama wote wakitumia akili zao halisi bila unafiki wana akili kubwa lakin kwa kipimo cha hayo yaliyopo hapo mezani ni kwamba H.POLEPOLE kaongea kwa mazoea na H.BASHE kaongea kwa uhalisia.
 
Ni bora umuamini ibilisi baba yake shetwani mjomba wake Laanakum kuliko kumuamini mwanasiasa
 
Back
Top Bottom