Polepole: CCM kitakuwa chama cha maskini na wanyonge - Bashe: Umaskini sio sifa

Polepole: CCM kitakuwa chama cha maskini na wanyonge - Bashe: Umaskini sio sifa

Naona kuna watu washaona Watanzania watabaki masikini miaka yote. Wanawaundia chama chao......
So low
Hahahahaha badala ya kuwasaidia kwa mikakati iliyo thabit na inayo onekana wana wapa ahadi na kuwaundia chama chao waendelee kua maskin
 
Chaka la wezi lililokuwa linaongozwa na lowassa
Katika hizi skendo Lowassa kuhusika ipi.?

Loliondo gate.
Chavda.
Epa.
Net group.
Bot Twin Towers.
Dowans.
Escrow.
Symbion power.
Iptl.
Mabilioni ya JK.
Pesa za Ghadafi, Libya investment company.
Rada ya jeshi.
Pesa za vitambulisho Nida.
Gage ya mafuta bandarini.
Wizi wa makontena bandarini.
Tenda ya kofia na t-shirt za kampeni - deni la shigongo.
Meli ya uvuvi ya wa Vietnam.
Ununuzi wa meli mbovu, mv Dar es Salaam.
Uuzaji wa nyumba za serikali.


Kashfa hizi na nyingine nyingi ziliratibiwa (usimamizi na utekelezaji) na chama kile.

Chama kile na mafisadi ni damu damu.
 
Katika hizi skendo Lowassa kuhusika ipi.?

Loliondo gate.
Chavda.
Epa.
Net group.
Bot Twin Towers.
Dowans.
Escrow.
Symbion power.
Iptl.
Mabilioni ya JK.
Pesa za Ghadafi, Libya investment company.
Rada ya jeshi.
Pesa za vitambulisho Nida.
Gage ya mafuta bandarini.
Wizi wa makontena bandarini.
Tenda ya kofia na t-shirt za kampeni - deni la shigongo.
Meli ya uvuvi ya wa Vietnam.
Ununuzi wa meli mbovu, mv Dar es Salaam.
Uuzaji wa nyumba za serikali.


Kashfa hizi na nyingine nyingi ziliratibiwa (usimamizi na utekelezaji) na chama kile.

Chama kile na mafisadi ni damu damu.
Ni kweli ccm na mafisadi ni damu damu ni mlezi wake na ndio iliyomlea lowassa. Kifupi ccm na lowassa hawafai
 
Kwa hiyo sera ya CCM ni kuwafanya watu wanyonge na masikini hapana huyu Polepole amesahau kauli mbinu yetu ya chama
Sasa mkiwa matajiri mtasema wenyewe hamtakuwa wanyonge wala ili msemewe na ccm. Ccm itasema kile ambacho ni kizuri machoni mwa ccm.

Ccm ina wenyewe, na wenyewe wanahitaji maskini ili wa wanyonge na kuwasemea.
 
Polepole anasema hivyo kufurahisha baraza. Anafahamu fika kuwa CCM ndiyo imelifikisha taifa hapa ilipo hivyo bbasi wakati akihangaika kutafuta ungwaji mkono lazima aeneze propaganda kama hizi.

Bashe kwa upande wake anazungumza ukweli halisi ambao wengi ndani ya CCM hawataki kuusikia. Bahati nzuri mambo kama hata yanatokea wakati wananchi hawadanganyiki tena.

Ni ukweli usiyopingika kuwa historia ikizingatiwa ndiyo pumzi za mwisho mwisho kwa CCM.

Viwanda vimekufa mikononi mwao na madhambi mengi kama vile Deep green, Meremeta, Richmond, Lugumi, Escrow zilikofanyika. Tusiaminishwe uongo waliohusika wote ambao ni matajiri walioisadia hiyo taasisi inayodaiwa na polepole kuwa ni ya wanyonge waadhibiwe wote kwa mujibu wa sheria. Hii itatupa imani kuwa CCM kweli ni kimbilio la wanyonge.

Vinginevyo tuendelee kuimba ngonjera isiyokuwa na ukweli na utakatifu ndani yake.
Ccm ni ile ile hata atakaporudi Yesu Kristu.

Ccm ina wenyewe.
 
Kimsingi CCM ijiangalie vizuri sana kiitikadi ili iweze kukidhi matakwa ya watu wote.
Umasikini sio dili, na mtu masikini siku zote atataka kuondokana na umasikini.

Sasa kama utakuwa na sera ya kuendeleza viwanda, hii ninaendana vipi na suala la ajira na kuondoa umasikini, hilo ndio swala muhimu.
Halafu watakaojenga viwanda ni nani haswa, ni serikali au wafanya biashara?
Je serikali itaweza kujenga viwanda vingi ili ku absorb vijana wengi walioko mitaani na hatimaye kuondoa umasikini na umachinga?
Je nini nafasi ya wawekezaji wa ndani/afayabiashara ambo ni dhahiri sio masikini, ni vema serikali ikatamka kuwa hawa maslahi yao ni yepi?
Au kama tumeshawabatiza jina geni la wapiga dili!!!

Haya ni masuala ya muhimu sana kuapatia majibu, kwa maana kwa lolote tutakalo amua una madhara.
Ni heri tu tukazane kelekea kwenye malego tuliyojiwekea ya kujenga viwanda vingi iwezekanavyo, ili kuondoa si tu umasikini bali kuinua uchumi.
Kipaumbele cha kwanza ni ndege za mapangaboi, "tunataka watalii wapande ndege zetu".

Ajira, viwanda, kilimo, biashara, elimu, afya weka kule.!
 
Polepole kwa sasa ni mganga njaa. Sisi tunapambana na umaskini yeye anajipambanua kwa sifa umaskini. Binafsi nauchukia sana umaskini. Ni bora ajipambanue ktk dhana ya 'chama cha wakulima na wafanyakazi' umaskini na ynyonge mwiko
 
No way Ccm ikabadilika unless makada wakuu watoke waanzishe vyama vingine au Ccm ife kwanza...Hivi ccm ikifutwa leo nini kinatokea kwa viongozi waliopata madaraka kupitia chama hiki?
 
Kwa maana hiyo mtaji wa ccm ni umaskini siyo? Na haitakaa hata siku moja inahakikisha hao watu wanapata sauti yao wenyewe maana wakipata sauti chama hakitakuwepo, siyo? Kwa jinsi yoyote ile ccm inahakikisha watu wanabaki na elimu duni ili majinga yawe mengi muyaburuze mtakavyo. Na mjinga hawezi kuwa na sauti kwasababu haijui kazi ya sauti yake ni nini. Na mjinga hana maarifa ya kuyakabili mazingira na kuboresha maisha yake. Fanyeni hayo lakini mjue Mungu anawaona.
Kwani ulikuwa hujui?

Ccm ina hitaji
1. maskini,
2. wajinga(wasiokuwa na elimu)
3. wapumbavu(wenye elimu lakini hawajitambui) .
4. Siasa mbovu (fitna, dhuluma, uonevu, uvunjifu wa haki za binadamu)
5. Ufisadi.
6. Afya mbovu (maradhi)
7. Ubinafsi (ukanda, ukabila, udini,)
 
Kina Lowasa walijiunga wakiwa hawana chochote na utajiri wameupatia CCM, sasa CCM wanafanyaje wawe masikini.. Jaribu kumuelewa Polepole... Tunajua siku zote masikini hana sauti, ni mnyonge sasa CCM inataka awo watu wakimbilie CCM, ili kupaza sauti
Bashe ndio ameongea kitu cha muhimu...Elimu! Ungekuwa na elimu ungebaini nani ni kinara wa kuwakataza wanyonge kupaza sauti...hadi imetungwa sheria kuwabana wenye midomo halafu we unataka kuniambia nini?
 
Sauti ya wanyonge kivipi akati mkuu wao anataka watu waishi kama mashetani?
 
..
Ni vizuri kuuchukia umaskini, lakin usiwachukie maskini, kaa nao, kula nao, waheshimu na wape nafasi ya kujikwamua na umaskini. naona bashe anauchukia umaskini pamoja na maskini wenyewe...
Wahenga walinena, "aliye juu mgonje chini".

Sauti ya maskini na mnyonge ni umoja.

Tofauti ya Polepole na Bashe ni mtizamo wa maana ya "maendeleo".

Mmoja anawakilisha kundi la wanaotumiwa (nguvu ya maskini ndo utajiri wake) mwingine anawakikisha kundi la wanawaowatumia wengine (nguvu ya maskini ni mtaji wa tajiri).

Wanaochukia umaskini hawajui maisha ya umaskini. Wanauchukia umaskini kwa kuwa hawajisikii vizuri kuishi nao japo nguvu zao ndo utajiri wao.

Hao wanaochukia umaskini ni hao hao wanaoishi peponi, ambao utawala wa sasa unawajengea mazingira ya kuishi kishetani.

Hiyo ndo tofauti ya Polepole na Bashe.
 
Kwa hiyo target kuu ya CCM ni kuwafanya Watanzania kuwa wanyonge na Maskini
Unasikia kauli kama hizi :-

"walikuwa wanaishi kama malaika sasa wataishi kama mashetani"

"mlizoea kupiga dili, sasa dili hakuna"

"serikali haitaweza kuwasaidia, kila mtu abebe msalaba wake "

" natamani jeshi la malaika lishuke kutoka mbinguni ili lizime mitandao ya kijamii "

" ccm ni chama cha maskini na wanyonge"

Mpaka hapo ushafahamu wanataka nini.
 
Eti kila ck CCM wanasema chama cha masikini mm sitaki kuwa masikini kwahiyo si wezi kushabimia chama hicho hata ukikaa na mjinga utajifunza ujinga ukikaa na mwelevu atakufundisha welevu je ukiaa na masikini utakuwa nani?
 
Iko wazi when we talk about umasikini huwezi kuexclude ccm,actually umasikini ni subset ya ccm
 
Back
Top Bottom