Pole Frank, mchumba hasomeshwi

Pole Frank, mchumba hasomeshwi

Safi sana alitakiwa kusomesha ndugu zake sio mtu aliye kutana nae ukubwani!

Mtu anasomesha akitegemea alipwe fadhila ya kupendwa huko ni kujidanganya...!
Ukiamua kumsomesha mtu ni kama kutoa sadaka tuu..!

Umenena kk, m nakumbuka npo zang field ya teaching nkiwa nmekaa na mwl wa pale nlpopangiw mara nkamwona km kaanza kuchanganyikiw yan haamn, kumuulza nn tatzo kadai alkuwa anasomesha mchumba wake chuo cha ualimu na demu kamtosa, aliumia xn. Cku hyo hakufundsha
 
Kama nitamsomesha lazima awe mke rasmi na tayari ana watoto wangu wasiopungua watatu
 
Hakika kupenda kuna shida zake. Usishangae unamhurumia wakati yeye atasamehe na kumwoa kabisa. Ila inasikitisha kwa kweli. Pole zake
 
Wanawake wengi wanaosomeshwa na wanaume kisha kuwatosa wana uoga wa kutumika, na ubinafsi umewajaa ndio maana
 
Mimi simpi pole kama mliotangulia, Ila nakwambia Frank jipange upya. Pesa hutafutwa, mwache huyo bint afanye maisha. Kumbuka watu wa zamani walisema Fimbo ya mbali haiuwi nyoka.
 
mimi nina ushuhuda dhahiri wa mtu wangu wa karibu kamsomesha binti,ingawa huyo binti jamaa alizaa nae. kamsomesha chuo cha Ruaha miaka minne yule dada alikuwa anasoma Sheria, baada chuo kuisha binti akamtamkia hataki kuwa na future na YEye, binafsi niliumia sana hasa nikiwa nakumbuka sucrifice alizokuwa anafanya jamaa juu ya yule mwanamke. i guess Chriss Breezy was right these Ho**es aint LOyal.

Habari wana Jf,

Mwaka 2009 nilisafiri na Rafiki yangu ambaye sasa hivi yupo Mara sec ni mwalimu kwa sasa tulikuwa tukielekea Nansio Ukerewe katika mihangaiko ya kimaisha, nikiwa kwenye meli nilikutana na kijana mmoja ambaye anaitwa Frank, katika kupiga piga story sehemu ambayo mimi nilikuwa naenda na yeye alikua anakwenda pale pale Chuo cha ualimu Murutunguru. Shida yetu kubwa ilikuwa ni kuonana na mkuu wa chuo ili tupate nafasi pale chuoni lakini tulipofika pale tuliambiwa mfumo wa kuingia vyuo vya ualimu kwa sasa umebadilishwa.

Tulirudi makwetu lakini niliendelea kuwasiliana na Frank. Baadae yeye alipata nafasi ya JKT na hatimaye alijiunga na Jeshi la Wananchi (JWTZ) na kupostiwa Songea, mwaka 2013 Frank alinipigia simu wakati huo mimi nikiwa Bukoba, kuwa amepata mchumba ambaye elimu yake ni form 4 anaona bora amtafutie chuo cha ualimu."Akaniambia sina mtu Wizarani atufanyie mishe, nikamwambia sina ila kuna chuo cha ualimu kipo Biharamuro ni kizuri tu ni cha Dini na wanachuo hufanya vizuri.

Kwa sababu yeye yupo mbali Songea mimi nilikuwa Bukoba kipindi kile nikaenda kuchukua form pale Nyamahanga ada yao ni kama mlionimoja au mbili hivi kwa mwaka. Frank akasema ataimudu kijana kajikunja kusomesha mwaka wa kwanza, mwaka wa pili huku akimuhudumia kila kitu, Frank akafunga safari kuwa aende kuhudhulia graduation ya mchumba wake ambayo ilikuwa tarehe 27 May mwaka huu.

Alipofika pale alikuta hali tofauti lakini yule mchumba wake alimwambia ukweli kuwa ana mmba ya miezi miwili ambayo kwa namna yoyote ile isingewezekana kumsakizia Frank. Mimba yenyewe kapewa na mwanachuo mwenzie nimemhurumia sana Frank anatia huruma, jamani hawa wasichana tunaowasomesha tuwe nao makini najua wanawake wapo wengi kama wa huyu mchumba wa Frank.

NDO MAANA WATU UCHUKUA MAAMUZI MAGUMU

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom