Lukundo utafananisha na kila ,ila kumbukumbu mateso yanapozidi Kigoma ,mateso na shida zinapozidi Tanga uvumi huwepo kuwa ni bora wajitenge , au huko kuna Wanyarugusu ndio hamkuoni ,ila hili la Zanzibar ni lazima mulielewe ,sijui kwa nini mnakuwa wabishi ,Jamani kwa vyovyote vile iwavyo hizi ni nchi mbili ,sasa ni lazima pawepo na masikilizano na heshima ,urafiki ndipo unapokomaa na ukizidi urafiki hushinda udugu ,sasa rafiki analalamika ,wewe unajifanya kama husikii au huoni na kila siku zikienda rafiki anaona au anakuona unampuuza na kutokumheshimu sasa mnafikiri rafiki huyo ataendelea tu kuendeleza urafiki ?
Ni lazima tukubaliane katika misingi ya umoja uliosawa kabisa ili urafiki wetu uwe wa damu ,marafiki hawawezi kuwa ndugu hata siku moja ,lakini kinachosemwa urafiki ukiwa mzuri basi hushinda hata wa ndugu ,kama tunavyoona CCM Zanzibar na CCM bara unashinda udugu uliopo kati ya Unguja na Pemba.Ndivyo inavyoonekana kwamba jinsi urafiki ulivyomkubwa wanatoka watu bara kwenda kuwapiga WaPemba ,dogo hiloo ?
Sasa Zanzibar analalamika mbona urafiki wetu una matatizo ,kwamba hata serikali yangu haina njia za kupatia mapato zote umezifunga na kuzibana ,rafiki yangu wewe hutaki niendelee ,ssasa nikianza kutafuta rafiki mwengine pia hutaki ,kuna wema hapo au kuna ubaya uliojificha ? Maana inatokea marafiki wengine wakawa wabaya na japo ni rafiki lakini hataki kukuona mwenzake unapendeza ,mwenzake unavaa ,mwenzake unaneemeka ,siku zote anataka ufikwe na shida ili uende ukamuombe ni urafiki gani huo ?
Pinda anasema mbao zikigawika kuna upande utapata taabu ,sawa nakubaliana nae kuwa kuna upande utapata tabu ,(Sijui alikusudia kuwambia CCM Zanzibar) ,lakini hapa tulipo kuna matatizo yanatokea Pemba ,Pinda anajua ,Kikwete anajua na jamii ya WaTanzania karibuni wote wameshapata habari ,Tuwaulize wao kama wadau na sio wadau bali ni Serikali ya Muungano hivi wamefanya kitu gani ? Serikali ya Kikwete ilipigiwa kura Pemba japo kura moja lakini wapo wananchi ambao walimchagua , sasa matatizo yanayowakuta wananchi wa Pemba kupelekewa majeshi kwa ajili ya kuwapora haki yao ,wanayaonaje ? Au yanawafurahisha ? Ni kitu rahisi kabisa kuonekana mbali ya hayo wanayoyaita kero ,hili ni kubwa zaidi kwa sababu roho za watu zinapotea bure ,kwa ajili ya madaraka ya miaka kumi au mitano.
Sasa kusema Muungano hauna faida sio akina Seifu wala wafuasi wa Karume bali yale ni matakwa ya wananchi ambao manung'uniko yao yamekuwa kero kwa viongozi wa Zanzibar na hawana budi isipokuwa kuyafuata ,ili waonekane ni viongozi wanaojali maisha yao ,ndio tukaona leo hii hata CCM kule wanausema Muungano na kuutilia vizingiti kwa sababu shida zimekuwa hazifichiki tena ,Raisi hana pa kuuweka uso wake ,viongozi wanaona soo , huku mmeshikilia tu Muungano tutaulinda kwa namna yeyote ile ,Mapinduzi tutayalinda kwa hali yeyote ile ,sasa hao wenye Mapinduzi nao wamefikia kusema Muungano ndio kikwazo kinachowanyima wao kupeleka maendeleo Zanzibar ,kuna kubwa zaidi ya hilo ? Mnalinda Muungano wa kina nani ,mnalinda Mapinduzi ya wepi ? Kwa kauli ya viongozi waandamizi wa Zanzibar nyinyi ni waongo hamna mnachokilinda hata kimoja ,ni kujidanganya ,haiwezekani mnachotaka kukilinda na waliomo humo mnamolindwa wakafikia kusema kuwa kuna matatizo.
Mimi sioni kama Mheshimiwa Pinda amekosea katika kuusemea Muungano yupo sawa kabisa ,lakini usawa huo utatizamika kama wangekuwa wanafuatilia hali ya Zanzibar ,serikali ya Muungano ingekuwa mbele katika kuona kuwa serikali ya Zanzibar inaangaliwa na inapewa vipau mbele katika kuendeleza wananchi wake na pale inapokwenda usongo ,Serikali ya Muungano ingekuwa inaingilia kati kwani ndio Serikali kuu ,sasa wananchi wanapigwa risasi ,wanapigwa virungu serikali Kuu inashangilia na kuongeza nguvu ili watu wauliwe na wapigwe zaidi ,Serikali haijaonekana kupeleka majeshi kwa ajili ya kulinda sheria zisivurugwe bali inapekela kuzidisha kupindwa kwa haki , mwanzo ikisemwa ni vikosi vya SMZ lakini sare zinazoonekana kutumika ni za vikosi vya Serikali ya Muungano ,hivi watu wataufahamu vipi Muungano huu kama sio unaoleta matatizo ?
Watu wanapolalamika basi mjue kuwa wameshachoka na matatizo ambayo nyinyi Serikali kuu mnayaelewa fika ni akina nani wanaosababisha ,lakini mnafumbia macho faida yake hata wale mnaowafumbia macho mambo yakiwashinda wanawatupia mzigo Serikali kuu au wanautupa kuwa yanasababishwa na Muungano.
Sasa hii ndio sababu ya kuudharau mwiba au faida ya kumfuga Nunda. Nunda sasa anakuona hata wewe Serikali kuu inafaa kuvunjwa.