Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,172
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amewashangaa viongozi waandamizi wastaafu serikalini na CCM kuacha kuzungumzia malalamiko yao katika vikao halali kabla ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari. Vyama vina mifumo yao ya kuendesha shughuli zao vina maeneo ya kusemea mambo yao na huko ndiko kusaidia chama na kuweka mikakati ya kukiendeleza, alisema Waziri Mkuu alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana.
Alikuwa akijibu swali kuhusu viongozi wa CCM wakiwamo wastaafu, kulumbana na umoja wa vijana wa chama hicho hadharani badala ya kutumia vikao halali vilivyopo. Alisema kutoa madukuduku kwa kutumia magazeti kabla hata ya kukataliwa katika vikao halali vilivyopo, si dhamira nzuri. Kama malalamiko yako uliyatolea katika vikao halali na ukakataliwa kusikilizwa na hivyo ukaamua kutoka na kuyasema nje, hilo halina tatizo. Na hasa viongozi wastaafu. Hawa wana fursa ya ziada, wana uhuru hata wa kumwona Rais na kusema naye, wakitumia uzoefu walionao kumsaidia hata yeye, alisema Pinda.
Aliasa kuwa si picha nzuri kuona kana kwamba viongozi hao wanakataliwa kusikilizwa katika vikao na hivyo kuamua kuyasema hadharani. Msiwe waoga kusema ndani ya vikao halali kwani huko ndiko hasa pa kujenga na si kusemea kwingine huko ndiko kukisaidia chama na kupanga mikakati zaidi ya kukiimarisha, alishauri Pinda.
HabariLeo
hakulia?