Pinda aonya malumbano ndani ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda aonya malumbano ndani ya CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Mar 28, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mtoto wa mkulima asiyekuwa wa mkulima Bro Pinda amevunja ukimnya wa viongozi wa juu wa CCM baada ya kuwaomba wanaolumbana wafuate taratibu za chama...

  Amesema asiyependa kufuata utaratibu huo labda awe anapenda kuonekana katika magazeti na vyombo vingine vya habari.

  Source: Channel Ten News Bulletin
   
 2. escober

  escober JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  the same shit now and again
   
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yeye je anapenda pia?
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Badala ya kunungunika ni vema mh. Pinda akajiuliza ni kwanini watu wameamua kujitokeza hadharani kukemea mambo wanayoamini hayaendi sawa, badala ya kusubiri huo utaratibu uliozoeleka wa vikao? Jibu ni moja, nalo ni kwamba katika siku za hivi karibuni vikao vimekuwa vikitumika kulinda maovu badala ya kushughulikia utatuzi wake. Katika hali hiyo vikao hivyo vimeanza kupoteza umuimu machoni mwa watu wengi, hii ikiwa ni pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi ndani ya CCM yenyewe.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi Pinda na yeye si mjumbe wa hivyo vikao vya chama? Mbona hakuleta malalamiko na mashauri yake kwenye vikao vya chama? au yeye ni exception kwenye hiyo kanuni anayotaka wenzie wafuate?
   
 6. m

  matawi JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Too late Pinda. Inawezekana press conference ya Sumaye Pinda hakuiangalia. Ni wakati wa Kugawa ccm mbili moja iwe ccm asili na nyingineccm- Uccm halafu tuone mpambano
   
 7. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Nchi ya malalamiko. Kila mtu analalama, kuanzia Rais, Waziri Mkuu, Makamba hakuwa anayetoa suluhisho. Sijui kama tutafika
   
 8. only83

  only83 JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Ni lazima kuwe na mgawanyiko wa wazi kati ya CCM ASILI na CCM KAMPUNI(MAFISADI)...................
   
 9. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  namshangaa!!! Anatenda tofauti na yale anayoyataka wenzie watende. Ni wale wale washerekeao ushindi wa mafisadi-mwoga wa kutoa maamuzi pamoja na madaraka makubwa aliyo nayo.
   
 10. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,742
  Trophy Points: 280
  a bunch of whiners!

  that's why opposition (aka Chadema) inawabidi wao waendelee kukemea. kuonya na kutoa mawazo mbadala badala ya kunasa kwenye hii sarakasi ya ulalamishi!
   
 11. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Yeye alimuumbua Magufuli hadharani badala ya kumuita ofisini na kumalizana naye kiofisi?
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MHESHIWA PINDA CHINI YA RADAR YA ALIYEWAHI KUMUAMINI: UWEZO TUNAO

  Eti umesema Mhe Peter Kayanza Mizengo Pinda aka Mtoto wa Mkulima niliyewahi kumpenda na kumuamini ni JAAAAASIRI??? Ni ujasiri gani tena huo, huyu mtoto wa mkulima nisioifahamu mie???

  Nakuambia mimi huyu mtoto wa mkulima siku hizi simuelewi kabisa juu ya lolote lile!! Na kwa kukuthibitishia hilo mwenzenu tayari nimekua nikijihesabia KUMPOTEZA KIPENZI sawa sawa na ninsi nilivyowahi kujihesabia huko nyuma nikiwa sekondari huku nikion CCM ikinilazimisha kumpoteza KIPENZI CHA ROHO YANGU KISIASA MHE AUGUSTINO LYATONGA WA MREMA (the bureaucratic rule arch-rival charismatic leader) na hivi majuzi tena nikalazimishwa KUMPOTEZA KIPENZI MWINGINE JOHN POMBE MAGUFULI kwa kukataliwa kuzingatia sheria mstari kwa mstari kwenye utendaji wake.

  Nakuuliza mwenzangu ni ujasiri gani huo ulioigundua kwa huyu aliyewahi kuwa Mtoto wa Mkulima huko nyuma na sasa hivi kabakia tu kuwa Mtoto wa walima bustani ya mchicha Mto Msimbazi Dar es Salaam??

  Hakika ili niweze kumtendea haki katika kuanza kwangu kumkataa kule kwanza kulitokea azimio nzito sana katika kikao cha kukata na shoka ambapo wahudhuriaji walikua ni akina (1) Uwezo Tunao mwenye Kupenda, (2) Uwezo Tunao akili na fikra pamoja na (3) Uwezo Tunao jicho la walalahoi. Mkutano huu wa zaidi ya wiki ulikua mkali kweli kweli tena wenye futa nikuvute mkubwa mno.

  Lakini labda nianze kwa kuwashukuru sana tena sana ndugu zangu wengine hawa (Uwezo Tunao family) kwa kuafiki mapendekeza ya huyo mjumbe wa pili hapo juu ya kwamba kwanza tufanye utafiti utakaotuelekeza kama kweli bado kuna matumaini yamebakia ndani ya Baba huyu 'Mtoto wa Mkulima' hadi hapa tulipofikia au laa. Katika kutekeleza azima hiyo sote watatu tulichagua kujipa siku 90 kumsoma juu ya kauli zake na kwa kiasi gani zinavyokubaliana na matendo yake katika jamii yetu hii.

  Kiukweli kabisa, japo MATOKEO YA UTAFITI WA UWEZO TUNAO FAMILI NA HATIMA YA MHESHIMIWA PINDA A.K.A MTOTO WA MKULIMA utakamilika hapo Aprili 23, hata hivyo dalili za awali hazimpendelei saaana huyu kipenzi changu ambaye nasikitika kuelekea kumpoza hivi karibuni katika kitabu changu cha Wanasiasa ninaowaamini nchini.

  Hizo dalili za awali zisizompendelea huyu 'rafiki wa roho yangu, mara baada ya kumsogeza kwa karibu zaidi chini ya drubini yangu kwenye maabara binafsi ya siasa nchini (microscope) kumebainika mambo kadhaa wa kadhaa juu yake huyu mwenzetu. Na endapo dlili hizi zenye gizo totoro hazioonekana kupona kitu basi nawahakikishieni kwamba sitochelewa kupendekeza hapa JF na kote nchini kwamba hicho cheo cha heshima cha 'Mtoto wa Mkulima' nacho tukamnyang'anye kabisa kwa kutoitendea haki ipasavyo.

  Kwa mwenzetu, ndugu yetu na Baba yetu wa Taifa Mwalimu Nyerere cheo kile cha heshima toka kwetu wananchi aliendelea kukitumikia hadi dakika ya mwisho aliposema maneno mawili mtatu kwa Mzee Rashidi Simba wa Vita pembeni mwa kitanda chake hospitalini kule Uingereza hivyo hata akaendelea kustahili kubakia nayo hata baada ya safari ya kurudi kwa muumba wake ilipowadia.

  Mapungufu mazito tuliyoyaona ni haya na ni bora akayafanyia kazi kwa haraka kabla hatujafunga faili na kuikabidhisha kwa wapiga kura kumpima nayo zaidi pamoja na kwamba keshaahidi kurudi kupumzika nyumbani mara baada ya utumishi wake kama Waziri Mkuu, Mheshimiwa Pinda ni:

  1. Kiongozi anayeogopa sana LAWAMA:

  Hii tabia imegeuka kuwa jela yake binafsi anayotembea nayo kila mahali kama mfungwa wa hiari. Kwa kukuthibitishia madai yangu haya utagundua kwamba Mhe Pinda siku zote hajawahi kuonyesha OWN INITIATED ACTION BALI NI MZEE WA REACTIONS tu. Nasema akome kukimbizana na upepo kwa mtindo wa zimamoto kwa kila atendalo.

  2. Mtaalam wa Kukasimu Madaraka, Mchovu wa Kufuatilia:

  Delegating power is a very good sign of a leader who has confidence in colleagues and teamwork spirit. Lakini kama huna muda wa kufuatilia ulioyakasimu, wala uwezo wa kuhakikisha kwamba kweli ulioyakasimu yanaleta matunda ya kugusika kwa mikono na kuonekana kwa macho basi mwenzetu ukae ukijua kwamba wengi huku nje wanajiuliza kiti hicho unachokalia unakiachia wazi lini???

  Uthibitisho wa madai yangu; Mzee Pinda alijichagulia kuparamia swala nyeti la Madai ya Katiba nchini na kwa kuelewa kwamba anayo GOODWILL kwetu sie walalahoi tulio wengi basi akaona vema kuchangamkia tenda hiyo.

  Lakini, kwa bahati mbaya sana 'Wa Mkulima ' hajagundua siri kwamba goodwill ni goodwill tu na inayo ukomo wake na kwamba kitendo cha kuuchukua swala la katiba na kujirithisha kuuficha ndani ya mfuko wake wa suruali ya nyloni ni jambo la hatari kuliko angeliacha tu swala hili bila kuahidi kulishughulikia kabisa.

  Katika hili nasema Mhe Pinda usiombe mtu na au kundi la watu waliyokumini pindi wanapogeuka na kukosa imani kwako - mungalie Ndugu yetu Mhe Kikwete na jinsi alivyotuchukulia for granted imani yote kwake na kura zote katika kipindi chake cha kwanza mpaka akafika mahala na kuona kwamba tuliomuamini baada ya kutusaliti basi ni bora akatumie njia ya mkato KUTUIBIA KABISA KARU nadhani lengo likiwa ni kupata SECOND CHANCE kurekebisha mambo lakini ndio hivyo maji ya kunywa yakishamwagika bora ukayapigie tu deki.

  Mheshimiwa Pinda kwa taarifa tu ni kwamba 'Nguvu ya Umma' tunasubiri kwa hamu kuona endapo tena utaipigia danadana swala la Katiba Mpya na Mtume huru za Uchaguzi; Bara na Visiwa hata isipitishwe kwenye bunge hili la mnamo mwezi huu wa April 2011!!!!

  3. Group Thinking

  Mheshimiwa Pinda ni muumini mkubwa wa kanisa au msikiti wa maamuzi ya kikundi kundi hivi. Hili jambo linampa shida sana kwa kuwa kila mara anakosa ORIGINALITY katika msururu wa mambo ya kutekeleza hivyo jambo linapoenda kombo anashindwa kulitafutia lango la pili kwa kuwa he is NOT never married to the original idea either.

  Kwa mtindo huu 'Wa Mkulima' ni kwamba utajikuta siku zote unageuka kuwa MTUMWA WA FIKRA ZA WASHAURI ambao pindi mambo yanapoharibika wao hucheka mtindo wa Jino-Pembe kwa kuwa siri yote wanayo kwamba wewe hauna input yoyote mle na kwamba hata zile perspective mikanganyiko walizokupa washauri mbali mbali wala haukuweza hata kujitengea muda wa peke yako with a BRUTALLY CRITICAL MIND.

  Kama uliwahi kusikia Mheshimiwa Mwl Nyerere, Mkapa, Dr Shein na Dr Magufuli walipata kuheshimika sana ni kule katika wao kujitengea muda usioingiliwa hata na mama watoto pale nyumbani ili AKALIFIKIRIE TAIFA LAKE KWA UDHATI KABISA NA MOYO WA KIZALENDO ili ku-Question, kuomba ufafanuzi zaidi, uthibitisho wa maelezo na hata kule kufanya SUPRISE SELF-FACT FINDING MISSION bila kuwa pompus anda embarrassing to others kama Vijikamati Vya Bunge tunavyovishuhudia hivi leo viki-play both Police and Court roles together on their subordinate line ministries and related institutions whereas the costitution ONLY asks the to Oversee and Advise.

  Wakati bado utafiti wetu juu ya Mtoto-wa-Mkulima na hasa kwa kumpima zaidi atakavyoshugulikia jambo la msingi zaidi kwa taifa (an immediate People-Centred Constitutional Overhaul call) au kuyaacha kwenye mikono ya wachache akina Oliver Mhaiki na Celina Kombani au atawaita wadau wote kuliweka sawa kabla ya kutinga nayo bungeni Aprili, mambo mengine yatakayoendelea kuangaliwa kwake ni pamoja na:

  a. Pinda Leadership style and frame (Theories X and Y tools).

  b. Whether Pinda is already at the Plateaue of his performance or not (Goal-setting & Abraham Maslow's Theory of Needs)

  c. Jibu kama Mhe Pinda ni Innovative, Proactive or not

  ... na mjadala wa Uwezo Tunao family bado unaendelea juu ya kiongozi huyu kabla ya kuingia kwenye kuwachambu with a brutally critical mind mtu yeyote ambaye amewahi kutajwa kutamani kuwa kiongozi wetu ama wa kisiasa au technocrat kinamna fulani hivi.

  Nyote mnakaribishwa kwenye huu mkutano endelevu wenye lengo la kukosoa hadi wale tunaowapenda ndani ya CHADEMA chenyewe ili kila mmoja aweze kupata marejesho jinsi tunavyomuona na mambo gani yafanyike huruka vihunzi kadhaa kuelekea kwenye mafanikio maridhawa kwa Wa-Tanzania tulio wengi.

   
 13. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #13
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Unajua Pinda anapenda kuonekana Goodboy...mnafiki tu.Pinda ni mfano mbaya wa viongozi wa kizazai kilichopo madarakani,yeye ni muumini mkubwa wa siasa za kizandiki za CCM.Kazi anayo
   
 14. Ikimita

  Ikimita JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 302
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hana hoja, ni wa kupuuza.

  Haya malumbano yanayotokea sasa ndani ya CCM hayana tofauti kabisa na masahibu aliyofanyiwa Magufuli. Kulikuwa na sababu gani kwenda kumshtaki Magufuli kwa wananchi, tena nyumbani mbele ya wapiga kura wake na wizarani kwa wale anaowaongoza. Ninaamini kwa dhati kabisa shambulizi ambalo Pinda na JK walimfanyia Magufuli wangeweza kulimaliza ndani ya vikao vya Baraza la Mawaziri. Sasa kama vikao vya Baraza la Mawaziri haviwezi kutumika kuonyana au kubadili mienendo ya utendaji, huko huwa wanajadili vitu gani??

  Kwa ufupi ni kwamba chama kimeparaganyika na serikali yake pia imeparaganyika. Malumbano ya sasa ni harakati mahsusi kwa pande zinazosigana kukomoana.

  Nyani haoni kundule, Pinda aangalie kibanzi ndani ya jicho lake mwenyewe kwanza kabla ya kuwaangalia wenzake.
   
 15. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  hivi yeye anavyoonekana hataki hii kitu ya 2015 kweli?? maana simuamini mtu yeyote sasa hivi.
   
 16. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Na nadhani angeuachia uongozi wa juu wa chama ndio uzungumzie! Wapi msekwa?
   
 17. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Mbona nawe Pinda unafanya hivyo hivyo? kwa nini msiitishe kikao cha dharura mka tatua matizo yenu.

  Au ndio spinning ingine baada ya Loliondo ya kunyamazisha wadanganyika kuhusu mambo muhimu ya Dowans na hali ngumu ya maisha?
   
 18. c

  chama JF-Expert Member

  #18
  Mar 29, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mh. Pinda anapaswa kuwa muwazi na mkweli hizi siasa za kinafiki hazimsaidii lolote, yeye kama waziri mkuu anafahamu chanzo cha malumbano na mipasuko ndani ya CCM, anaposema wanaolumbana wafuate taratibu za chama anaamanisha nini? chama kimepoteza dira, demokrasia hakuna kilichobaki ni uhuni na ubabe, kama anataka kuwa mkweli amshauri mwenyekiti wake azipe mipasuko ili hadhi ya chama irudi, vinginevyo malumbano yataendelea siku zote, wote tunajua Rais amesimamia kundi gani utakuwa ni unafiki mkubwa kama yeye Pinda atajifanya hana kundi kwenye malumbano haya ushauri wangu wa bure mheshimiwa Pinda angalia utendaji wa kazi wa mawaziri wako ili waondoe kero za maisha zinazowakabili watanzania hizi siasa za CCM mwachie Luteni Makamba na wahuni wenzake.
   
 19. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #19
  Mar 29, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amewashangaa viongozi waandamizi wastaafu serikalini na CCM kuacha kuzungumzia malalamiko yao katika vikao halali kabla ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari. “Vyama vina mifumo yao ya kuendesha shughuli zao … vina maeneo ya kusemea mambo yao na huko ndiko kusaidia chama na kuweka mikakati ya kukiendeleza,” alisema Waziri Mkuu alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana.

  Alikuwa akijibu swali kuhusu viongozi wa CCM wakiwamo wastaafu, kulumbana na umoja wa vijana wa chama hicho hadharani badala ya kutumia vikao halali vilivyopo. Alisema kutoa madukuduku kwa kutumia magazeti kabla hata ya kukataliwa katika vikao halali vilivyopo, si dhamira nzuri. “Kama malalamiko yako uliyatolea katika vikao halali na ukakataliwa kusikilizwa na hivyo ukaamua kutoka na kuyasema nje, hilo halina tatizo. “Na hasa viongozi wastaafu. Hawa wana fursa ya ziada, wana uhuru hata wa kumwona Rais na kusema naye, wakitumia uzoefu walionao kumsaidia hata yeye,” alisema Pinda.

  Aliasa kuwa si picha nzuri kuona kana kwamba viongozi hao wanakataliwa kusikilizwa katika vikao na hivyo kuamua kuyasema hadharani. ”Msiwe waoga kusema ndani ya vikao halali kwani huko ndiko hasa pa kujenga na si kusemea kwingine … huko ndiko kukisaidia chama na kupanga mikakati zaidi ya kukiimarisha,” alishauri Pinda.

  HabariLeo
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Mar 29, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,806
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  Msanii mwingine huyu mbona hajashangaa kauli zake nyingi zilizojaa utata ikiwemo, "Mafisadi wa EPA ni matajiri wakubwa sana nchini kama watakamatwa basi nchi itawaka moto."
   
Loading...