Pinda afuta amri ya Waziri Magufuli

attachment.php

Hali kama hii inatisha pengine hawa wakandarasi ni sawa na wale waliojenga Barabara ya Kurasini to Mbagala... 10% zitatuua... Magufuli hatofua dafu akizibia mrango huu mingine inafunguka... Pinda ndie wakujiuzulu... Bwai bwai tu
 
makufuli kesha piga hela kwa makandarasi. na kwenda kujenga kijiji kwao Lubambangwe. kama kutuchuna tuchuneni kizungu bana
 
Makufuli mwizi tu. alijua barabara hazitadumu ndipo akajifanya kusimamia sheria. aibu yake hiyo
 
Usimamizi wa sheria kwetu ni msamiati, ndo maana nchi zilizoendelea ziliendelea kwa vile sheria zinafanyiwa kazi hapa bongo ukitaka tu kuenforce sheria yanaanza:

1. Muwe na nyuso za huruma

2. Hili linazungumuzika tutalifanyia kazi

3. Ukerewe ni kisiwa inabidi sheria hapa ipindishwe ili Ukerewe isiwe na upana kama sehemu zingine - je England pia hufanya hivyo kwa vile nacho ni kisiwa?

4. Waacheni wazidishe mizigo aka overloading, tuvunje sheria - tutaunda tume

5. ETC

Unategemea nini kwa nchi changa kama hii, ndo maana Ulaya na kwingineko kulikoendelea watu waliumia kwanza wakaelewa maana ya sheria ni nini - leo hii tunaenda kutalii maendeleo yao wakati wao wakija kutalii umasikini wetu.
 
Pinda nadhani hakufaa kuwa waziri mkuu ila kwavile tunaye basi tunaendelea kuumia kwa maamuzi yake hadi 2015. Barabara hizi zinaharibiwa kweli mimi nimepata kuendesha gari mara kwa mara eneo hili la RUVU hadi CHALINZE usipokaa vizuri ni rahisi sana kupindua gari ndogo uwe makini unapokanyaga hiyo migongo iliyowekwa na magari makubwa yanayozidisha mizigo kwa ruhusa ya waziri mkuu Pinda....shame on him
 
Tatizo ni zaidi ya overloading. Tatizo ni viwango vya barabara zetu. Ujenzi wa Highways ni tofauti na ujenzi wa barabara za mitaani ambazo zina viwango vya magazi yasiyo zidi tani 5-10. La msingi hapa ni kuhakikisha wakandarasi wanachaguliwa wenye viwango vya hali ya juu katika ujenzi wa barabara zetu. lakini pia, wanainchi tuko wapi? iweje tukubari kupewa barabara chini ya kiwango? Na huyo waziri au mwakirishi wake anapokwenda kufanya ufunguzi wa hizo barabara, huwa wanajua wanachokubali kukipokea? Ndugu wa Tanzania wenzangu. Tufike maali tutambue kuwa, pesa inayoutumika katika ujenzi wa barabara hizi ni zetu walipa kodi. Basi, kama haturiziki na viwango, tusikubali hizi barabara zifunguliwe na sisi tukiangalia tuu. WATANZANI TUACHE KUONGEA BILA VITENDO. TUACHE KULALAMIKA WAKATI KATIBA INATUPA HAKI YA KUFANYA CITIZEN ARREST...
 
Tatizo ni zaidi ya overloading. Tatizo ni viwango vya barabara zetu. Ujenzi wa Highways ni tofauti na ujenzi wa barabara za mitaani ambazo zina viwango vya magazi yasiyo zidi tani 5-10. La msingi hapa ni kuhakikisha wakandarasi wanachaguliwa wenye viwango vya hali ya juu katika ujenzi wa barabara zetu. lakini pia, wanainchi tuko wapi? iweje tukubari kupewa barabara chini ya kiwango? Na huyo waziri au mwakirishi wake anapokwenda kufanya ufunguzi wa hizo barabara, huwa wanajua wanachokubali kukipokea? Ndugu wa Tanzania wenzangu. Tufike maali tutambue kuwa, pesa inayoutumika katika ujenzi wa barabara hizi ni zetu walipa kodi. Basi, kama haturiziki na viwango, tusikubali hizi barabara zifunguliwe na sisi tukiangalia tuu. WATANZANI TUACHE KUONGEA BILA VITENDO. TUACHE KULALAMIKA WAKATI KATIBA INATUPA HAKI YA KUFANYA CITIZEN ARREST...

Mimi ni Mhandisi (Engineer) naomba niwaeleweshe nini kinaendelea ktk barabara zetu tunazozijenga kwa gharama kubwa:

1. Barabara ina design yake ya kuhimili mzigo (pavement design)hivyo basi uzito wa magari hutakiwa kuzingatia uwezo wa barabar yenyewe ndo maana kukawa na mizani

2. Ujenzi wa barabara zetu hufuata maanadalizi, maadili na taratibu zote za kihandisi, ndiyo maan utaona barabara ikishakamilika kujengwa huwekwa katika kipindi cha uangalizi/matizamio kisichopongua miaka miwili, ikitokea barabara ikaharibika basi mhandisi mshauri na mkandarasi watawajibika kurudia ujenzi wa barabara husika kwa gharama zao, mfano ni ile barabara ya Kilwa. Hivyo ni vigumu sana kujenga baraba chini ya kiwango.

3.Nchi zilizoendelea hujenga barabara zake na tena zenye ubora kuliko zetu (Asphalt Concrete) ni tabaka la lami zuri kabisa. Katika barabara zao uzito ni mdogo ukilinganisha na sisi, mfano Marekani ni tani 36.2, Uingereza tani 40, Ujerumani tani 40, Ufarasa tani 40, Urusi tani 38, lakini kwa Tanzania ni tani 56 ambacho ni kiwango kikubwa sana.

4. Kuna utafiti umefanyika hapa Tanzania na umeweka wazi kuwa barabara zetu zinaharibiwa na wafanya biashara wasioitakia mema nchi kwa kuwa wanatumia tairi zijulikanazo " Super Single Tires" ambazo ni adui mkubwa sana kwa uharibifu wa barabara, simple physics, Pressure between two surfaces "the smaller the area the greater the pressure" malori mengi sana wa hao wafanyabiashara yana hizo tairi na bado yanazidisha uzito wewe unategemea nini kwa barabara iliyojengwa kuhimili Dual Tires (Tairi mbili kwa pamoja). Hapo barabar zitatoboka na ndicho hicho mnachokishuhudia ktk picha, na bado yatatokea madhara makubwa kuliko unavyoona kama serikali itaendelea kuwakikingia kifua wafanyabiashara waroho kuzidisha uzito.

5. Hitimisho, Serikali itafakari upya kuzuia kuwadhibiti wasafirishaji (Transporters) kwa kutumia sheria namba 30 ya mwaka 1973 ya usalama barabarani. La sivyo barabara tunazozijenga si lolote zitakwisha harahaka sana na wala tusisingizie eti zimejengwa kwa viwango duni- never!!!
 
Usimamizi wa sheri Tanzania ni msamiati, Dr.Magugfuli alijaribu kusimamia sheria kuhusu kuzidisha uzito akashambuliwa sasa tizama barabara zinanvyotoboka..


Dr.Magufuli kiboko:

Dr Magufuli ni mwadilifu, hupangua hoja kwa mifano na live data, na pia ni mfuatiliaji wa mambo. Pia hana jazba ya kugombeza watu hadharani. Tukitaka TZ isonge mbele kote kote, DR MAGUFULI ni mtu sahihi kwa sasa.

Wananchi wa leo wanataka zaidi kuona miradi ya serikali ikikamilika kwa wakati na pia kua na value for maney (VfM). Magufuli alipokuwa Ujenzi, ardhi, Uvuvi na Mifugo, amefanya kazi zinazoonekana.

Dr Magufuli, ni kati ya mwaziri watakao irudisha CCM 2015 bila kuweka mabango kama mwaka 2010, la sivyo bajeti ya Mabngo ya kampeni 2015 itaongezeka mara nyingi zaidi mwaka 2015.

Dr Magufuli sii mchezo, Jamaa anafuatilia barabara, ujenzi umefikia wapi, ameziweka kichwani, anatoa tathmini zitaisha lini, wakandarasi wazembe wanapigwa chini, kule wizara ya vitoeo - Samaki alikua anadeal nao mpaka watu wakazika nyavu haramu wakaweka na misalaba ukidhani marehemu kumbe nyavu za kuvulia samaki. Alishawahi kukamata magari mengi ya serikali yanayofanya shuguli binafsi, anapangua hoja kwa hoja.

Dr Magufuli kiboko ya wakurugenzi na watendaji wengine wazembe

Dr. Magufuli, alipopewa wizara ya Ardhi, palianza kuwa pasafi, sasa sijui aligusa maslahi ya wakubwa hakuchukua muda pale akapelekwa Mifugo na Uvuvi, nako huko akafanya mambo, meli ilikamatwa hana utani na haina maana zilikua haziibi samaki ila waliokuwepo walikua hawafuatilii
 
Nadhani hapo point ni kuwa je waziri mkuu alisema kuwa magari yapite hata yale yenye uzito mkubwa? Hapo swali halikujibiwa, kama waziri mkuu alimpinga magufuli basi alikosea kwa sababu magufuli anatetea barabara zetu zisiharibike. Nilichoona hapo ni kuwa waziri mkuu amejitetea kuwa hakupishana maneno na magufuli lakini hakueleza alimpa maagizo gani. Nimeona swali limekwepwa na waziri mkuu.....anachosema ni kuwa kuna athari kubwa kama bidhaa hazitasafirishwa. kama alisema hivyo bila kuangalia uharibifu wa barabara zetu basi waziri mkuu amekosea.
 
Hahahaa, kweli kilim, nadhani baada ya kuruhusu hilo, hata magari yaliyokuwa yamezidisha uzito yalipita. Na ni lazima tukubali, ilimvunja nguvu waziri Magufuri (tunaomba usivunjike moyo minister jembe), maana ona hali ilivyo kwenye barabara hiyo leo, kwa muda mfupi inatisha kuliko. Ni hasara kwa taifa pia, maana zinaongeza ajali nyingi, kuua na kupoteza nguvu kazi ya taifa na mali pia. Waziri Magufuli aachwe afanye kazi kutetea maslahi ya nchi hii kwakuwa hainuki na kujifanyia mambo yake kivyake, bali anafuata taratibu kanuni na sheria zilizotungwa na bunge letu wenyewe!Sijui, lakini nionavyo mimi nivizuri wakati mwingine kukubali maumivu kidogo ya muda mfupi kwa faida itakayo patikana muda mrefu baadaye.
 
Kama pale mitaa ya mbezi mwisho, kwa jinsi kulivyoumuka ukiwa lena kama mimi unaweza kujikuta unahama upande na kuhamia kwingine.

Sehemu nyingine baada ya kupita ruvu
 
Akiwa Waziri wa Ujenzi na Miundombinu Wizara inayosimamia weighbridges kuna kipindi kulitokea ukiukwaji mkubwa wa upitishaji mizigo mizito inayoua barabara zetu.

Watumishi wa mizani walisimama kidete na Waziri wao Dr Magufulu lakini wasafirishaji wakamzunguka wakaenda kwa Prime Minister Mizengo Pinda akatengua amri ile na kuruhusu malori yaendelee kutimba barabara.

Sijui anakumbuka?

Sijui akipata nafasi hii ataacha yaendelee kutamba kwa amri ya Pinda?
 
Nakumbuka huyu jamaa maamuzi yake mengi yalitenguliwa na PM wake (Pinda), ni kama alkwa speed gavana yake. Sasa kama yeye ndiyo atakuwa kinara sijui itakuwaje. Ila akitaka apite kirahisi, atangaze kurudisha nyumba za serikali ili ionekane haikuwa ridhaa yake, la sivyo tutamuhoji sana kuhusu hili jambo.
 
Nakumbuka huyu jamaa maamuzi yake mengi yalitenguliwa na PM wake (Pinda), ni kama alkwa speed gavana yake. Sasa kama yeye ndiyo atakuwa kinara sijui itakuwaje. Ila akitaka apite kirahisi, atangaze kurudisha nyumba za serikali ili ionekane haikuwa ridhaa yake, la sivyo tutamuhoji sana kuhusu hili jambo.

Ukimuorodheshea madhaifu kwenye maamuzi ni mengi sana ila hilo ulilolitaja Lyimo ndio kubwa lao

Hata kama nyumba zilichakaa je na viwanja vilichakaa???

Mbona wanajenga nyumba mpya kila siku??

Mbona wanapangishia viongozi mahoteli kila siku??

Hatutamuelewa kamwe!

Kama haukuwa uamuzi wake na hakubaliana nao mbona hakuupinga ama kujiuzulu??

Ule ni uporaji..nyumba ni zetu wote wakulima,wafanyabiashara,watumishi wa umma nk
 
Last edited by a moderator:
Jana nilimuonea huruma sana Pinda! Alikuwa kama mtu aliyemwagiwa maji ya baridi pale mbele. Hata kusoma ile report ya serikali ni kama alikuwa amelazimishwa.

Kweli Kikwete hatabiriki, hivi unawezaje ukakata jina la PM wako? hata kwenye tano bora asiingie. Hili limeweka rekodi katika nchi yetu, haijawahi kutokea.

Tuliona Mwinyi alimpitisha PM wake John Malecela 1995. Mkapa alimpitisha PM wake Sumaye 2005. Lakini mwanaume Kikwete amewakata ma-PM wake wote aliofanya kazi nao i.e Lowassa na Pinda.
 
Jana nilimuonea huruma sana Pinda! Alikuwa kama mtu aliyemwagiwa maji ya baridi pale mbele. Hata kusoma ile report ya serikali ni kama alikuwa amelazimishwa.

Kweli Kikwete hatabiriki, hivi unawezaje ukakata jina la PM wako? hata kwenye tano bora asiingie. Hili limeweka rekodi katika nchi yetu, haijawahi kutokea.

Tuliona Mwinyi alimpitisha PM wake John Malecela 1995. Mkapa alimpitisha PM wake Sumaye 2005. Lakini mwanaume Kikwete amewakata ma-PM wake wote aliofanya kazi nao i.e Lowassa na Pinda.

Ukiambiwa Jk ndo mfanya maamuzi magumu utabisha?😀
 
Back
Top Bottom