Ujenzi daraja la Mbutu waokoa bil.18/-
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amesema serikali imeokoa sh bilioni 18 kwa kutumia makandarasi wa kizalendo kujenga Daraja la Mbutu.
Magufuli alitoa kauli hiyo wilayani Igunga, Tabora, akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo.
Alisema ujenzi wa daraja hilo umegharimu sh bilioni 12 badala ya sh bilioni 30 endapo lingejengwa na makandarasi wa nje.
Daraja la Mbutu pamoja na tuta la barabara lenye urefu wa kilometa tatu linajengwa na muungano wa makandarasi wa kizalendo 13 unaojulikana kama Mbutu Bridge Joint Venture chini ya usimamizi wa muungano wa wahandisi washauri wawili unaojulikana kama PIDAEL Joint Venture.
Mkataba wa ujenzi wa daraja hilo ulisainiwa Aprili mwaka jana na umepangwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Nimeridhishwa na kasi ya ujenzi wa daraja hili na nimeona tayari mmefikia karibu asilimia 80.
Hii ni kazi nzuri inayostahili kupongezwa kwani mmeanza kudhihirisha uwezo wenu kama makandarasi wazalendo, alisema Magufuli na kuwataka kukamilisha mradi huo kwa muda na viwango vilivyopangwa.
Magufuli pia amewataka wananchi wa maeneo hayo kuhakikisha wanalitumia daraja hilo vizuri kwani hiyo ni fursa nyingine ya kuwaletea maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu, alimshukuru Waziri Magufuli na kwamba mambo aliyojionea na kutoa maelekezo yatasaidia kukamilika kwa daraja hilo kwa wakati.
Source:Tanzania Daima Jumatatu, 21,October 2013