Pinda afunguka sakata la Escrow

Pinda afunguka sakata la Escrow

pindahasira_300_182.jpg

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema taarifa nyingi za mjadala wa akaunti ya Escrow iliyofunguliwa kutokana na mgogoro wa malipo ya gharama za umeme kati ya kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) ambao unaendelea bungeni, umeongezwa chumvi na wakati ukifika Watanzania watatolewa taarifa kamili.

Kauli hiyo ya Pinda aliitoa kanisa kuu la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika wakati wa kumsimika Dk Jackson Chilongani kuwa Askofu wa Sita wa dayosisi hiyo.

Awali, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini, Jacob Chimeledya aliitaka Serikali kutoa taarifa juu ya akaunti ya Escrow ili wananchi wajue kilichotokea ili ijulikane ukweli upi na uvumi upi kwani iko hatari ya kutengeneza taifa lenye kuamini uvumi.

Dk Chimeledya alisema Watanzania sasa wanaishi kwenye hali ya sintofahamu kwani hawajui yupi anasema ukweli na yupi ni `mzushi’. Alisema ni lazima Serikali itoe maelezo kwa wananchi juu ya kashfa hiyo ili wajue kilichotokea kwani ipo hatari ya kutengeneza taifa linaloishi kwa kuamini uvumi.

“Hatutakiwi kuishi kwenye taifa linaloamini uvumi… taifa halitapiga hatua kwa taarifa za kusikia tu bila kujua ukweli uko wapi, nini kimetokea na hatua gani imechukuliwa,” alisema.

Pia Askofu Chimeledya alitumia fursa hizo kuuzungumzia mchakato wa Katiba iliyopendekezwa na Bunge, akiitaka Serikali kutoa elimu kwa wananchi kabla ya kupiga kura ya maoni Aprili mwaka kesho.

Alisema wananchi waachiwe waamue baada ya kuisoma katiba hiyo na si kuwafuata wanasiasa ambao wamekuwa na milengo tofauti kutokana na wengine kushawishi wananchi kupiga kura ya ndio huku kundi lingine likitaka Katiba hiyo kupigiwa kura ya hapana.

Alisema kama Serikali haitasimama imara kusimamia mchakato huo, basi utatekwa na watu wenye nia mbaya.

“Makundi yote yakae kimya Katiba hii ni ya wananchi, waachiwe waamue na si kuwasemea watu wapige kura ya ndio au hapana.

Askofu huyo aliwataka viongozi wa kanisa hilo kuongoza vizuri kwani ni aibu kwa Mkristo au kiongozi wa kanisa kuharibu kanisa, kinachotakiwa kila mmoja kuchukua nafasi yake kuongoza kanisa vyema.

Akitoa salamu za Serikali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema kuhusiana na kashfa ya Escrow na IPTL alisema taarifa nyingi zimeongezwa chumvi. Hata hivyo hakutaka kuingia kwa undani kuzungumzia suala hilo, huku akisisitiza kuwa, wakati ukifika Serikali itatoa maelezo ya kina na kuwafanya Watanzania wapate ukweli.

Sakata la madai ya kuchotwa kwa fedha katika akaunti ya Escrow ndilo linalotawala kwa sasa nchini, hasa baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Swerikali (CAG) kuwasilishwa bungeni, na sasa ikitarajiwa kujadiliwa bungeni kwa siku mbili kuanzia keshokutwa. Akizungumzia Katiba Inayopendekezwa, alisema Serikali itatoa nakala za kutosha za katiba hiyo ili wananchi wengi wasome na kupata fursa ya kutoa maoni yao.

Aidha, alisema Kanisa la Anglikana nchini limetoa mchango mkubwa katika kuendeleza huduma za jamii kwa kujenga shule, hospitali, vituo vya afya na miradi mingine ya kijamii. Pia aliutaka uongozi wa kanisa hilo kuibua fursa za miradi ya maendeleo ili kusaidia familia masikini kuwa na miradi midogo ikiwemo ya ufugaji kuku.

Kwa upande wake, Dk Chilongani aliahidi kuboresha elimu na huduma za jamii na kusimamia kikamilifu vitenga uchumi vya kanisa hilo.

“Sikuota kuwa askofu ni neema ya Mungu,” alisema.

Chanzo :Habari leo


Chumvi gani huyu naye?! kazi kuhangaika kulinda wezi; apigwe huyu!
 
Kakimbilia chachi? Kweli simba akizidiwa hunywa hata supu ya kabeji.

Mbona ushabiki umekuwa mwingi katika sakata la Escrow?tuache siasa tujadili ukweli wa sakata hili kwa hoja zilizojitosheleza kuliko kuwa makuwadi wa kuwatetea wanasiasa fulani na kuwaponda wanasiasa fulani kwasababu ya masilahi binafsi mmeweka utaifa nyuma ubinafsi mbele.
 
Conference ameitoa wapi wakati alikua anahaha bungeni kutaka kuchomeka court order ili binge lisijadili, hapa ndipo utakapo on a wabunge was ccm hawana maana. Wawekwa kiti moto na 100ml kwa kila mmoja zinatosha kabisa kujadili pumba hiyo kesho kutwa.

Labda Esther Bulaya huyu mdada namuamini yy hatokuwepo atapata uzuru kama kwenye baraza la katiba
 
Wee kondooo.....

Unajua PER DAY IPTL INALIPWA TSHS. NGAPI...!!?? HADI MGOGORO UNATOKEA KUWA NI PESA NYINGI SANA...!!??


PER DAY...Tanesco pays IPTL tshs 400 mil.....


Hii ni sawa na tsh 12 bilions....kwa mwezi.....!!!!!


Hiyo ni CAPACITY CHARGE tshs 4 bil plus tshs 8 bil gharama za umeme, ndio UGOMVI ULIKOTOKEA...KUWA IPTL INAUZIA TANESCO UMEME GHALI SANAAAAAAA....


BAADA YA KESI KUISHA NA AUDITING KUFANYWA....IKAONEKANA KTK ZILE FEDHA ZA ESCROW AMBAZO ZILIFIKIA US$ 250 MIL ilitakiwa 75% ZIRUDI TANESCO....kuwa tanesco ililipa ZAIDI....

250,000,000 × 1720 = tsh 430 billions...


So 75% × 425 = tshs 322 bilions ZIRUDI TANESCO

Alafu 25% zilizobakia ziende IPTL...na umeme uuzwe tshs 80 kwa unit moja


Sasa ww kima, tanesco ni mali ya UMMA, badala ya hizo kurudi tanesco ZIMELIWA....


PINDA NDIE WAZIRI MKUU....alipewa mgawo wake...na ni mtuhumiwa namba moja...aliona watu wakigawiwa fedha yeye akijua na kapokea pia....


Ukirejea kikao cha NEC CCM Dodoma, Mangula alisema waziii kuna ATM mpya ya ECSROW...wana CCM...yaani UVCCM wanagawiwa hela kama njugu...akimtaja wazi Pinda....hivyo hata Mangula anajua Pinda kapewa hongo hiyo....


Sasa ww una mtindio wa ubongo ww....!!!

Where is ur intellectual skills on this matter...!!? Usomi upi unataka kujadili...!!?


Kuhusu Lowassa hakuhusika ktk Richmond...jua vitu kwa undani ww...!!




Ebu tujadiri hii hoja kisomi tuache ushabiki wa kisiasa,naoma utuambie ni kwa namna gani Mizengo Pinda anahusika na uwizi huo?manake tukikumbuka kwenye sakata la Richmond ripoti ya Mwakyembe ilidadavua vizuri kwa ushahidi uliojitosheleza namna Bw. Edward Lowassa alivyohusika kukwapua fedha za umma bila huruma zaidi shilingi mil.152 kwa siku iwe umeme umezalishwa au haujazalishwa kwenda kwenye gridi ya Taifa.Ebu piga mahesabu kwa mwaka ingekuwaje na je ingekuwa miaka mitano ingekuwaje pia? Edward Lowassa na mafisadi wenzake wangeweza kukwapua kiasi gani cha fedha kama mkataba usingesitishwa baada ya ripoti ya Mwakyembe kuibua uwizi huo.Hiyo ni moja ya mikataba mibovu ya kinyonyaji aliotuingiza Edward Lowassa muda mfupi baada ya kuteuliwa kuwa waziri mkuu.Huyo ndiyo Edward Lowassa kamwe huwezi kumfananisha na Mizengo Pinda katika uaminifu wao,uadilifu wao na weledi wao katika utekelezaji wa majukumu ya serikali.
 
Makanisa sasa yanatia kinyaa kusafisha Majizi... hapo ndo amefunguka? Ukanjanja katika uandishi sasa yanafikia kilele cha ujinga...

Acha kukashifu imani za watu kwa sababu ya udini wako,changia mada kwa hoja zenye mashiko kama huna hoja kaa kimya si lazima uchangie kila mada
 
Naona makanisa yamegeuka kuwa vijiwe vya siasa. Hivi hawa viongozi wa dini hawayaoni haya?
 
MAFISI wakubwa! kila jitu likaharibu linaenda kukunja makunyanzi kanisani au msikitini. viongozi wa kanisa wanaowaruhusu hawa WEZI kulinajisi kanisa walaaniwe na kila mwananchi anayeitakia mema nchi hii.
 
Unatumika kinyume na maumbile....ushapasuka msamba ww...!!! Useless...!!

Mtaangaika sana mwaka huu huyo babu yenu Edward Lowassa ni mgonjwa anatetemeka mwenyewe hata kushika glass hawezi,hata kuinua mikono juu hawezi mikono imekakamaa kwa ugonjwa ,aoni vizuri ni kama kipofu kila kukicha ujerumani kutengeneza macho na kubadilisha damu ni mdhaifu hata kusimama muda mrefu hawezi uwezo wake wa kufikiri umepungua sana ndiyo maana muda mwingi akiwa bungeni anasinzia.Ni mgonjwa na mdhaifu sana kwa kweli kamwe hawezi kwa amirijeshi mkuu wa JMT atafia madarakani
 
apo nimemtetea nani vile? Nkumbushe...

Mbona ushabiki umekuwa mwingi katika sakata la Escrow?tuache siasa tujadili ukweli wa sakata hili kwa hoja zilizojitosheleza kuliko kuwa makuwadi wa kuwatetea wanasiasa fulani na kuwaponda wanasiasa fulani kwasababu ya masilahi binafsi mmeweka utaifa nyuma ubinafsi mbele.
 
Sipendi kuona hawa maaskofu wanawaalika mafisadi...nachukia sana
 
Watanzanzia sasa inabd tuwe macho yawezekana kuna baadhi yao ni mafisadi
 
Ukiulizwa swali umtaje mtu walau mmoja tu aliye msafi ndani ya CCM - aisee ni bora mtu akwambie ukabebe zege.
 
Kwani uyo askofu yeye hajui kuwa kuna tume ya PAC na hajui kama umeshapangwa muda na siku ya kuliweka wazi jambo hilo kule bungeni? Kama hiyo serikali ndio mtuhumiwa then anataka mtuhumiwa atoe taarifa ya wizi?? Mbona naona kama uyo askofu haikua sahihi kutokana na mazingira ya uo wizi eti uiambie serikali itoe tamko serikal yenyewe ni akina pinda
 
MAFISI wakubwa! kila jitu likaharibu linaenda kukunja makunyanzi kanisani au msikitini. viongozi wa kanisa wanaowaruhusu hawa WEZI kulinajisi kanisa walaaniwe na kila mwananchi anayeitakia mema nchi hii.

Mkuu ujanja huo ni wa Edward Lowassa wa kupita makanisani na misikitini kujisafisha ili aonekane mwema kwa jamii ya watanzania wakati yeye ni fisadi aliyebobea tokea enzi za utawala wa Mwl.Nyerere alifanya ufisadi mwingi tu moja wapo ikiwa kutafuna pesa za ujenzi wa ofisi za TANU kwa mkoa wa Arusha aliadhibiwa na chama kwa kuambiwa arudishe pesa zote na kufika ofisi kila siku kuanzia asubuhi mpaka jioni bila kufanya kazi yoyote baada muda mrefu Sokoine alimwombea msamaha kwa mzee hapo akasamehewa baada ya kutumia adhabu hiyo na kupangiwa majukumu mengine.
 
Back
Top Bottom