Pinda afunguka sakata la Escrow

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,162
2,000

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema taarifa nyingi za mjadala wa akaunti ya Escrow iliyofunguliwa kutokana na mgogoro wa malipo ya gharama za umeme kati ya kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) ambao unaendelea bungeni, umeongezwa chumvi na wakati ukifika Watanzania watatolewa taarifa kamili.

Kauli hiyo ya Pinda aliitoa kanisa kuu la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika wakati wa kumsimika Dk Jackson Chilongani kuwa Askofu wa Sita wa dayosisi hiyo.

Awali, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini, Jacob Chimeledya aliitaka Serikali kutoa taarifa juu ya akaunti ya Escrow ili wananchi wajue kilichotokea ili ijulikane ukweli upi na uvumi upi kwani iko hatari ya kutengeneza taifa lenye kuamini uvumi.

Dk Chimeledya alisema Watanzania sasa wanaishi kwenye hali ya sintofahamu kwani hawajui yupi anasema ukweli na yupi ni `mzushi’. Alisema ni lazima Serikali itoe maelezo kwa wananchi juu ya kashfa hiyo ili wajue kilichotokea kwani ipo hatari ya kutengeneza taifa linaloishi kwa kuamini uvumi.

“Hatutakiwi kuishi kwenye taifa linaloamini uvumi… taifa halitapiga hatua kwa taarifa za kusikia tu bila kujua ukweli uko wapi, nini kimetokea na hatua gani imechukuliwa,” alisema.

Pia Askofu Chimeledya alitumia fursa hizo kuuzungumzia mchakato wa Katiba iliyopendekezwa na Bunge, akiitaka Serikali kutoa elimu kwa wananchi kabla ya kupiga kura ya maoni Aprili mwaka kesho.

Alisema wananchi waachiwe waamue baada ya kuisoma katiba hiyo na si kuwafuata wanasiasa ambao wamekuwa na milengo tofauti kutokana na wengine kushawishi wananchi kupiga kura ya ndio huku kundi lingine likitaka Katiba hiyo kupigiwa kura ya hapana.

Alisema kama Serikali haitasimama imara kusimamia mchakato huo, basi utatekwa na watu wenye nia mbaya.

“Makundi yote yakae kimya Katiba hii ni ya wananchi, waachiwe waamue na si kuwasemea watu wapige kura ya ndio au hapana.

Askofu huyo aliwataka viongozi wa kanisa hilo kuongoza vizuri kwani ni aibu kwa Mkristo au kiongozi wa kanisa kuharibu kanisa, kinachotakiwa kila mmoja kuchukua nafasi yake kuongoza kanisa vyema.

Akitoa salamu za Serikali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema kuhusiana na kashfa ya Escrow na IPTL alisema taarifa nyingi zimeongezwa chumvi. Hata hivyo hakutaka kuingia kwa undani kuzungumzia suala hilo, huku akisisitiza kuwa, wakati ukifika Serikali itatoa maelezo ya kina na kuwafanya Watanzania wapate ukweli.

Sakata la madai ya kuchotwa kwa fedha katika akaunti ya Escrow ndilo linalotawala kwa sasa nchini, hasa baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Swerikali (CAG) kuwasilishwa bungeni, na sasa ikitarajiwa kujadiliwa bungeni kwa siku mbili kuanzia keshokutwa. Akizungumzia Katiba Inayopendekezwa, alisema Serikali itatoa nakala za kutosha za katiba hiyo ili wananchi wengi wasome na kupata fursa ya kutoa maoni yao.

Aidha, alisema Kanisa la Anglikana nchini limetoa mchango mkubwa katika kuendeleza huduma za jamii kwa kujenga shule, hospitali, vituo vya afya na miradi mingine ya kijamii. Pia aliutaka uongozi wa kanisa hilo kuibua fursa za miradi ya maendeleo ili kusaidia familia masikini kuwa na miradi midogo ikiwemo ya ufugaji kuku.

Kwa upande wake, Dk Chilongani aliahidi kuboresha elimu na huduma za jamii na kusimamia kikamilifu vitenga uchumi vya kanisa hilo.

“Sikuota kuwa askofu ni neema ya Mungu,” alisema.

Chanzo :Habari leo
 

FUKO LA DHIKI

JF-Expert Member
May 8, 2011
416
225
Pinda muda wa kuumbuliwa unakaribia,unajifanya mtoto wa mkulima kumbe ni walewale wachumia tumbo
 

mavumbi

JF-Expert Member
Feb 8, 2013
433
250
Upuuuzi mkubwa! Tumefikia mahali badala ya kutumia Makanisa kama mahali pa kushahijisha kuendelea kumtukuza Mungu, tunaruhusu kuzungumzia mambo yanayostahili kuongelewa kwingineko, au walipanga kumsaidia Bwana Pinda kusema yale anayoshindwa kuyasema Bungeni?
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
35,886
2,000
Ukiona anaongea hivyo ujue amejiandaa barabara sasa wale wa timu yerico mjiandae kuwa very disappointed msije sema hatukuwambia.
 

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
7,633
2,000
Chanzo cha habari: Habari Leo

Mmiliki wa chanzo: serikali ya Ccm

Wezi wa pesa za escrow: viongozi wa serikali ya ccm

Concl:
Mwizi hawezi kusema ameiba hasa sehemu kama kanisani.
 

MWINZA

Member
Jan 10, 2014
57
0
Pinda anasema watanzania watapewa taarifa sahihi kuhusu escrow muda ukifika! Anasubiri nini kutoa tarifa hiyo? bwawa limeelemewa na maji yanataka kuvunja bwawa eti anasubiri muda. Au ndo kusubiri uchakachuaji wa taarifa ya CAG?
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,954
2,000
Duh.... kumbe source ya habari yenyewe ni gazeti la Habari leo?

Yeye Pinda asianze kuweweseka kwa kudai kuwa habari zinazoongelewa kwa sasa zimetiwa chumvi.

Yeye atulie tu ifike hiyo k'kutwa ripoti ya CAG isomwe bungeni, yeye Pinda sisi waTz, hatumwamini tena.

Ni yeye Pinda mwanzoni alisema pesa za Escrow siyo mali ya umma.

Ripoti ya CAG iliyotoka imemuumbua, kwa kuthibitisha pasipo shaka yoyote, kuwa pesa ile ilikuwa ya umma ya shirika la TANESCO.

Majuzi tena Pinda, alijaribu kutaka kuwalaghai wabunge kuwa kuna zuio la mahakama ili hoja hiyo isijadiliwe.

Pinda akaumbuka kwa mara nyingine tena,baada ya mahakama kukanusha kuandika barua hiyo,

Kwa sasa watanzania tunalaximika kuwa na msimamo mmoja tu.

We want our money back, and all those found guilty of stealing our money, to serve long terms in jail!
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
Ukiona anaongea hivyo ujue amejiandaa barabara sasa wale wa timu yerico mjiandae kuwa very disappointed msije sema hatukuwambia.
Wenye nchi wako tayari kusikia viongozi hawako tayari kusema!!!
Ndio maandalizi hayo???!!!!
 

sexologist

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
2,289
1,195
Hii taarifa ishachakachuliwa sanaaa.... Mpaka Pinda amenza kusema watu wanaongeza chumvi... Means kuna habari ambazo zilisambazwa kimakosa na kwamba sasa zipo tofauti.
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
Hii taarifa ishachakachuliwa sanaaa.... Mpaka Pinda amenza kusema watu wanaongeza chumvi... Means kuna habari ambazo zilisambazwa kimakosa na kwamba sasa zipo tofauti.
Watu wa IT wapo mkuu, lini imetengenezwa na lini ilikiwa edited yatafahamika!!!
Authors wapo hai, yaani ikizimika sasa wakati wa uchaguzi itainuka tu! !!
Kazi iliyopo ni kuzima sasa na kuhakikisha haliibuki tena kitu ambacho hakijawahi kufanikiwa!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom