Pinda afunguka sakata la Escrow

Pinda afunguka sakata la Escrow

Pinda anasema watanzania watapewa taarifa sahihi kuhusu escrow muda ukifika! Anasubiri nini kutoa tarifa hiyo? bwawa limeelemewa na maji yanataka kuvunja bwawa eti anasubiri muda. Au ndo kusubiri uchakachuaji wa taarifa ya CAG?

Hata mimi hapo kanishangaza ............................ huo muda utafika lini?? Kama kweli anaona uvumi ukiendelea mwisho utakuwa ukweli kwa nini serikali bado inaendela kukaa kimya. Na kwa nini akasemee makanisani!!? Off course Taifa letu limekuwa la uvumi kwa kuwa serikali huwa inanyamaza mambo kama haya yakitokea. Sasa ameona pressure imezidi anataka kuleta longolongo.....................!!
 
Pm ananiudhi kutumia kanisa kama jukwaa la kisiasa.
shame on you!
 
Mwiziiiiiiiii mkubwaaaaaaaaa....jizi kweliiiiiiii.....!!!!


Kila mtu anajua huyu mwizi alivyokuwa siku hizi....muongo mkubwa....!!!
 
pindahasira_300_182.jpg

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema taarifa nyingi za mjadala wa akaunti ya Escrow iliyofunguliwa kutokana na mgogoro wa malipo ya gharama za umeme kati ya kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) ambao unaendelea bungeni, umeongezwa chumvi na wakati ukifika Watanzania watatolewa taarifa kamili.

Kauli hiyo ya Pinda aliitoa kanisa kuu la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika wakati wa kumsimika Dk Jackson Chilongani kuwa Askofu wa Sita wa dayosisi hiyo.

Awali, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini, Jacob Chimeledya aliitaka Serikali kutoa taarifa juu ya akaunti ya Escrow ili wananchi wajue kilichotokea ili ijulikane ukweli upi na uvumi upi kwani iko hatari ya kutengeneza taifa lenye kuamini uvumi.

Dk Chimeledya alisema Watanzania sasa wanaishi kwenye hali ya sintofahamu kwani hawajui yupi anasema ukweli na yupi ni `mzushi’. Alisema ni lazima Serikali itoe maelezo kwa wananchi juu ya kashfa hiyo ili wajue kilichotokea kwani ipo hatari ya kutengeneza taifa linaloishi kwa kuamini uvumi.

“Hatutakiwi kuishi kwenye taifa linaloamini uvumi… taifa halitapiga hatua kwa taarifa za kusikia tu bila kujua ukweli uko wapi, nini kimetokea na hatua gani imechukuliwa,” alisema.

Pia Askofu Chimeledya alitumia fursa hizo kuuzungumzia mchakato wa Katiba iliyopendekezwa na Bunge, akiitaka Serikali kutoa elimu kwa wananchi kabla ya kupiga kura ya maoni Aprili mwaka kesho.

Alisema wananchi waachiwe waamue baada ya kuisoma katiba hiyo na si kuwafuata wanasiasa ambao wamekuwa na milengo tofauti kutokana na wengine kushawishi wananchi kupiga kura ya ndio huku kundi lingine likitaka Katiba hiyo kupigiwa kura ya hapana.

Alisema kama Serikali haitasimama imara kusimamia mchakato huo, basi utatekwa na watu wenye nia mbaya.

“Makundi yote yakae kimya Katiba hii ni ya wananchi, waachiwe waamue na si kuwasemea watu wapige kura ya ndio au hapana.

Askofu huyo aliwataka viongozi wa kanisa hilo kuongoza vizuri kwani ni aibu kwa Mkristo au kiongozi wa kanisa kuharibu kanisa, kinachotakiwa kila mmoja kuchukua nafasi yake kuongoza kanisa vyema.

Akitoa salamu za Serikali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema kuhusiana na kashfa ya Escrow na IPTL alisema taarifa nyingi zimeongezwa chumvi. Hata hivyo hakutaka kuingia kwa undani kuzungumzia suala hilo, huku akisisitiza kuwa, wakati ukifika Serikali itatoa maelezo ya kina na kuwafanya Watanzania wapate ukweli.

Sakata la madai ya kuchotwa kwa fedha katika akaunti ya Escrow ndilo linalotawala kwa sasa nchini, hasa baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Swerikali (CAG) kuwasilishwa bungeni, na sasa ikitarajiwa kujadiliwa bungeni kwa siku mbili kuanzia keshokutwa. Akizungumzia Katiba Inayopendekezwa, alisema Serikali itatoa nakala za kutosha za katiba hiyo ili wananchi wengi wasome na kupata fursa ya kutoa maoni yao.

Aidha, alisema Kanisa la Anglikana nchini limetoa mchango mkubwa katika kuendeleza huduma za jamii kwa kujenga shule, hospitali, vituo vya afya na miradi mingine ya kijamii. Pia aliutaka uongozi wa kanisa hilo kuibua fursa za miradi ya maendeleo ili kusaidia familia masikini kuwa na miradi midogo ikiwemo ya ufugaji kuku.

Kwa upande wake, Dk Chilongani aliahidi kuboresha elimu na huduma za jamii na kusimamia kikamilifu vitenga uchumi vya kanisa hilo.

“Sikuota kuwa askofu ni neema ya Mungu,” alisema.

Chanzo :Habari leo

Nothing new!?
 
spencer, Kimbunga, ocampo four na wengine wote,
Hii inaitwa jaza jaza thread na yeye aonekane ameandika uzi uliochangiwa na watu wengi.
Mmejitahidi kumjazia komenti lakini si mbaya
 
Last edited by a moderator:
Wkati upi ukifika? Labda anamaanisha wakikamilisha uchakachuaji ndio muda utakuwa umefika
 
Mwizi mkubwa huyo.

Mbona umeongea kiushabiki mkuu,ebu jaribu kujenga hoja ni kwa namna gani PINDA amehusika na uwizi huo?Kwani tunakumbuka wakati wa ufisadi wa Richmond uliofanywa na Edward Lowassa ripoti ya kamati ya Mwakyembe ilizungumza kwa kina namna ambavyo Edward Lowassa alivyokuwa anashinikiza watendaji wa serikali walio chini yake kufanikisha mchakato wa Richmond na Kuiba pesa za umma mpaka ikapelekea jamaa kujiuzulu kwa lazima
 
Tunakuaminia Waziri mkuu wetu wakati ukifika wekeni wazi ukweli wa yote kuhusu sakata la ESCROW tunajua siasa imeingia kwenye suala hilo Edward Lowassa na team yake wanatumia nafasi hiyo kuihujumu na hatimaye kuiangusha serikali ya J Kikwete njama zao hizo zinajulikana na muda si mrefu wataumbuka.
 
Wkati upi ukifika? Labda anamaanisha wakikamilisha uchakachuaji ndio muda utakuwa umefika

Nani achakachue wakati kila kitu kipo wazi tusubiri ripoti isomwe mkuu acha kuwa na mawazo hasi kwa kila kitu akili ya kuambiwa changanya na za kwako!
 
Pinda muda wa kuumbuliwa unakaribia,unajifanya mtoto wa mkulima kumbe ni walewale wachumia tumbo


Unanichekesha mkuu. Hivi nani kakuambia kuna kiongozi msafi ndani ya CCM? Kile chama kimejawa na wasanii na wanaotaka kuja madarakani nao pia mawazo yao ni kuja kuiba na kulipiza visasi kwa wenzao huku wakisahau maendeleo ya nchi na mahitaji ya wananchi wao.
 
Kakimbilia chachi? Kweli simba akizidiwa hunywa hata supu ya kabeji.
 
''umeongezwa chumvi na wakati ukifika Watanzania watatolewa taarifa kamili''
Mheshimiwa Pinda anafanya kosa kubwa sana hapa......
 
Mwiziiiiiiiii mkubwaaaaaaaaa....jizi kweliiiiiiii.....!!!!


Kila mtu anajua huyu mwizi alivyokuwa siku hizi....muongo mkubwa....!!!

Ebu tujadiri hii hoja kisomi tuache ushabiki wa kisiasa,naoma utuambie ni kwa namna gani Mizengo Pinda anahusika na uwizi huo?manake tukikumbuka kwenye sakata la Richmond ripoti ya Mwakyembe ilidadavua vizuri kwa ushahidi uliojitosheleza namna Bw. Edward Lowassa alivyohusika kukwapua fedha za umma bila huruma zaidi shilingi mil.152 kwa siku iwe umeme umezalishwa au haujazalishwa kwenda kwenye gridi ya Taifa.Ebu piga mahesabu kwa mwaka ingekuwaje na je ingekuwa miaka mitano ingekuwaje pia? Edward Lowassa na mafisadi wenzake wangeweza kukwapua kiasi gani cha fedha kama mkataba usingesitishwa baada ya ripoti ya Mwakyembe kuibua uwizi huo.Hiyo ni moja ya mikataba mibovu ya kinyonyaji aliotuingiza Edward Lowassa muda mfupi baada ya kuteuliwa kuwa waziri mkuu.Huyo ndiyo Edward Lowassa kamwe huwezi kumfananisha na Mizengo Pinda katika uaminifu wao,uadilifu wao na weledi wao katika utekelezaji wa majukumu ya serikali.
 
Makanisa sasa yanatia kinyaa kusafisha Majizi... hapo ndo amefunguka? Ukanjanja katika uandishi sasa yanafikia kilele cha ujinga...
 
Back
Top Bottom