Pikipiki za honda zinauzwa

Pikipiki za honda zinauzwa

nimecheka lakini pia nimesikitika sana kusoma hii post ..... yaani ina maana nyumba nyingi za tembe na udongo zisizo na hata choo ambazo ndizo nyingi Tanzania ndiyo ubora Wa maisha? .....

teh teh teh ... kazi kweli kweli
izo pikipik mnazosema orignal haziwez ubavu wa pikipik za kichina kama hauamin jaribu..mi nna experience na tuktuk...watu tunabeba debe had 12 za viaz mzigo ambao honda haitapanda mlima...
 
Mkuu mi ninayo Honda CT 110,nahitaji spears zake kama carburator,oil filters,plugs etc naweza kuzipata hapo ofisini kwenu?
Ni hii hapa namaanisha
37303_honda_ct110_thumb-4b77aa8124c86-750x400.jpg
kama hutu walitusifia zamani lakin kwa mchina habari ingine
 
halafu kuna wadau naona wanakuja huku kucomment habari za kusifia pikipiki zingine, sawa sikatai maoni ya wadau maana kila mtu ana mapenzi yake lakini kama wewe mdau unapenda brand ya pikipiki fulani na hutaki kusikia pikipiki za honda basi, anzisha uzi wako wa pikipiki zako ili upate watu wako. Tuachie wadau wa Honda wapate habari na maendeleo ya pikipiki za Honda. Honda ni pikipiki iliyovumbuliwa na mjapan kwa miaka mingi na mpaka leo kuna nchi 21 zinatengeneza Pikipiki Honda under licence from japan kwahiyo Honda itaendelea kuwepo kizazi hadi kizazi.
 
Habari wadau wa biashara, napenda kuwatangazia Kwa wale wanunuzi wa piki piki, Tunazo piki piki za Honda kutoka Quality Motors ltd. Mnaweza kutembelea na kuziona kwenye showroom ya Msasani karibu na Hospitali CCBRT, Msasani. Piki Piki za Honda ni mpya na imara kabisa, na vile vile zina fahamika sana kwa wadau wetu.

Aina za piki piki ambazo tunazo ni kama ifuatavyo;

1. Honda CG 110 - Bei ni mil.1.9 pamoja na usajili na warranty ya mwaka mzima.
2. Honda Ace 125 cbd- Bei ni mil. 2.8 pamoja na usajili na warranty ya mwaka mzima.
3. Honda TUF 125- Bei ni mil.3.4 pamoja na usajili na warranty ya mwaka mzima.

kwa mawasiliano zaidi fika showroom yetu ya Honda, Eneo la Msasani. Au piga simu 0717 518359. Barua pepe- jonelias6@gmail.com

Honda Spare parts zipo tunauza hapo hapo ofisini. Karibuni wateja wetu.
Ndugu naomba nikupe shukrani za dhati kwa maelezo yako na namna ulivyofikisha ujumbe kwa wateja (Watanzania). Mimi niliingia chaka kwa kununua pikipiki mbili aina ya LML CRD 100 pale kwa Bin Mussa mtaa wa Mfereji wa Wima Zanzibar mwaka 2008. Ni nzuri na hazitumii mafuta mengi lakini huyu jamaa alivyo wa ajabu hana spea hata moja zaidi ya helmet!! Nilimletea baba na mimi lkn ninavyoongea na wewe zote nimepaki kwa kukosa Cabulator, kick rod na spea zingine. Niloshafika kama mara mbili kipindi natembelea huko lkn ukifika anakushauri uweke injini ya pikipiki za kichina!! Takutafuta siku nikija Tz maana Honda wako vizuri.
d4ad952dbfd854ab925e1e7ede8b11dc.jpg

c5feb50c31757dfba7331deae3340a68.jpg
 
Inafaa kwa boda2?
Inafaa vizuri sana na wapo wadau wengi tu nimewauzia hizo CG 110, wanazitumia kwa bodaboda na imewaletea faida. Njoo ofisini kwetu msasani kucheki pikipiki mwenyewe au nipigie simu 0717518359.
 
Inafaa vizuri sana na wapo wadau wengi tu nimewauzia hizo CG 110, wanazitumia kwa bodaboda na imewaletea faida. Njoo ofisini kwetu msasani kucheki pikipiki mwenyewe au nipigie simu 0717518359.
Nikja Dar nitakuja tuongee vizur angalau niwe nalipa kidogokidogo
 
izo pikipik mnazosema orignal haziwez ubavu wa pikipik za kichina kama hauamin jaribu..mi nna experience na tuktuk...watu tunabeba debe had 12 za viaz mzigo ambao honda haitapanda mlima...
Kupanda itapanda, tena zaidi ya huo mchina wako, ila honda suspension yake ni laini, haikukusudiwa kubeba hiyo miviazi yote. Ukinunua kitu hebu soma manual yake kwanza. Gari ya salon unataka ubebee mawe na kokoto?Nunua pikap.
 
Honda TUF 125 ni kickstarter. kwa Piki piki ya Honda yenye engine ya 125 cc inauwezo wa kutembea mpaka KM 160 au mpaka KM 220 bila kupumzika. zaidi ya hapo utachemsha na kuunguza engine . Honda za engine kubwa kama 200cc mpaka 250 cc hizo zinaweza kutembea umbali mrefu zaidi ya hapo.
Dar mpaka Songea ni umbali wa KM 1000. kwa piki piki ya 125 cc haitaweza safari hio. ni bora upakize piki piki kwenye lori usafirishe ipelekwe huko. Sidhani kama kuna dereva ambaye atakubali kuendesha umbali mrefu wa KM 1000 na piki piki.
kama picha nilizotuma hujaziona basi nipe namba yako ya whatsapp nikutumie. Asante.

Majibu yako yanashangaza kidogo, hivi hizo pikipiki zimehundwa Japan kweli? Pikipiki gani zinachemsha injini ikitembea 160KM - mimi sijawahi kusikia Honda genuine kutoka Japan zenye matatizo ya ajabu kama hayo!! Sina nia mbaya ila nataka ufafanuzi zaidi.
 
Nina Honda nx250 nishawahi kui post humu kuwa naiuza Mashine hiyo nliinunua Denmark IPO mpaka sahvi ...bado naiuza ntafutie mteja

Mkuu tujuze kidogo maanake pikipiki yako ni Honda halisi, hivi kwenye manual yake kuna sehemu yoyote inayo kushauri kwamba ukitembea kilometa fulani ni lazima uipumuzishe kuepusha injini kuchemka!!! Kama huna manual , je, katika uzoefu wako umewahi kukumbana na tatizo la injini ya pikipiki yako(Honda) kuchemka kutokana kusafiri safari ndefu?
 
Back
Top Bottom