utaratibu nikesh tu?hakuna utaratibu wa kukopesha na kulipa kidogo kidogo?nauliza mufti wangu
Papaa kishimba, utaratibu wetu wa mikopo upo.
kuna kulipa kwa kubandika yaani unaanza kulipa asilimia 50 ya malipo kisha zingine unalipa kwa awamu na muda wa kumaliza deni usizidi miezi 3. Kwa utaratibu huu, chombo hupewi mpaka umalize malipo.
Utaratibu mwingine, tupo na crbd bank, wanatoa mikopo ya Honda kwa wateja wetu. kuna masharti ambayo lazima utekeleze pale crdb, kama kujaza fomu, kuweka wadhamini, na mambo mengine. ukifanikiwa kumaliza masharti yao utatakiwa ulipe asilimia 20 ya malipo. kisha wao watakupa piki piki ya Honda na kila mwezi lazima upeleke 120,000 au 150,000. Crdb wao wanatoa mikopo ya boda boda ya mwaka au miaka miwili.
utaratibu mwingine, tupo na saccos ya Kitunda, wao nao wanatoa mikopo ya Honda Pikipiki kwa wanachama wao. hawana masharti mengi kama crdb, unachotakiwa ni kujiunga na chama chao na kuwa mwanachama wao. kisha kuna masharti yao unatakiwa utekeleze kama unaomba mkopo kwao. Kitunda saccos ni saccos kubwa ina members zaidi ya 8000. ni taasisi kubwa na inahudumia wakazi wote wa dar es salaam. ofisi zao zipo kitunda shule.
Hizo ndio njia ambazo nazifahamu.