Pigo takatifu dhidi ya Chadema muda huu

Pigo takatifu dhidi ya Chadema muda huu

Tangu Uhuru tulikubali kua maadui wetu ni
1.Ujinga
2.Magonjwa
3.Umaskini
Bila shaka awa maadui bado wapo ila hamna jituhada za maana za kuwaondoa awa maadui kama tunavyofanya kuwatoa wapinzani kwenye vyama vyao.
Very primitive.. uncultured.. insane.
 
Huyo mbatia ikulu alienda kula miwa au?
Alienda kuahidiwa kupewa wabunge na madiwani wa kutosha. Baada ya kuona ahadi yake ya kuufuta upinzani imeshindikana ameona bora awe na 'upinzani' upinzani wa mfukoni. Nawaonea huruma wagombea wa CCM kwenye majimbo yenye wagombea wa NCCR. Maana hapo Chadema au CCM hawana chao.
 
Marehemu Franco Lwambo lwanzo Makiadi alisema: WHEN YOU JOIN IT IS ORCHESTRE KINSAHSA JAZZY , BUT WHEN YOU LEAVE IT IS KINSAHSA ORCHERSTER. MEANING THEY JOINED CDM WHEN IT WAS WEAK,BUT THEY ARE LEAVING WHEN IT IS MUCH STRONGER.
Luambo alikuwa haongei Kiingereza, acha fiksi zako. Kinsahsa ndio wapi huko?
 
Wakati anaondioka CCM aliwakusanya waandishi wa habari kama hivi? Tupate clip yake ili tulinganishe hoja zake za kuondoka CCM na hizi za kuondoka CDM.
Kwa mtizamo wake ni sawa na wengine watakuwa na mtizamo tofauti. Kuwapoteza mawaziri wakuu wastaafu ilikuwa ni pigo na udhaifu wa uongozi wa CDM.
Waziri mkuu mstaafu Sumaye alitaka kuwa kiongozi wa CDM Taifa - nilikuwa sijui hilo; kumbe alipokosa akaamua murudi CCM!
Kumbe nawe ulimpinga Sumaye! Kwa nini ulimpinga wakati sasa unasema lilikuwa ni pigo kumpoteza? Contradiction
 
Hivi kwa Nini Hawa watu wasichunguzwe kwa tuhuma za rushwa.
 
Mbowe anazidi kubamizwa.

Kwa siasa za kiafrika hayo mbona ni mambo ya kawaida sana!! Lazima afanye hivyo ili kumridhisha, jamaa anayechochea moto!! Wakina sumaye, lowasa, mgenja ilikuwahe kipindi kile wanahama ccm?!!! Siasa za kiafrika zinatawaliwa na njaa!!!
 
Naona malumumba yanafurahia sana
Mbowe ni mwamba futeni chadema sasa mbaki nyie wenyewe mfurahi ila mbowe anawakimbiza hamlali mala chama kimekufa sasa sijui mnahangaika na mini kwa chama mfu
 
Nimemsikiliza vizuri Mustapha Muro mwanzo mwisho

Halafu nimesoma comment zote za waliochangia huu mjadala hapa

Mustapha Muro namfahamu vizuri sana. Simfahamu kama mwanasiasa tu, bali namfahamu kama msomi mtaalamu wa networking engineering, aliyewahi kuwa mmoja wa watu muhimu kwa kushika top position kwenye hii mitandao ya simu unayoifahamu hasa Vodacom ambapo alifanya kazi kwa muda mrefu

Namfahamu kama mfanyabiashara na mdau muhimu katika sekta ya mawasiliano hapa Afrika mashariki kwa kuwa miongoni mwa wamiliki wa makampuni ya minara

Namfahamu kama Baba mwenye familia imara, kaka, mjomba na aina ya mtu mstaarabu na ni miongoni mwa watu wenye siasa za kistaarabu na za kisomi

Mwaka 2015 kipindi cha uchaguzi mke wake ndio alikuwa mtu muhimu wa mfumo uliotumiwa kukusanya kura toka mikoani

Kwa kifupi, yeye ndio alikuwa organizer wa wale vijana waliokamatwa hotelini wakikusanya na kuhakiki kura kutoka majimboni

Baada ya sakata lile, mke wake na baadhi ya wanafamilia wake walipitia wakati mgumu sana maana walikamatwa wote na kufunguliwa kesi tofauti kabisa ya human trafficking. Mke wake alisota segerea karibu mwezi mzima

Muro kama msomi na mtu mstaarabu anajua anachokiongea

Hoja inayotoka kwa Muro si ya kubeza hata kidogo. Ni mtu mzima na anafahamu mengi ndani ya chama na ndani ya nchi hii

Ni bahati mbaya sana wanachadema wengi hadi sasa bado wanaamini katika siasa za matusi, udhalilishaji na kukoseana adabu

Ni bahati mbaya sana chadema bado inaamini aina ya ukosoaji wa kina mdude mitandaoni

Namfahamu Bwana Malisa, ni mtu wa chadema. Anaandika sana mitandaoni. Anakosoa kwa hoja. Sikumbuki kama ameshawahi kuonekana mkosa adabu na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi au udhalilishaji wa kimtandao

Ifike mahali tujadili hoja zinazotolewa kuliko kubeza na kujipa moyo kwamba chama kiko imara

Wanachadema wengi hata hamjui kwanini siku hizi Mnyika kawa kimya sana

Si jambo la kawaida sana wanamageuzi kama kina Mabere Malando, Prof. Safari na wengine wengi walioisapoti chadema nao wakawa wendawazimu kusema chadema haiko sawa

Kwanini? Lazima kuna kitu

Tuachane na hao wengine wanaolilia pesa ambazo wanafahamu kabisa kwanini walikuwa wanakatwa na miaka yote imekuwa hivyo

Tuachane na hao wanaolilia kudhalilishwa kingono kwasababu wanazozijua wao maana wanajua madawati rasmi ya kwenda kulalamika lakini hawakwenda

Tujadili hoja kama hizi za Muro. Ni hoja nzito zilizo na ushahidi na zinaweza kujadilika na kizuri zaidi hoja za Muro hazina majungu wala vijembe. Ni hoja ambazo zikichukuliwa zinaweza kukirudisha chama kwenye mstari

Huwezi kutaja umasikini wa Tanzania bila kuitaja CCM, huwezi kuisema serikali iliyoko madarakani bila kumtaja Magufuri. Hali kadhalika huwezi kutaja udhaifu unaotokea chadema bila kumtaja Mbowe!

Ifike mahali tukubali kwamba "huwezi kukwepa ngumi kwa kufumba macho"
 
Back
Top Bottom