PICHA: Ziara ya Rais Magufuli nchini Rwanda

PICHA: Ziara ya Rais Magufuli nchini Rwanda

Barbarosa
Mkuu kwenye UTAMADUNI na MILA hakuna kitu hii:- ati haziendani na TIME !! You are wrong rafiki!!

Mkataa kwao Mtumwa !! WHY uidharau kiTZ.. na uitukuze ya wengine...? hapo kila moja ina taste na uhodari wake... TZ kuna makabila meeeengi... your choice na zote bomba!!
 
Mahusiano yetu ni mazuri kati ya Tanzania na Rwanda.
 
Unakumbukumbu sana mkuu, hilo koti kama sikosei alipiga siku ile anaenda kuwasilisha silaha zake kutii agizo la mkuu wa mkoa wa Dar. Ukizingatia ametumia usafiri wa barabara.....

Yeah...Presidaa wetu yupo kamili!
 
Huko atatumia lugha gani maana Kiswahili sanifu cha kuongea na raisi wa Rwanda hajui
Kiingereza ndo usiseme
 
images
Hapo alikua anamchora jk
 
la uncle magu halijanda?manaake rwanda kwa watoto duu!alaf n mambo gan ya kiushrikiano wamekubaliana?
 
UKIANZA KURUKA TUA KWANZA RWANDA

Wakati gazeti moja la kila siku likichapisha taarifa ambayo haijathibitishwa kuwa Ikulu imesema Rais Magufuli huenda akaanza kusafiri kwenda nje kuanzia mwezi Juni mwaka huu, Rwanda inapaswa kuwa kituo muhimu mno cha kiongozi huyo kuzuru mwanzo.

Rais Magufuli hapaswi tu kwenda nje pindi atakapoanza kufanya hivyo badala yake ni lazima safari hizo ziwe za kimkakati na stratejia na kwa ujumla katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, Rwanda ni nchi ya kimkakati.

Rwanda miongoni mwa nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara ni nchi ya kustaajabisha na kujifunza. Inatushangaza sote na hasa tuliobahatika kuisoma na kuizuru. Na ndio maana magufuli aende Kwanza Rwanda.

Kwanza ni jirani lakini pili ni nchi yenye kufanya maaajabu.

Taifa hilo lililokumbwa na jinamizi la mauaji ya kimbari, si taifa la kilofa na maskini tena, katika huduma za jamii yaaan afya, Elimu, maji, miundombinu na mawasiliano Rwanda imezipiku mbali nchi za dunia ya Kwanza ikiwemo za Barani ulaya.

Asilimia 92 ya wanyarwanda wanapata huduma bora za afya kupitia mpango wa serikali wa bima ya afya kwa raia wake, hiyo ni zaidi ya nchi kama Bulgaria, Estonia, Lithuania, Serbia, Ureno, Malta na Cyprus zote za Barani ulaya. Liko la kujifunza hapa na magufuli aende Kwanza Rwanda kabla ya Kwengine kokote.

Magufuli aende amuulize mwenzake Kagame imekuaje Rwanda inapeleka shule zaidi ya Asilimia 90 ya watoto na tena katika mazingira mazuri na salama.

Akifika aulize imekuaje miundombinu ya Rwanda imeboreka na kustaajabisha kwa uzuri kiasi hicho na ilhali hawana dhahabu wala Tanzanite?

Amkamate kooni Kagame aseme miradi ya kuwasaidia watu maskini vijijini ilibuniwaje na Rwanda haina ardhi wala rasilimali za kutosha. Maana ndo nchi ambayo watu wake wanakunywa maziwa ya kutosha katika eneo jumla la Afrika Mashariki na kati.

Ikisha amuhoji taratibu imekuaje maafisa hawali rushwa na miradi ya umma inatekelezwa kwa wakati na ubora?

Asiache ajue wanapata wapi fedha na Bandari hawana? Magufuli akae darasani, aelekezwe aelewe, asibabaishe ajifunze, asibishe aulize, aandike akumbuke na arudi kutoka ziara hiyo ya Kwanza ya nchi akiwa na mkakati mpya wa kuelekea mafanikio j makubwa.

Wasikuhadae kina Sefue mzee, usichome mafuta kwenda kunywa chai mbali, ukianza kuruka fika Kwanza Rwanda.
 
kweli magu noma.....nchi ya kwanza kuvisit na rwanda amabe alikuwa mgomvi wa kikwete...hahaaa magufuli anajua kuchagua marafiki....,kagame yupo vzur mkishauriana vzur. mtafika mbali...big up
 
Saaafi my Honorable President JPM, naona Paul Kagame anakubeep kubana matumizi (Hajapiga suti) sasa kumuonyesha kwamba wewe ndo muasisi wa kubana matumizi kesho piga pensi na simple kwenye maazimisho ya kimbali.


Hahah, nimecheka. Ila ni 'maadhimisho' na ni 'mauaji ya kimbari'....blaza!
 
Nimeipenda hii ya Rwanda angalia wanavyopendeza na inaonekana kabisa ni utamaduni wa Kistaarabu hivyo kwa kuwa kitu kizuri hakuna ubaya kukiiga basi ningependekeza tuige hivi na ile mingoma ngoma yetu ya sijui Sindimba mara kucheza na Mijoka tuiachilie mbali, hii ya Rwanda imekaa poa zaidi inaendana na karne ya 21!


CfW1xc3XEAErq4a.jpg


Hii ya kwetu tuiache, siyo ya kistaarabu!
images
images
images
We jamaa umenichekesha sana usiku huu basi tu, hahah. Ngoma za mwanamalundi hizo, hahah
 
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg


Hizi ni picha mbalimbali za Mh. Magufuli akiwa ziarani Rwanda. Rais Magufuli alipewa ng'ombe watano na Rais Kagame na kwa mila na desturi hubeba fimbo wakati wa kupewa hao ng'ombe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom