Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,356
UKIANZA KURUKA TUA KWANZA RWANDA
Wakati gazeti moja la kila siku likichapisha taarifa ambayo haijathibitishwa kuwa Ikulu imesema Rais Magufuli huenda akaanza kusafiri kwenda nje kuanzia mwezi Juni mwaka huu, Rwanda inapaswa kuwa kituo muhimu mno cha kiongozi huyo kuzuru mwanzo.
Rais Magufuli hapaswi tu kwenda nje pindi atakapoanza kufanya hivyo badala yake ni lazima safari hizo ziwe za kimkakati na stratejia na kwa ujumla katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, Rwanda ni nchi ya kimkakati.
Rwanda miongoni mwa nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara ni nchi ya kustaajabisha na kujifunza. Inatushangaza sote na hasa tuliobahatika kuisoma na kuizuru. Na ndio maana magufuli aende Kwanza Rwanda.
Kwanza ni jirani lakini pili ni nchi yenye kufanya maaajabu.
Taifa hilo lililokumbwa na jinamizi la mauaji ya kimbari, si taifa la kilofa na maskini tena, katika huduma za jamii yaaan afya, Elimu, maji, miundombinu na mawasiliano Rwanda imezipiku mbali nchi za dunia ya Kwanza ikiwemo za Barani ulaya.
Asilimia 92 ya wanyarwanda wanapata huduma bora za afya kupitia mpango wa serikali wa bima ya afya kwa raia wake, hiyo ni zaidi ya nchi kama Bulgaria, Estonia, Lithuania, Serbia, Ureno, Malta na Cyprus zote za Barani ulaya. Liko la kujifunza hapa na magufuli aende Kwanza Rwanda kabla ya Kwengine kokote.
Magufuli aende amuulize mwenzake Kagame imekuaje Rwanda inapeleka shule zaidi ya Asilimia 90 ya watoto na tena katika mazingira mazuri na salama.
Akifika aulize imekuaje miundombinu ya Rwanda imeboreka na kustaajabisha kwa uzuri kiasi hicho na ilhali hawana dhahabu wala Tanzanite?
Amkamate kooni Kagame aseme miradi ya kuwasaidia watu maskini vijijini ilibuniwaje na Rwanda haina ardhi wala rasilimali za kutosha. Maana ndo nchi ambayo watu wake wanakunywa maziwa ya kutosha katika eneo jumla la Afrika Mashariki na kati.
Ikisha amuhoji taratibu imekuaje maafisa hawali rushwa na miradi ya umma inatekelezwa kwa wakati na ubora?
Asiache ajue wanapata wapi fedha na Bandari hawana? Magufuli akae darasani, aelekezwe aelewe, asibabaishe ajifunze, asibishe aulize, aandike akumbuke na arudi kutoka ziara hiyo ya Kwanza ya nchi akiwa na mkakati mpya wa kuelekea mafanikio j makubwa.
Wasikuhadae kina Sefue mzee, usichome mafuta kwenda kunywa chai mbali, ukianza kuruka fika Kwanza Rwanda.
Niliwaangalia Bill na Melinda Gate kwenye BBC breakfast miaka kama miwili iliyopita, walikuwa wanaongelea jinsi wanavyotoa pesa, walisema wamebakiza pesa itakayo wasaidia wao mpaka uzeeni lakini pesa ya ziada ni kheri isaidie masikini................. Any way, walisema katika nchi za Afrika walizosaidia wanapata moyo sana na mabadiliko ya maisha yaliyoletwa na pesa zao Rwanda, nchi nyingine zinawavunja nguvu.