PICHA: Ziara ya Kinana Mtwara yafana

PICHA: Ziara ya Kinana Mtwara yafana

Secretarieti ya kina mkama ilianza hivi hivi mara ghafla ikatoweka na hata yale waliyokuwa wakiyahubiri ya kuvuana magamba wakayakana.
.
 
29555_492009197506234_986802517_n.jpg
 
Kufana ni pale watu wanapojitokeza kwa hiari yao kuhudhuria /kushiriki mkutano. Hapa ccm inaonekana wameambiwa ni lazima kila kiongozi afike na watu wa chini yake wakiwa wamevaa sare . Kwa wale ambao hawana sare walinunuliwa ili wasijeta aibu. Jamani siasa hizo zimepitwa na wakati, ni kiini macho .tein imeshaondoka.
 
Hakika mshauri wa chama naona alishakufa,maana wanavyokurupuka utadhani hawakwenda shule,siku mbili hizi ni kipi kipya watawaeleza watanzania juu ya kujenga hicho chama,ni lini wamepanga na kutengeneza action plan? Hii ni nguvu ya pepsi hawatakwenda mbali.Zama za sifa zimepitwa na wakati
 
KINANA,NAPE,KHATIB WATUA MTWARA..kazi ya kusimamia ilani ya uchaguzi yapamba moto.

Napata taabu sana kuelewa hivi ilani ya uchaguzi si ina shughuli ambazo zinatakiwa kufanywa na watumishi wa Serikali, Hivi katibu wa Chama ana mamlaka ya kusimamia na kutolea matamko juu ya shughuli hizo au waziri ndo mwenye dhamana na shughuli hizo? ninachoona hapa kutakuja mkanganyiko ambao mwisho wa siku hakutakuwa na msimamizi mkuu juu ya kusimamia shughuli za maendeleo kwani siku zote kiongozi wa chama asiye na madaraka serikalini ni mwanasiasa na shughuli kuzipeleka kisiasa zitaishia kisiasa na mafanikio yatakaa kisiasa pia nikiwa namaanisha POROJO TU.
 
Tembo wetu wanaishi maisha ya taabu sana huko mbugani.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
NImetoka ss hivi katika mkutano wa CCM nimegundua CCM bila nape hali itakua ngumu'swala la korosho na gesi ni gumu kwa serikali ya chama changu cha CCM,wananchi wa kusini tunauliza kwanini gesi ipelekwe KINYEREZI,GHASIA kajiuma umauma mpaka Nape kaja kumuokoa.kazomea mpaka amepaniki,wanakusini wanataka kujua kwanini huo mtambo uliojengwa KINYEREZI USIJENGWE MTWARA

i hate it when everything is centred in Dar!
 
ccm chukizo sana,,
sasa nimelielewa hili picha,,kwa waliowahi fika mtwara hapo panaitwa makonde beach,,panamilikiwa kwa joint venture ya kijana wa ccm anaitwa maarifa wakishare na police mtwara,,hawa ghasia na mkuchika ndio wahusika na waliofanya kampeni ya kumwingiza mjasiriamali huyu ndani ya ulingo wa siasa hadi kufikia hatua ya kumpa nafasi ya katibu uenezi wa ccm mkoa wa mtwara kwa kura za kishindo ktk uchaguzi huu wa ndani ulioisha hivi karibuni,,
hata rais kikwete alipozuru kule mtwara hili ni eneo ambalo alifikia pia,kwaiyo imekua ni mchezo wa kupeana ulaji na kuzid kutengeneza channel za kupitishia pesa za walipa kodi wa nchi hii
ccm muogopeni mungu

umeona eeh, maskini hatuna chetu kt nchi hii, watu hawamuogopi mungu, wao lao ni kucheza madeal tu, pia kupiga ela
 
CHADEMA huwa wanauzaga nini?Wanachama wao basi wanazo, tatizo la CCM ni kwamba chama ni chawanyonge labda ndo maana wanatoa bure.
Inawezekana ni kweli chama cha wanyonge,lakini swali la msingi hapa ni kuwa hayo mabilioni ya fedha wanayapata wapi?
*Je ni ruzuku ya chama?
*Je ni fedha za kifisadi?
*Je ni fedha za walipakodi zinazotumiwa tofauti na matarajio ya walipa kodi?
==Fungua akili yako na ujadili kwa kina mambo haya na hasa ukizingatia CCM ndiyo chama tawala!
 
Back
Top Bottom