Picha za shule ya msingi Chato; hakika maendeleo hayana chama

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
1581629689168.png


1581629716337.png


1581629737605.png


1581629760913.png


SERIKALI YARIDHISHWA NA MAJENGO YA SHULE YA MSINGI CHATO

Serikali imepongeza hatua ya ujenzi na ukarabati wa shule ya msingi Chato kwa kujenga majengo yanayozingatia ubora na thamani halisi ya fedha.

Hayo yamesema na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga alipofanya ziara shuleni hapo na kujionea majengo mbalimbali na samani zilizowekwa kwenye baadhi ya majengo.

“kazi iliyofanyika inalingana na fedha iliyotolewa kwa hiyo tuendelee kusimamia fedha zinazotelewa katika Sekta ya elimu kwani Serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya kugharmia elimu ikiwa ni pamoja na Elimu Bila Malipo na fedha za Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R), wananchi waendelee kujenga madarasa ili kupunguza uhaba uliopo”

Katibu Tawala Mkoa wa Geita Bw. Dennis Bandisa amesema shule ya msingi Chato imeingia kwenye historia ya nchi yetu kwani Mheshimiwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amesoma kwenye shule hiyo na hilo ni jambo la kujivunia ndiyo maana mkoa na halmashauri umechukua hatua za makusudi kuienzi shule ya msingi Chato.

“sisi tumeona hapa ni mahali pa kujivunia na kuna ujenzi na ukarabati unaendelea, mkoa unashirikiana na halmashauri kuona ni namna gani tutapaboresha hata Mheshimiwa Rais (Dkt. John Pombe Joseph Magufuli) yeye mwenyewe ameunga mkono kwa kujenga baadhi ya majengo (madarasa matatu na ofisi mbili)”

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chato Eliud Mwaiteleke amesema wamekuwa na tatizo kubwa la miundombinu ya elimu katika shule za msingi na sekondari na sasa wamepatiwa fedha ambazo zitasaidia kupunguza tatizo la miundombinu msingi kama matundu ya vyoo, nyumba za walimu, madarasa, ofisi na miundombinu mingine.

“tumepata nafasi kubwa sana ya kupatiwa fedha kwenye ujenzi wa miundombinu, namshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na msituchoke kwa sababu kwenye miundombinu msingi pekee yake tunahitiji bilioni 119 na sekondari tunahitaji bilioni 19 na sasa tunaendelea kupunguza kutoka kwenye lile andiko tulilokuletea (Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI)”

Naye Alphonce Mnyaga Mwenyekiti wa Kamati ya shule ya Msingi Chato akiongea kwa niaba ya walimu na wazazi wa shule hiyo ameshukuru jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kuendelea kuwekeza katika miundo mbinu ya elimu katika shule hiyo na kwamba wao wapo tayari kujitolea kwa hali na mali.

“sisi wananchi wa Chato tunahitaji maelekezo tu kwani kila jambo ambalo linatokea kwa mazingira ya hapa wananchi wakishirikishwa jambo hata kama la kujitolea kama taarifa inavyojieleza wanaweza lakini pia ni wakarimu sana”

Awali akisoma taarifa ya shule ya msingi Chato A na B Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Chato A Bw. Honest Theobald amesema jumla ya shilingi milioni 389 na laki sita na nusu zilitolea kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 13, matundu 40 ya vyoo, ujenzi wa uzio wa shule, vyumba vitatu vya madarasa na ofisi mbili zilizojengwa na Mhe Rais na ununuzi wa samani ambapo nguvu za wananchi (force account) pia zilihusishwa.

Aidha, Bw. Theobald amesema changamoto kubwa shuleni hapo ni idadi kubwa ya wanafunzi ambayo inafikia 4,073 na pia kuna upungufu wa vyumba 31 vya madarasa.

Katibu MKuu Mhandisi Joseph Nyamhanga yupo ziarani mkoani Geita kujionea utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika miradi mbalimbali na utoaji wa huduma kwa wananchi.
 
Rais Magufuli achangia madarasa matatu na ofisi ya walimu baada ya kutembelea Shule ya Msingi Chato ambayo alisoma.

 
Wakarabati na shule zingine nchi nzima!

Watoto wote wanastahili kusoma kwenye mazingira mazuri na salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli.
Rais amesoma hapo na amechangia ujenzi wa madarasa matatu. Tujifunze kukarabati shule za msingi na sekondari tulizosoma. Tumekazania kuwa na groups za WhatsApp tuliosoma msingi, sec lkn hakuna la maana huko tunakusanyana tu bila kuwa na malengo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapo jiwe hajafanya kosa
mi sipendi kuona shule na ofisi za serikali zimechoka


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ni kweli.
Rais amesoma hapo na amechangia ujenzi wa madarasa matatu. Tujifunze kukarabati shule za msingi na sekondari tulizosoma. Tumekazania kuwa na groups za WhatsApp tuliosoma msingi, sec lkn hakuna la maana huko tunakusanyana tu bila kuwa na malengo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa. Ni jambo jema kuchangia ila sio lazima!

Serikali inachukua kodi matrilion ya shilingi kwa ajili ya kazi hiyo! (Kujenga na kuboresha miundombinu).

Hiyo "Rais kuchangia" sijui ni hisani au alitoa fungu lililoidhinishwa rasmi!?

Hata hivyo, kafanya vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom