Uchaguzi 2020 Picha: Ukumbi wa Mlimani City ukiwa tayari kwa Vikao vya Maamuzi CHADEMA kuanzia kesho, taratibu za kujilinda na COVID-19 zimezingatiwa

Wakuu sijui kwanini moyo wangu unakuwa mzito hivi, nina wasiwasi hawa wajumbe hasa mikoani wanaweza kupindua meza wakampa Nyalandu.

Aisee ikifika stage hiyo ni heri udikteta utumike wakuu apite Lissu kipenzi cha watanzania.
Kama wajumbe wataamua nyalandu apewe, ndo demokrsia.ila Jpm ataenda kulala, maana uchaguzi utakuwa umekwisha
 
Hatimaye dimba limekamilika kwa ajili ya vikao vya kuanzia hapo kesho. Kila kitu kimezingatiwa ikiwemo taratibu za kujikinga na Corona.

Picha za awali zilizotumwa (Isipokuwa ya meza kuu ambayo inajumuisha viongozi wakuu wa chama) ni za vikao vilivyowahi kufanyika siku za nyuma yaani vya Uchaguzi wa viongozi ndani ya chama.

View attachment 1525198

Mkuu. Naomba nikumbushe. Ile habari ya ndege za Tanzania kutotua kenya kwa kuwa kenya inajitambua. Hawana unafiki imeishia wapi. Mana wengine nyuzi zao hawaletagi feedback. Ndo mana nimekimbilia kwako mkuu. Samahani kwa usumbufu.
 
Cdm haikuazishwa jana, imepitia mikutuo kibao na hasa mikutuo ya kuanzia mwaka 2015 hadi sasa.

Kingekuwa chama cha kuokoteza kingesha jiunga na kina TLP, NCCR, CUF, NLD,
Najua unathamini mchango wa EL 2015. Ila mwaka huu wabunge wakizidi Sana Saba.
 
Kwa Mara ya kwanza CDM wanafanya hivi katika chaguzi za Urais... Tuone matokeo yatakavyo kuja na Kama watabaki wamoja.
Kwa kura za Urais matokeo yanajulikana. Tayari WAJUMBE wanaingia na jina la mtu wao walioelekezwa. Kwa wiki nzima tumewasikia na tumewaelewa. Hata wagombea wenza hilo wanalijua wanaona aibu kujitoa😂😂😂
 
Naomba kujuzwa, je pana hoteli/gesti nzuri karibu na mlimani city? kama zipo, majina ya hoteli na hadhi zake tafadhali.
Mlimani City si mbali sana na Sinza huko Kuna Guest za kila rangi
 
Mlima I City si mbali sana na Sinza huko Kuna Guest za kila rangi

Asante Sky Eclat Je hizo hoteli/gesti za sinza unaweza kwenda mpaka mlimani kwa mguu au itahitaji bodaboda maana mie kutembea mwendo mrefu siwezi. nitashukuru ukanipa jina la hoteli iliyo karibu sana na mlimani city.
 
Back
Top Bottom