Mwenyekiti wa CHADEMA Shinyanga asimamishwa Uongozi kwa muda wa mwaka mmoja kwa tuhuma za utovu wa Nidhamu

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Mwanza. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi na Katibu wake, Emmanuel Buyamba wamesimamishwa uongozi kwa muda wa mwaka mmoja kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.

Taarifa kwa umma iliyosainiwa na Katibu wa Kamati ya Uenezi Chadema Kanda ya Serengeti, Golden Marcus imesema uamuzi huo umefikiwa kupitia kikao cha Kamati Tendaji ya Chadema Kanda ya Serengeti kilichoketi Aprili 28 hadi 29, 2023.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Mei 2, 2023, Marcus amethibitisha usahihi wa taarifa hiyo ya Aprili 30, 2023 akisisitiza kuwa wawili hao wamezuiwa kujihusisha na shuguli zozote za kiuongozi kuanzia Aprili 29, mwaka huu.

Amesema kwa sasa, nafasi ya uenyekiti wa mkoa utakaimiwa na Mwidini Mpagano ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee (Bazecha) huku nafasi ya Katibu ukikaimiwa na Katibu Baraza la Wanawake (Bawacha) Mkoa wa Shinyanga, Agatha Mamuya.

Bila kuwa tayari kutaja sababu za vigogo hao wa chama kusimamishwa, Marcus amesema; “Taratibu za chama zinatoa fursa kwa wahusika kukata rufaa dhidi ya maamuzi haya ndani ya siku 30….naamini wote watatumia haki hiyo kwa sababu ni viongozi na wachama wazoefu na walishirikishwa katika vikao halali hadi hatua kwa hatua kabla ya uamuzi wa mwisho,”

Ingawa taarifa ya viongozi hao kusimamishwa haikutaja sababu, vyonzo vya kuaminika vimeieleza Mwananchi kuwa Ntobi na mwenzake wanakabiliwa na tuhuma kadhaa ikiwemo kukiuka katiba ya chama, kukaidi maagizo, maelekezo na maamuzi ya vikao na kuibua taharuki ndani ya chama kwa kutoa kauli zinazowavunjia heshima viongozi wenzao.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Mei 2, 2023, Ntobi amesema hajapkea barua rasmi kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi yake zaidi ya kuziona kupitia mitandao ya kijamii.

“Ninachofahamu ni kwamba nilitengenezewa mashtaka ya uongo na uzushi kwa lengo la kunichafua na kushusha heshima yangu; sikupata nafasi ya kusikilizwa,” amesema Ntobi

Huku akihusisha suala hilo na ajali za kisiasa, Ntobi amewasihi wana Chadema Mkoa wa Shinyanga kuwa watulivu kwa sababu chama chao ni taasisi imara inayohimili na kuvuka salama mawimbi yote ya kisiasa na kuendelea kuwa imara zaidi.

"Kwa sasa sina maoni mazuri zaidi kuhusu suala hili kwa sababu bado sijajua sababu wala kifungu gani cha Katiba ya chama kilichotumika kuniadhibu. Nitakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumza baada ya kupokea barua rasmi ya kusimamishwa uongozi,” amesema Ntobi.
 
Kwasasa kukaa kwenye Chadema kama kutafuta msongo wa mawazo tu. Ntobi kama anapitia humu sas ni muda wake kujiunga na CCM tutampa kata ya N'gokolo au Bushushu. CHADEMA kwasasa hipo mikononi mwa Yuda akina Lema,Msigwa,Mbowe,Wenje et al wanakula pesa za ruzuku,kila wakifanya mikutano sehem lazma wachukue wadada,pombe nk. Mwisho ni kwamba tuliwaambia kua CCM aiwezwi na vyama vinavyo ongozwa na watu wenye tabaa na pesa.
 
Aiwezi = haiwezi
Tabaa= tamaa
Yule mbunge aliyepata ajali juzi pale dodoma alikuwa anatoka wapi?
Chadema wametajwa ukurasa wa ngapi kwenye report ya CAG???
 
Cha ajabu nn hapa
Mtavangu yupo wapi?
Sophia simba yupo wapi?
Bernard membe yupo wapi
Wasira yupo wapi
Waitara mwita yupo wapi?
 
Huu ugatuzi wa madaraka Chadema nimeukubali. Ngazi za mikoa/wilaya ziwe handled na Kanda. Safi sana.
 
Kwasasa kukaa kwenye Chadema kama kutafuta msongo wa mawazo tu. Ntobi kama anapitia humu sas ni muda wake kujiunga na CCM tutampa kata ya N'gokolo au Bushushu. CHADEMA kwasasa hipo mikononi mwa Yuda akina Lema,Msigwa,Mbowe,Wenje et al wanakula pesa za ruzuku,kila wakifanya mikutano sehem lazma wachukue wadada,pombe nk. Mwisho ni kwamba tuliwaambia kua CCM aiwezwi na vyama vinavyo ongozwa na watu wenye tabaa na pesa.
Kweli kabisa
 
Hiki chama ni cha wahuni, wanasema ukikipeleka chama mahakamani ni kujifukuza uanachama halafu wanasema wakakate rufaa au hy rufaa inakatwa kwenye chama chao wenyewe.?
 
Back
Top Bottom