Picha: Samuel Sitta amenihuzunisha

Picha: Samuel Sitta amenihuzunisha

Hapo mwisho umejijibu mwenyewe! Siyo kwamba tunadharauliwa na Jirani zetu wa EAC tu bali hata huku Kusini hatuna ushawishi tena wa enzi hizo za Mwl. Nyerere. Wachawi ni sisi wenyewe tusimtafute mchawi nje ya Tanzania. Tusiendelee kuishi kwa nyota ya Mwl. Nyerere wakati tunachagua watawala wa hovyo na wajinga!

Nyerere ni sehemu ya hili tatizo, soma Historia pande zote mbili - hawa wote unaowaona sasa hivi kwenye CCM na serikali katika ngazi za juu ni vijana wa TANU Youth League!!
 
Hapo napo kajitakia..........si angebaki tu kwa Magreth akajipumzikia.
 
Kwani ugonjwa wa mkuu wa kaya haumuruhusu kutembea safari ndefu.
Basi tutaokoa pesa nyingi.
 
Nyerere ni sehemu ya hili tatizo, soma Historia pande zote mbili - hawa wote unaowaona sasa hivi kwenye CCM na serikali katika ngazi za juu ni vijana wa TANU Youth League!!

Nyerere ndiye anatuchagulia hawa jamaa?
 
Hizo ni mind games tu wakuu hakuna haja ya kusononeka sana.
 
10410297_824822447577597_4592484584682590232_n.jpg

Hii picha kila nikiiangalia na nikimuangalia Mh Samuel Sitta anavyowaangalia wenzake kwa hasira baada ya kumtenga kwenye majani na kwenye kiti cha peke yake wenzake wako kwenye red carpet roho inaniuma, kama mbwai mbwai tu na ndoa ivunjike

Duh! Hii picha nzito sana. Yawezekana hawakumaanisha, ila kwa sisi wengi inatuletea meseji ya ajabu.
 
Uhuru amekaa kama ZUZU. Sitta kama PIMBI.

Sidhani kama kuna haja kuitafakari hiyo picha sana. Hatuelewi nani mkosaji. Vipi ikiwa ni Sitta alichelewa, kama ilivyo kawaida ya maCCM?
 
Duh! Hii picha nzito sana. Yawezekana hawakumaanisha, ila kwa sisi wengi inatuletea meseji ya ajabu.

Barafumoto....Wataalamu wa saikolojia na biolojia walitafiti kujua yaliyomo moyoni mwa mtu [MINDS] kama HAONGEI je tutajuaje nini kinaendelea kichwani kwake.Watafitihao wakaibuka na kitu kinaitwa BODY LANGUAGE.

Tunachokiona hapo kwenye picha hiyo ni BODY LANGUAGEYA KILA MKMOJA WAO NA MATENDO KUPITIA MATERIALS HIZO ZILIZO WAZUNGUKA.

Ukitizama kuanzia material alizokalia Mzee Sita na Setting ya kiti chake, njoo utizame body language ya Mzee Sitta HAYUKO COMFORTABLE na eneo husika.Lakini tizama kaa ya wenzie na setting yao ya ukaaji na BODY LANGUAGE utaona dhahili wako Shwari na hali hiyo ya upiga picha huo.Hivyo hoja yako mkuu hapana ...........wachina wao wakaenda mbali wakasema picha huwa inaongea,hivyo tunavyoina na kuitolea tafsiri ndicho kilichotekea hayo mengine Mbwembwe.
 
Dhambi ya kuwasaliti watanazania.
Ila tunatakiwa tujue kuwa alikuwa anawakilisha Tz, sidhani kama alienda kama yeye au chama. Ila kama alikuwa anawakilisha chama, POA tu, hata kwenye mkeka wangemkalisha tu!
 
Hapo mwisho umejijibu mwenyewe! Siyo kwamba tunadharauliwa na Jirani zetu wa EAC tu bali hata huku Kusini hatuna ushawishi tena wa enzi hizo za Mwl. Nyerere. Wachawi ni sisi wenyewe tusimtafute mchawi nje ya Tanzania. Tusiendelee kuishi kwa nyota ya Mwl. Nyerere wakati tunachagua watawala wa hovyo na wajinga!

Na wanavyojua kusafiria nyota ya Nyerere hawa wanafiki utashangaa, kila inapokaribia uchaguzi au jambo muhimu wanajidai kumuenzi na kutangaza hotubavza mwalimu, wapuuzi sana.
 
Ila tunatakiwa tujue kuwa alikuwa anawakilisha Tz, sidhani kama alienda kama yeye au chama. Ila kama alikuwa anawakilisha chama, POA tu, hata kwenye mkeka wangemkalisha tu!

Kwani huwa wanajali wao mambo muhimu ya taifa hili, ona walivyoharibu katiba wakiongozwa na hili nafiki. Wangelipa choo likalie, ndio linastahili.
 
Guys...naona kila mtu analalamika hapa kuhusu mzee Sitta. Sitta kaomba kupiga picha na hiyo delegate...the only option was for him to move with his chair na akajibanza hapo. Wageni wote walikuwa na type ya viti vya Sitta except marais
Kabla ya kulaumu tuwe tunajiuliza kwanza!!

we acha masihara huyo wa kulia ni rais wa wapi na huyo mwana mama ni rais wa wapi hapo marais watatu tu na viti vitano why tanzania tukalishwe kwenye majani
 
View attachment 210433
HUYU NI BABU YAKE NA SAMWEL SITTA ALIKUWA ANAITWA MTEMI SAID FUNDIKIRA AKA SULTAN SAID

''Alitawala kuanzia mwaka 1917 mpaka 1927. Alifanikiwa kuwashawishi watemi wengine wa kanda ya magharibi kuchanga pesa, mifugo na mali nyingine ili kupata pesa za kujenga shule mbili za Tabora Boys na Tabora Girls.

Na yeye akatoa ardhi ya kujenga shule hizo kwa kuwa eneo hilo lilikuwa chini ya himaya ya Ikulu ya Unyanyembe. Vile vile Mtemi Said alikuwa mkarimu mno kiasi kwamba mtu akiunguliwa na nyumba yeye alimjengea nyumba mpya na kumpa chakula cha kumtosha kwa mwaka mzima.
...............................................

Yeye aliondolewa madarakani na wakoloni wa kiingereza baada ya kuwa hapeleki serikalini kodi aliyotoza wananchi, inasadikika alitumia pesa hizo kusaidia masikini. Hivyo kwa heshima na upendo aliyokuwa nao kwa wananchi wake wakoloni wa Kiingereza walilazimika wasimfunge jela ila walimuondosha Itetemia na kiti chake akakitwaa Mtemi Kiyungi II huyu alikuwa mtoto wa Mtemi Isike Mwana Kiyungi.''

Hivi Jeuri ile ya Fore Fathers [Ancestors] Kama hawa ilipotelea wapi jamani hizo damu zimebadilika vipi tunapitia hatua kama walizopitia Wahenga huku tushakuwa huru toaka 9/dec/1961. Wao pasipo Uhuru hawakukubali KUMNYENYEKEA MKOLONI..........IWEJE LEO MZEE SITA NA VIONGOZI WENGINE TUKO HURU TUNAPOTEZA HESHIMA!!!!!!!!!!!!
Nyerere akiwa kijana kabisa aliwahi kubishana na Kwame Nkrumah hadharani kutetea msimamo wake kwenye mambo kama haya ya intergration na akashinda,na kuna story tunasikia kuwa malkia alivaa groves kumsalimia na JK (original) akampa kifimbo sijui kama ni kweli,hata kama sio kweli but hiyo yote ni kutaka kuonyesha jinsi utawala wa Nyerere ulivyokuwa na ile jeuri ya kutopenda manyanyaso hata kama ni masikini
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Yaani mkiambiwa hao CoW ni wabaguzi mnabisha.Sasa hebu ona hata kiti tu wamempa cha rangi tofauti na wenzie.Yeye wamemuweka kwenye majani.Hii kitui shauri yao.SittA Akiwa Raisi au waziri mkuu uchaguzi wa mwakani hivi nyuso zao hao wakenya watazipeleka wapi? S i ndio itakuwa Tanzania inasema bye bye EAC?

Huyo mtu wa protocol wa Kenya INABIDI AFUKUZWE KAZI.Picture kwa tuliosomea kwa undani mambo ya picture reading it speaks a lot.
 
Guys...naona kila mtu analalamika hapa kuhusu mzee Sitta. Sitta kaomba kupiga picha na hiyo delegate...the only option was for him to move with his chair na akajibanza hapo. Wageni wote walikuwa na type ya viti vya Sitta except marais
Kabla ya kulaumu tuwe tunajiuliza kwanza!!
EAC nchi zipo tano, viti vya kwenye zuria vipo vitano. Sasa huyo mwingine huko mwishoni aliekalia kiti cha mwakilishi wa nchi tuseme yetu ni nani? Yaani ni dharau za wazi kabisa dhidi ya Tanzania. Putini wa Urusi haki ya nani asingekubali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom