Ni sawa mkuu unavyomtetea lakini kusema ukweli muheshimiwa kazidi kwa safari hutulii nyumbani kila siku kiguu na nchia kama ni suala la kutafuta misaada ya kujenga nchi yake mbona hao anaokwenda kuomba msaada kwao ndio wanaokuja kuchukua rasilimali zetu na kwenda kujengea mataifa yao ni kwanini asikae chini akafikiria ni jinsi gani anaweza kutumia rasilimali za nchi yake kujenga taifa lake? Mbona kina kibaki wa kenya na hata mseveni wa uganda hatuwaoni wakisafiri hovyo hovyo kama yeye kulikoni au ndio njia ya kuchuma kwa per diem kwa sababu akisafiri kunaposho kwa hiyo walikini ndio njia yake na yeye ya kujipatia posho kwa safari lukuki.Tujifunze kutoka kwa wenzetu juzi masalani raisi wa brazili alikuwa anahudhuria kikao nje ya nchi akapata taarifa kuwa kuna maafa yametokea nchini mwake watu 230 wamefariki kwenye ukumbu wa disco lakini alikatisha safari akarudi nchini kwake kushuhulikia matatizo ya nchi yake je huyu wakwetu alishawahi kufanya hivyo? Tusimtetee tu eti kwa kuwa ni wana CCM la hasha kwenye ukweli tuseme ukweli yaliyotokea mtwara si madogo alitakiwa awepo akayashuhulikie lakini wamekaa kimya kama hakuna lililotokea juzi ndio pinda kajibaraguza anakwenda mtwara kuzungumza na wana mtwara sasa hihi ni nini tuko serious kweli na ustawi wa taifa letu?
Mkuu,
Kwa swala la Mtwara tuko wote kabisa, lakini kumbuka serikali ilikuwa tayari imeboronga na hata hako ka kitengo ka Mh. Wassira kanakohusika na mahusiano kati ya serikali sijui kanafanya kazi gani.
Swala lilikuwa tayari limekuwa la moto kwa pande zote mbili yaani wizara ya nishati na madini na wanaMtwara. Kitengo cha mahusiano kilikuwa kinatakiwa kifanye kazi yake kwanza, kwa maana kuwa, wajue nini hasa tatizo na njia ya kulikabili, badala yake wakawa kimya. Siamini kama Mh. wassira anafaa katika hiki kitengo kwa sababu hata swala la Mwanza limemshinda. Kitengo chake kinasubiri tatizo litokee ndipo kifanye kazi badala ya kunusa tatizo kabla halijatokea na kuanza kulifanyia kazi mapema. The guy is incompetent at the highest level.
Serikali ya CCM ilishajifunza madhara ya kumtanguliza Rais kwanza katika matatizo kabla ya kuhakikisha kama heshima ya ofisi ya Rais itawepo pale anapoamua kwenda. Refer Rais Mwinyi wakati wa uchaguzi wa mbunge Temeke. Kwa hiyo ninaamini hilo lilichukuliwa umuhimu wa juu, ndiyo maana imebidi Waziri mkuu atangulie kwanza pamoja na kwamba alitakiwa afanye hivyo mapema.
Kutorudi kwa Rais ni kwa sababu hiyo niliyoieleza hapo juu, kwa sababu kama angekatisha safari bado angetakiwa aje na kwenda moja kwa moja Mtwara.
Labda kitu kingine hatukifahamu, ni feedback gani alipewa na watu wa usalama wa Taifa, polisi na wizara ya nishati na madini kuhusiana na kilichokuwa kinaendelea Mtwara.
Ni rahisi sana kurusha lawama lakini pia tunatakiwa tuangalie picha kwa mapana.
Kwa swala la safari kuwa nyingi, hili mkuu inabidi tukubali kutokubaliana. Yaani Rais wa nchi atengeneze safari ili apate posho. Cummon brotha, this is too low. Kwa point yako hii kama ni kweli basi maneno na debate ya kuwa Rais Kikwete ni fisasi yatakuwa antiquated.