Hongereni sana Fastjet, nyinyi ni wafanyabiashara kabisa. Na ndivyo inavyopaswa. Fastjet wanabadilika kulingana na Mazingira, Nyakati na Mahitaji.
ATCL kamwe wasijaribu kuwaiga Fastjet katika mikakati yao, kwa sababu..
1/Fastjet hapa Tanzania ni sehemu tu ya Fastjet "international" ambayo iko katika nchi kadhaa Afrika, Ulaya nk. Wana mtaji mkubwa, wana uzoefu wa biashara hiyo katika kona tofauti, wana link pana sana na makampuni mengine ya Ndege duniani.
2/Wakati wowote biashara ikiyumba hapa Tanzania, Fastjet wanaweza kuondoka na kwenda nchi nyingine kufanya biashara pasipo kutikisika kwa mtaji wao wa kibiashara.
3/Wakati wowote ule, Fastjet wanaweza kuongeza ndege au Kupunguza, kubadilisha aina ya ndege zao au kuboresha huduma ndani ya ndege zao pasipo kuathirika kimtaji, kwa sababu kampuni mama ya Fastjet iko katika nchi nyingi tena ikiwa na utitiri wa ndege.